Kenya tarehe 12 Disemba 2018 ili sherehekea Siku ya Jamhuri ili kuadhimisha Miaka 55 tangu kupata “Uhuru Bandia” tarehe 1 Juni 1963. Ukweli ni kwamba Ufalme wa Uingereza ulibadilisha tu wasimamizi wa shamba “koloni” lake Kenya kutoka kwa Gavana Malcolm Macdonald- mzungu hadi kwa Rais Jomo Kenyatta –muafrika. Raisi Jomo Kenyatta alikabidhiwa nyenzo za mamlaka na Prince Philip, mumewe Malikia Elizabeth II. Malcolm Macdonald alirudi tena Kenya na kuwa Kamishna Mkuu wa Uingereza wa kwanza. Na alipokufa Jomo Kenyatta –Prince Charles mtoto wa Malikia Elizabeth II alikuweko mazishini kama asante kwa kazi nzuri! Kila kitu ikiwemo sera na mipango inayotumika kuendesha shamba la mkoloni “Kenya” zimebakia zile zile hadi leo isipokuwa tofauti ni rangi za wasimamizi tu kutoka kwa wazungu hadi waafrika. Ili tufahamu hilo tutataja mifano baadhi tu kama ifuatavyo:
Kwanza: Kenya inatawaliwa na mfumo wa kisekula wa kirasilimali uliorithiwa kutoka kwa wakoloni waliotutawala na wanaendelea hadi sasa kupitia vibaraka wao. Mfumo huu umekitwa juu ya ufisadi mkubwa nao ni kumtenga Muumba katika maisha na badala yake kumwachia mwanadamu kujiendeshea mambo anavyotaka kwa kichwa chake ambacho hakidiriki dhati ya Muumba katika kuwapangilia maisha ya viumbe wake. Kipimo chake kikiwa ni maslahi pekee.
Pili: Kupitia utekelezwaji wa mfumo huu batili na nidhamu zake zinatokamana nao imepelekea kukithiri kwa ufisadi kila nyanja ikiwemo nidhamu yake ya kisiasa; ambayo inafahamika kama demokrasia. Inampa mwanadamu fursa kumpa mamlaka mwanadamu mwenziwe akamuwakilishe katika utungwaji wa sheria ili ziwaongoze katika maisha jumla. Siasa hizi zimepelekea kukithirisha ukabila kwa kuwa daima wakoloni wameifunga siasa juu ya kabila kubwa na zenye nguvu. Kiasi kwamba siasa imekuwa ni kinyang’anyiro kati ya makabila!
Tatu: Nidhamu ya uchumi ambao unaendeshwa kwa njia ya uporaji ambao ulianza tokea ukoloni wa moja kwa moja hadi wa leo. Mali za taifa zimetekwa na kuwa za wakoloni na vibaraka wao, ikiwemo ardhi, mabiashara msingi n.k. Raia jumla wamebakia kudidimizwa katika umasikini wa kupindukia kila kukicha kupitia kutozwa kodi zisizokuwa na huruma na ukopaji wa mikopo ya riba isiyoingia akilini. Huku kashfa za ufujaji wa mabilioni ya fedha ukiendelea daima!
Nne: Nidhamu ya kijamii imekitwa juu ya uhuru; kiasi kwamba ubinafsi umekithiri na kila mmoja yuwenda mbio ili kujistarehesha kwa kiwango cha juu kwa njia yoyote wakati wowote ule. Madhara yake katika jamii yakiwa ni yakushtusha na kuvunja moyo na kukatisha tamaa wengi wa watu na kuwapelekea watu kuwa kama wanyama au chini zaid kwa kutenda vitendo baadhi ya mfano kuvunja familia, uzinifu, usagaji, ushoga, , ulafi wa mali, kujiua, n.k! Hii ikiwa imechangiwa pakubwa na nidhamu ya kielimu ambayo inajenga kuzalisha vikaragosi kwa sura za watu lakini wenye mitizamo ya kiyahayawani iliyofungwa tu katika kipimo cha faida na hasara. Na kuipelekea thamani ya mtu kutegemea kitu/mali aliyokuwa nayo/anayozalisha.
Suluhisho na Uhuru wa kweli ni ule utakaohakikisha kuwa Kenya inatawaliwa na mfumo unaotoka kwa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu pekee ndiye aliye na uwezo wa kujua kizuri na kibaya kwa viumbe wake. Mfumo unaotoka kwa Mola ni ule wa Uislamu na unatakiwa kutekelezwa na Dola ya Kiislamu ya Khilafah iliyosimama kwa njia ya Utume. Kupitia kusimamishwa kwa Khilafah ndiko kutakakopelekea si tu Kenya bali Afrika kukombolewa kutoka katika utumwa wa kikoloni, vibaraka wake na mfumo wao muovu na nidhamu zake ambao ndio chanzo cha kusambaratika Kenya, Afrika na Ulimwengu kwa ujumla.
Ali Nassoro Ali
Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kenya