Mtazamo wa haraka haraka juu ya Aqida tukufu ya Kiislam,yabainisha kuwa ni Aqida pana,yenye kujumuisha mafungamano mawili muhimu.
Kwanza: FUNGAMANO LA KIROHO
Hili ni fungamano baina ya mja na Mola wake.Lenye kumuongoza mwanadamu sehemu hizi:A) Mafungamano baina ya mja na Mola wake.Kama kuswali,kufunga,kuleta dhikr nk .B)Mafungamano baina ya mja na nafsi yake.Kama kula,kunywa na kuvaa.Sehemu hii ya kwanza,Ahkam husika zaweza kutekelezwa bila Khilafah Rashidah kwa kiwango fulani.Japo,hata kiwango hicho pia,hakuna dhamana ya kutekelezwa kisawa sawa.
Mifano mizuri,ni namna ya sehemu hii,ikiwa haina Khilafah(DAULA)inavyoyumbishwa chini ya mfumo wa kitwaghuti:Ubepari Demokrasia,ni wakati wa kuibuka kwa gonjwa la COVID-19!Ambapo Waislam na wengine,walipigwa marufuku kuhudhuria majengo ya Ibada kama miskiti.Isitoshe,waliporuhusiwa kuhudhuria,pia Ibada hio,ilitolewa muelekezo mpya ya jinsi ya kuitekeleza,kinyume kabisa na muongozo wa ALlah Swt,na Sunnah ya Ar Rasul.
Mfano hai wa hivi karibuni,ni maamuzi ya mahkama ya upeo nchini Kenya,juu ya suala la kurithi mwanaharamu.Mahkama hio,ilitoa maamuzi kuwa,wanaharamu,au watoto walozaliwa njee ya ndoa,wana haki sawa ya kurithi.Kinyume kabisa na mafunzo matukufu,yenye kutoka kwenye Aqida sahihi ya Kiislam.Ambayo mafunzo yake,yatufundisha kuwa kuna vizuizi vya kurithi.Ikiwemo mtoto wa zinaa, mtu kushiriki ktk mauaji ya marhum.
Kutofautiana Aqida(Dini):Aqida hii,mafunzo yake yenda sambamba na umbile la mwanadamu.Juu ya kumpa muongozo wa kina ktk kila njia za maisha,bila mapendeleo wala mgongano wowote!Mafunzo ya Aqida hii,yafundisha mtu,kwa kuwa ameumbwa na hisia ya kuvutiwa na kiumbe cha pili,ili kuikidhi hisia hii na kuishibisha vilivyo,basi awe ni mwenye kuingia ndani ya fungamano jema la ndoa sahihi!
Tofauti na mfumo wa kikoloni:Ubepari na nidhamu yake ya kisiasa ya Kidemokrasia,ulokuja kufungua mlango wazi,kwa kuruhusu muozo wa jamii kama LGBTQ+! Matokeo yake leo kukawa na kuna watu walisha,wasomesha na kugharamikia watoto,ambao si watoto wao kidamu! Na linalotarajiwa,ni kuwa wanapokufa,mali hio watarithi wao na watu wengine ambao si damu yake.Ikiwakosesha fursa ya kurithi watu wake wa nasaba!Ambao wana haki zaidi ya mali hio,kuliko watu wengine.Hii ikiwa dhulma ya wazi.Hivyo,funzo ktk kuzuiwa mtoto wa zinaa kurithi,ni njia moja ya kuepusha zinaa ktk jamii.Ambapo mwanadamu atalazimika kuoa,ili mwanawe arithi.
Kando na kumuekea adhabu kali mzinifu. Ni kweli kwamba Mahakama ya Juu ya Kenya,imetoa uamuzi kwamba watoto waliozaliwa njee ya ndoa,na baba Waislamu wana haki ya kurithi mali ya baba yao.Uamuzi huu wa kihistoria ulitolewa tarehe 30 Juni 2025 katika kesi ya Fatma Athman Abud Faraj dhidi ya Ruth Faith Mwawasi na wengine 2 (SC Pet. E035/2023), mahakama hiyo, ilithibitisha uamuzi wa awali wa Mahakama ya Rufaa.
Mahakama ya Juu ilisisitiza kuwa kuwatenga watoto hao katika masuala ya urithi ni aina ya ubaguzi usio wa haki na ni ukiukaji wa kanuni ya kikatiba ya kutokubagua.Mahakama ilieleza kuwa watoto wote,bila kujali hali ya ndoa ya wazazi wao, wanapaswa kutendewa sawa kisheria katika masuala ya urithi na usimamizi wa mali.Uamuzi huu, umeweka mfano wa kisheria wa lazima (binding precedent), unaohakikisha kwamba watoto waliozaliwa njee ya ndoa,wana haki sawa za kurithi.Hata katika kesi zinazotawaliwa na sheria ya Kiislamu,ambayo kwa kawaida imekuwa ikirithisha watoto waliotokana na ndoa rasmi pekee.Mifano hii,yatubainishia wazi kuwa,bila Khilafah Rashidah,kuzilinda Sharia za ALlah Swt,basi hata sehemu hii ya kwanza,huwa ni yenye kubomolewa rahisi, kisha kwa kalamu tu.Wacha risasi na mizinga!
Sehemu ya pili ya Aqida ya Kiislam ni:
2)FUNGAMANO LA KISIASA
Fungamano hili,lamuongoza mwanadamu ktk nyanja za maisha yake yote:
A)KIUCHUMI
B)KIJAMII
C)KISIASA
D)KIELIMU
E)SIASA ZA NDANI NA JEE ZA KHILAFAH
Fungamano hili,pamoja na lile la kwanza,haliwezi kutekelezwa kikamilifu bila Khilafah Rashidah kulinda hukmu zake.Kukosekana kwa Khilafah Rashidah, Ahkam hizi,hubaki kwenye kurasa za vitabu,na rafu kwenye kuta za majengo.Hata kama Ahkam hizo,ni nzuri na zavutia vipi,zitabaki nadharia bila kuwa na uwezo wa kutekelezwa
Ndio ALlah Swt Akatwambia ktk Qur’an:
ٱلَّذِينَ إِن مَّكَّنَّٰهُمْ فِى ٱلْأَرْضِ أَقَامُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتَوُاْ ٱلزَّكَوٰةَ وَأَمَرُواْ بِٱلْمَعْرُوفِ وَنَهَوْاْ عَنِ ٱلْمُنكَرِ ۗ وَلِلَّهِ عَٰقِبَةُ ٱلْأُمُورِ(الحج:٤١)
“Wale ambao tukiwapa nguvu katika nchi,wataisimamisha Swalah,na kutoa Zakaa, na kuamrisha mema,na kukataza mabaya.Na kwa ALlah ndio maregeo ya mambo yote.”
(Al-Hajj: 41)
UFAFANUZI WA HII AYAH!
1)Tukiwapa nguvu(mamlaka/madaraka) katika nchi
Wanapopewa serikali yenye mamlaka,nguvu za utawala au uwezo wa kuongoza katika jamii.
2)Watasimamisha Swalah
Watahakikisha kuwa Waislam wote walobaleghe,waswali.Na wasoswali,basi hatua za kisharia zitatekelezwa kwao.Wala sio kuifunga miskiti na kuwazuia waumini kuswali! Masikitiko zaidi,hilo latekelezwa,kwa kunyenyekea maagizo ya matwaghuti!
3)Kutoa Zakaa
Watasimamia zoezi zima la ukusanyaji,uhifadhi na ugavi wa zakaa,kwa mujibu wa Sharia.
4)Kuamrisha mema.
Wanahimiza wengine kufanya matendo mema, kwa maadili na maagizo ya Kiislamu.
5)Kukataza mabaya
Wanazuia uovu, uadhalilishaji,na mambo yanayopingana na maadili ya Dini.
الَّذِينَ كَفَرُوا بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ إِلَّا تَفْعَلُوهُ تَكُن فِتْنَةٌ فِي الْأَرْضِ وَفَسَادٌ كَبِيرٌ
“Wale waliokufuru ni wasaidizi wa wao kwa wao. Msipofanya hivyo patakuwa na fitna katika ardhi na uharibifu mkubwa.”
Kwa maana kukosekana kwa Khilafah Rashidah,ndio chimbuko la fitna na uharibifu duniani pote.Kama inavyoshuhudiwa leo! Ndio Uthman bin Affan ra akasema:
إن الله ليزع بالسلطان ما لا يزع بالقرن
“Hakika Mwenyezi Mungu huzuia(munkar/maovu) kwa(nguvu za) mamlaka serikali kile kisichozuilika kwa(waadhi mtupu wa) Qur’an.”
Kwa maana haya alikuwa RA akitutanabahisha kuwa:
1.)Ufaradhi wa kuwepo serikali Ya Kiislam Kwa kuwa,Khilafah Rashidah pekee,ndio yenye uwezo wa kuzuia machafu au maovu,na kusimamisha mema.
2)Kisichozuiwa na Qur’an
Licha kuwa Qur’an ni muongozo mzuri kwa mwanadamu,kuna mambo ambayo Qur’an inayoamrisha au kukataza,lakini baadhi ya watu hawazingatii kwa kukosekana nguvu za kutekeleza amr hizo. Mfano wa hili ni pale Qur’an inapoamrisha,kuhukumiana kwa Ahkam zake.Lakini kukosekana serikali halisi ya Kiislam,watu bado wafuata kanuni za kibinadamu,kando na za Qur’an!Hivyo serikali ya Khilafah pekee,ndio yenye haki ya kutumia nguvu kuwafanya wafuate Ahkam Za ALlah Swt.
3)Khalifah Uthman ra alionyesha utenda kazi wa utawala halisi wa Kiislamu:
Kama alivyosema As Swabaha bin Sawaada Al Kindiy:
وقال الصباح بن سوادة الكندي : سمعت عمر بن عبد العزيز يخطب وهو يقول :
(الذين إن مكناهم في الأرض ) الآية ، ثم قال : إلا أنها ليست على الوالي وحده ، ولكنها على الوالي والمولى عليه ، ألا أنبئكم بما لكم على الوالي من ذلكم ، وبما للوالي عليكم منه؟ إن لكم على الوالي من ذلكم أن يؤاخذكم بحقوق الله عليكم ، وأن يأخذ لبعضكم من بعض ، وأن يهديكم للتي هي أقوم ما استطاع ، وإن عليكم من ذلك الطاعة غير المبزوزة ولا المستكرهة ، ولا المخالف سرها علانيتها
Aswabaḥ bin Sawadah al-Kindiy,alisema:
“Nilimsikia ‘Umar bin ‘Abd al-‘Azīz akihutubu akisema:
‘Wale ambao tukiwapa mamlaka katika ardhi’ (Aya).
Kisha akasema:
Aya hii haimhusu mtawala pekee, bali inamhusu mtawala pamoja na raia.
Jee,nikwambieni haki zenu juu ya mtawala,na haki za mtawala juu yenu?
Hakika haki yenu juu ya mtawala ni hii:
1)Awahasibu kwa haki za ALlah Swt zilizo juu yenu.
2)Achukue haki ya mmoja wenu kutoka kwa mwingine (kwa uadilifu).
3)Awaongoze kwenye njia iliyo nyofu kadri ya uwezo wake.
Na juu yenu kumhusu mtawala ni hii:
1)Kumtii kwa utiifu wa kweli.
2)Si kwa shingo upande,kushurutishwa wala kulazimishwa.
3Wala msiwe na tofauti kati ya yale mnayoyasema hadharani na yale mliyoficha moyoni.”
Khilafah Rashidah pekee,ndio nyongeza muhimu ya ulinzi wa mafundisho ya Qur’an na Sunnah.
Qur’an inatoa miongozo ya kiroho na siasa, lakini utekelezaji wa sharia kwa nguvu (kama adhabu za hukumi,mamlaka ya askari)ndiyo huizuia uovu kwa ufanisi zaidi katika jamii.
Kama ambavyo,mfumo wa kibepari,licha kuwa wadhihirisha mapungufu na dhulma ulimwenguni kote,lkn kanuni zake chafu hufuatwa na kunyenyekewa,kwa kuwa kuna askari na jeshi,kuhakikisha kanuni hizo zafuatwa.Hivyo,walofahamu Uislam vyema kama Ibn Taymiyyah,katika kitabu chake “As-Siyaasah ash-Shar’iyyah” (Siasa za Kisharia),asema kuwa maneno haya ya Uthman bin Affan ra, yanalenga kudumisha amani na haki katika jamii.Kauli hii,si kudharau Qur’an.Bali yaonyesha kuwa serikali halisi ya Kiislam,KHILFAH RASHIDAH,ni zana muhimu kwa kutekeleza amri zake.
MWISHO:
1)Ahkam na sharia za ALlah Swt,hazina hifadhi wala kinga chini ya mfumo wa kikoloni, ubepari demokrasia
2)Wale walokuwa wakisema au kuamini kuwa uhuru wa kuabudu wawapa Waislam uwezo wa kutekelezwa Ibada zao kikamilifu,matukio haya na mengine,yafaa kuwa funzo la kuwatoa taka masikioni!
3)Chini ya mfumo wowote,kando na Uislam,heshima,hadhi na mali za Waislam,ziko rehani mikononi mwa mataghuti,na hutairishaa kila wanapojisikia,na namna wamavyojiskia!
4)Ahkam Za ALlah Swt,pamoja na Sunnah za Ar Rasul saw,zitapata hifadhi,kuheshimiwa na kutekelezwa kivitendo,chini ya utawala halisi wa Kiislam: KHILAFAH RASHIDAH itakayo kusimama hivi karibuni.
Hussein Muhammad
Mwanachama wa Hizb-ut-Tahrir Kenya.