Siku ya Katiba: Miaka Sitini ya Kufeli kwa Katiba ya Kisekular

Taarifa kwa Vyombo Vya Habari

Tarehe 27 Agosti 2025, ni kumbukumbu ya miaka kumi na tano ya kuzinduliwa  kwa Sheria Kuu ya 2010. Katiba ya Kenya ya 2010 ilisifiwa kuwa ya mageuzi na kutajwa kwamba ndio iliyoanzisha mageuzi ya kimsingi ya kisiasa, kijamii, na kiuchumi yaliyolenga kumaliza miongo kadhaa ya ukosefu wa utulivu chini ya katiba iliyopita.

Kwa muktadha huu, tungependa kufafanua yafuatayo:

Tangu kuzinduliwa kwake, mizozo ya kikatiba ya Kenya imejikita zaidi kwenye mapungufu ya utekelezaji, migogoro ya uchaguzi, ugavi wa mamlaka, kanuni za kijinsia na mchakato wa marekebisho. Kama alivyosema mara kwa mara Dk. Willy Mutunga, Jaji Mkuu wa kwanza kuwa Katiba ya Kenya 2010 ni waraka wenye kuendelea na utachukua angalau miaka 20-30 kutekelezwa kikamilifu. Imani  kwamba katiba mpya itaweza kushughulikia matatizo ambayo katiba ya kikoloni ilishindwa kuyashughulikia, sasa miaka 15 imekua ni ushahidi tosha wa kushindwa kwa imani ya kisekula ya kikatiba, huku ikibakia tu ngano ya  kurefushwa kwa ugumu wa  maisha na kuongezeka kwa viwango vya rushwa, hali mbaya ya uchumi, mauaji nje ya mahakama na mengine mengi..

Katiba zilizotungwa na mwanadamu zinatumiwa kwa urahisi na taasisi za kisiasa kwa vile maslahi ya kisiasa yanapewa kipaumbele kuliko hata kanuni (sheria) na katiba

Msingi wa Katiba mpya iliyopigiwa kura na Wakenya baada ya kura ya maoni ya 2010 ni ule ule wa kimsingi kwa katiba ya zamani ya kikoloni katika kumpa mwanadamu mamlaka kamili ya kujitungia sheria na Kupokonya haki hiyo   Muumba wa Mwanadamu, Uhai na Ulimwengu ambaya kwa yakini ndiye anayepaswa  kuwa chanzo pekee cha mwongozo na sheria. Uhalisia wa katiba zenye misingi ya kilimwengu hudhihirisha asili dhaifu ya mwanadamu katika kuamua mwongozo wa mwanadamu kwani mara nyingi huathiriwa na hali hivyo  kufanyiwa marekebisho au hata kutayarisha rasimu kamili ya katiba mpya. Kwa yakini , historia imethibitisha mara kwa mara kwamba mwanadamu hawezi kuwa  chimbuko la  mwongozo.

Ili kutambua ukombozi wa kweli kutoka kwa dosari  na makosa makubwa ya  katiba za Kidemokrasia ambayo itikadi mbovu ya Ubepari inastawi, tunatoa wito kwa watu kutoka tabaka mbalimbali za maisha wakiwemo wasomi, wasomi na wanasiasa kufanya kazi katika kuweka muongozo wa  Mwenyezi Mungu ambayo kamwe haurekebishwe na kuathiriwa na ubinafsi wa viongozi wa kisiasa. Hakika Mwanadamu anahitaji mwongozo unaotoka kwa Allah (swt). Ukombozi huu ulifafanuliwa vyema na hotuba ya Rabiu bin Amri kwa Rustom Kamanda wa Dola ya Uajemi:

 “Mwenyezi Mungu Ametutuma tumtoe Amtakaye katika ibada ya waja na kumuabudu Mola Mlezi wa waja, na kutoka kwenye ufinyu wa dunia hadi kwenye upana wake, na kutoka kwenye ukandamizaji wa itikadi hadi kwenye uadilifu wa Uislamu’

Katiba ni waraka muhimu unaobainisha sura ya mfumo wa utawala na kutengeneza mkataba kati ya watawala na wananchi na vilevile kuwa kielelezo cha itikadi na maadili ya watu yanayoainisha nyanja zote za maisha. Uislamu kama mfumo kamili wa maisha, unataka  katiba ambayo imeegemezwa kwa uwazi juu ya sheria ya Mwenyezi Mungu. Katiba hii inaweza tu kutekelezwa kupitia Khilafah serikali  ambayo kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu itasimamishwa  hivi karibuni katika moja ya nchi za Kiislamu.

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari Hizb ut-Tahrir Kenya