Swala Ya Jamaa Ni Miongoni Mwa Tangavu Za Kiislamu, Na Haifai Kutekelezwa Isipokuwa Kwa Namna Ilivyokuja Katika Wahyi.

Swala ya jamaa ina sifa yake maalumu ambayo haifai kukhalifiwa. Nayo iko wazi katika hadithi ya Mtume wa Allah (S.W.A): “أقيموا الصفوف، وحاذوا بين المناكب، وسدوا الخلل، ولينوا بأيدي إخوانكم، ولا تذروا فرجات للشيطان، ومن وصل صفا وصله الله، ومن قطع صفا قطعه الله عز وجل” (رواه أحمد والبيهقي)

“Simamisheni(nyoosheni)safu,na mlinganishe kati ya mabega, na zibeni mianya, na muwe laini mikononi mwa ndugu zenu (wakiwanyoosha) na wala msiache mianya ya shetani, na yeyote atakayeunganisha safu naye Allah atamuunga, na yeyote atakayekata safu naye Allah Mtukufu na mshindi atamkata”

[Imepokewa na Ahmad na Baihaqi kwa sanad sahih].

Kwa hiyo, kusimamisha swala ya jamaa kinyume na mwongozo wa utume ni kufumua kamba ya swala. Ama suala la gonjwa ambukizi na kuzuia kuenea kwake, lifanywe kwa mbinu na vitendea kazi bila kuzua katika dini ya Allah lisilokuwemo. Na kama azma ni za kweli, basi yawezekana kufanya yanayolazimu (ili kujikinga) na kutekeleza tangavu za Allah kwa namna aliyoweka Allah mtukufu na alivyobainisha Mtume wake (S.W.A).

بسم الله الرحمن الرحيم

SWALA YA JAMAA NI MIONGONI MWA TANGAVU ZA KIISLAMU, NA HAIFAI KUTEKELEZWA ISIPOKUWA KWA NAMNA ILIVYOKUJA KATIKA WAHYI

Asema Allah:

“وأقيموا الصلاة وآتوا الزكاة وأطيعوا الرسول لعلكم ترحمون

 “Na simamishen swala, na toeni zaka, na mtiini Mtume, ili mpate kurehemewa”.

 Hakika Allah (Subhaanahu Wataala) alituamrisha kusimamisha swala, na akatumia tamko la amri kwenye kitendo “Qaama” wala hakutumia kitendo moja kwa moja, yaani: hakusema: “Swalluu” (swalini) bali imekuja amri ya swala kwa matamshi ambayo yanaamrisha swala pamoja na yale ambayo swala haitimii ila kwayo (أقام الشيء) ina maana: kudumisha kitu kwa ukamilifu zaidi, na kwa namna isiyobadilika”. Hivyo basi, kitendo cha amri (Aqiimuu) kina maana ya ziada kuliko neno (swalluu). na maana iliyokusudiwa ni: kudumisha utekelezaji wa swala kulingana na sababu zake, nguzo zake kamili, na masharti yake, kama alivyoitekeleza Mtume (S.W.A).

Na swala ni ibada tauqifiyyah (…..) na ina namna yake maalumu iliyopokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w) maneno na vitendo. na kuzua ndani yake ni bid-ah (uzushi). na kwa hakika, mjumbe wa Allah ametubainishia namna yake (ya kuswali) kwa mkaazi na msafiri, mzima na mgonjwa. na akatubainishia pia hukumu za swala ya jamaa na namna ya kuitekeleza. na Mtume (s.a.w) alimwamuru Malik ibnul Huwairith (r.a) na walio pamoja naye kwa kuwaambia:” … Na mswali kama mlivyoniona nikiswali…” [imepokewa na Bukhari].

Enyi waislamu: imepokewa kutoka kwa Abu Umamah Albahiliy (r.a) amesema: amesema Mtume wa Allah:” «لَتُنْقَضَنَّ عُرَى الْإِسْلَامِ عُرْوَةً عُرْوَةً، فَكُلَّمَا انْتَقَضَتْ عُرْوَةٌ تَشَبَّثَ النَّاسُ بِالَّتِي تَلِيهَا، وَأَوَّلُهُنَّ نَقْضًا الْحُكْمُ وَآخِرُهُنَّ الصَّلَاةُ”

[أحمد والحاكم وابن حبان بإسناد صحيح]

“Zitafumuliwa kamba (sheria) za Uislamu, kamba baada ya kamba. kila ikifumuliwa kamba moja, watu watashikamana na nyengine inayofuata.  na  itakuwa ya kwanza kufumuliwa ni utawala, na ya mwisho ni swala”

[Ahmad, hakim, na Ibnu Hiban kwa sanad sahih].

Watawala wa kishetani wamefunga misikiti, na wakazuia kusimamishwa swala za jamaa na swala ya Ijumaa, kwa hoja ya kuzuia janga la Korona. na wakatumia baadhi ya fat-wa kama ngao ya  makosa yao na la kuumiza zaidi, ni kwamba tumesikia miito ya kuswaliwa swala ya jamaa kwa namna inayohalifu alivyoamrisha Mtume (s.a.w) na kwa masikitiko, tumeshuhudia mfano huo katika baadhi ya miji ya Kiislamu!Tukawaona wakiswali mbali mbali wakiwa wameachanisha safu! Na hili ni kuhalifu namna maalumu ya swala ya jamaa, na ni kutengua kamba ya swala. na ili kubainisha hili, tutaleta dalili zifuatazo:

  • عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ أَنَّهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «سَوُّوا صُفُوفَكُمْ، فَإِنَّ تَسْوِيَةَ الصُّفُوفِ مِنْ تَمَامِ الصَّلَاةِ (رواه مسلم) وفي رواية البخاري:«سَوُّوا صُفُوفَكُمْ، فَإِنَّ تَسْوِيَةَ الصُّفُوفِ مِنْ إِقَامَةِ الصَّلاَةِ».

Kutoka kwa Anas ibn Malik kuwa amesema: amesema Mtume (S.W.A): ziwekeni sawa safu zenu kwani hakika kunyooka kwa safu ni katika kutimia kwa swala( imepokewa na Muslim) na katika mapokezi ya Bukhari: “Ziwekeni sawa safu zenu, kwani kunyooka kwa safu ni katika kusimamisha swala”.

  • عن النُّعْمَانَ بْنَ بَشِيرٍ، قال: كَانَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يُسَوِّي صُفُوفَنَا حَتَّى كَأَنَّمَا يُسَوِّي بِهَا الْقِدَاحَ حَتَّى رَأَى أَنَّا قَدْ عَقَلْنَا عَنْهُ، ثُمَّ خَرَجَ يَوْمًا فَقَامَ، حَتَّى كَادَ يُكَبِّرُ فَرَأَى رَجُلًا بَادِيًا صَدْرُهُ مِنَ الصَّفِّ، فَقَالَ: «عِبَادَ اللهِ لَتُسَوُّنَّ صُفُوفَكُمْ، أَوْ لَيُخَالِفَنَّ اللهُ بَيْنَ وُجُوهِكُمْ» [مسلم]

Kutoka kwa Nuumaan ibn Malik, kuwa amesema:” Alikuwa Mtume wa Allah(S.W.A) akizinyoosha safu zetu hadi ni kama ananyoosha mishale, mpaka alipoona tumeshamwelewa. Kisha siku moja akatutokea akasimama mpaka akakaribia kupiga takbira, mara akamwona mtu kifua chake kimetoka katika safu. akasema:” Enyi waja wa Allah! Wallahi mtanyoosha safu, wallahi mtanyoosha safu! Au la si hivyo, Allah atatenganisha kati ya nyuso zenu”. [Muslim]

  • عن أَنَس: قَالَ أُقِيمَتِ الصَّلاَةُ فَأَقْبَلَ عَلَيْنَا رَسُولُ اللَّهِ – صلى الله عليه وسلم – بِوَجْهِهِ فَقَالَ « أَقِيمُوا صُفُوفَكُمْ وَتَرَاصُّوا ، فَإِنِّى أَرَاكُمْ مِنْ وَرَاءِ ظَهْرِي» [البخاري])

Kutoka kwa Anas amesema: ilikimiwa swala, akatuelekea Mtume wa Allah (s.a.w) kwa uso wake, akasema:” Nyoosheni safu zenu, na mshikamane kwani hakika mimi nawaona kutokea nyuma mgongoni” [Bukhari]

  • عَنْ أَنَسٍ أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ:«أَتِمُّوا الصَّفَّ الْمُقَدَّمَ، فَإِنْ كَانَ نُقْصَانٌ فليكن في المؤخرة» [رواه ابن حبان بسند صحيح].

Kutoka kwa Anas kwamba Mtume (S.W.A) amesema:”Kamilisheni safu za mbele, na kama kutakuwa na upungufu basi iwe ni katika safu za mwisho” [imepokewa na Ibnu Hibban kwa sanad sahih].

  • عن جابر بن سمرة قال: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «أَلَا تَصُفُّونَ كَمَا تَصُفُّ الْمَلَائِكَةُ عِنْدَ رَبِّهَا فَقُلْنَا يَا رَسُولَ اللَّهِ وَكَيْفَ تَصُفُّ الْمَلَائِكَةُ عِنْدَ رَبِّهَا قَالَ يُتِمُّونَ الصُّفُوفَ الْأُوَلَ وَيَتَرَاصُّونَ فِي الصَّفِّ» [مسلم]

Kutoka kwa Jabir ibn Samura, amesema: amesema Mtume wa Allah (S.W.A):”Kwa nini msinyooshe safu kama malaika wanavyonyoosha safu mbele ya mola wao? Wanakamilisha safu za kwanza, na wanakaribiana kwa safu” [Muslim].

  • عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: «مَنْ وَصَلَ صَفًّا وَصَلَهُ اللَّهُ، وَمَنْ قَطَعَ صَفًّا قَطَعَهُ اللَّهُ»
    [رواه الحاكم وقال: حديث صحيح على شرط مسلم]

Kutoka kwa Abdullahi ibn Amri, kwamba Mjumbe wa Allah amesema:”Atakayeunga safu basi Allah naye atamuunga. na atakayekata safu basi Allah atamkata”[ imepokewa na H akim na akasema: ni hadith sahih kwa sharti za Muslim].

  • عَنْ ابْنِ عُمَرَ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «أَقِيمُوا الصُّفُوفَ، وَحَاذُوا بَيْنَ الْمَنَاكِبِ، وَسُدُّوا الْخَلَلَ، وَلِينُوا فِي أَيْدِي إِخْوَانِكُمْ، وَلَا تَذَرُوا فُرُجَاتٍ لِلشَّيْطَانِ، وَمَنْ وَصَلَ صَفًّا، وَصَلَهُ اللَّهُ ، وَمَنْ قَطَعَ صَفًّا قَطَعَهُ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ» [رواه أحمد والبيهقي بسند صحيح].

Kutoka kwa Ibnu Umar(r.a) kwamba, Mtume (S.W.A) amesema: “Zisimamisheni(nyoosheni)safu,na mlinganishe kati ya mabega, na zibeni mianya, na muwe laini mikononi mwa ndugu zenu (wakiwanyoosha) na wala msiache mianya ya shetani, na yeyote atakayeunganisha safu naye Allah atamuunga, na yeyote atakayekata safu naye Allah mtukufu na mshindi atamkata” [imepokewa na Ahmad na Baihaqi kwa sanad sahih]

Hizi dalili zinabainisha namna ya safu zinavyotakiwa kuwa katika swala ya jamaa. nazo ni dalili zinazofidisha ulazima wa safu kulingana sawa, na kushikana. Pia, dalili zilizotangulia, ndani yake mna viashiria vinavyofidisha uwajibu. Kwa hiyo, kunyoosha safu “Ni miongoni mwa kusimamisha swala” – Katika mapokezi ya Bukhari- “Ni miogoni mwa kutimia swala”- mapokezi ya Muslim-. na katika hadith iliyopokewa na imam Ahmad kuwa  Mtume (S.W.A) ameamrisha kusimamisha safu, na mabega kuwa sawa sawa. na hilo lamaanisha kunyooka safu, kisha akaamrisha kuziba mianya. na akaelezea hiyo mianya kuwa ni mapenyo ya shetani. Kisha akatilia mkazo ulazima wa kuunganisha safu na kutokuwa mbali mbali kwa kusema:”Yeyote atakayeunga safu, Allah atamuunga” kisha akaendelea kusema: “Na atakayekata safu, Allah atamkata”. Hili ni kemeo kali la kutokata safu, na ni kiashiria cha kukataa.

Na neno lake: «عِبَادَ اللهِ لَتُسَوُّنَّ صُفُوفَكُمْ، أَوْ لَيُخَالِفَنَّ اللهُ بَيْنَ وُجُوهِكُمْ» (Enyi waja wa Allah! Wallahi mtanyoosha safu, wallahi mtanyoosha safu, au la sivyo Allah atazitenganisha nyuso zenu” ndani yake kuna kiapo na msisitizo, na hili ni katika matamshi yenye nguvu zaidi katika kusisitiza, na hiki kiashiria kingine cha kuonyesha ulazima wa kuziweka sawa safu kwani kutangulia herufi ya “lam” ya kiapo kabla ya “Fiilu mudhwari” pamoja na “Nuun tawkid” yenye shada, zote zafidisha msisitizo. kisha kukaja jibu la kiapo likitilia mkazo kwa kutaja adhabu kwa kuhalifu yaliyotajwa katika kiapo. hivyo basi, kutokana na hizi dalili na viashiria vilivyo ndani yake, haifai kusimamisha swala ya jamaa hali ya kuwa safu zimeachana. Amepokea imam Malik katika “Muwatwa” na imam Baihaqi katika “Assunanul Kubra”:

أَنَّ عُمَرَ بْنَ الْخَطَّابِ كَانَ يَأْمُرُ بِتَسْوِيَةِ الصُّفُوفِ فَإِذَا جَاءُوهُ فَأَخْبَرُوهُ أَنْ قَدْ اسْتَوَتْ كَبَّر”َ

“Kuwa Umar (r.a) alikua akiamuru safu ziwe sawa sawa, halafu wakija kumueleza kuwa safu zishanyooka, ndipo hupiga takbira”.

Na hatujapata dalili japo moja inayoruhusu kuswaliwa swala ya jamaa hali ya kuwa mbali mbali, au safu hazikushikana!Na katika ilimu ya usul ni kwamba, haifai kuacha jambo la wajib ila kuwe na ruhusa au kizuizi, na kuwe na dalili ya kisheria iliyojulisha hilo. sawa kiwe ni kizuizi cha kutoamrishwa na kutotekeleza, ama ni kizuizi cha kutoamrishwa tu. na hatujapata ruhusa ya kisheria moja inayoruhusu kuswaliwa swala ya jamaa hali ya kuwa mbali mbali, au safu hazikushikana!.

Ama suala la kufanya “Qiyaas” swala ya jamaa kwa swala ya mgonjwa, yaani kuzingatia hili janga (la Korona) ni ruhusa ya kuwa mbali mbali, kama vile maradhi kuwa ruhusa ya kuswali kwa kukaa: hii ni qiyaas ya kiakili wala wala sio ya kisheria. nayo ni qiyaas pasipo (illah) ya kisheria. kwa sababu, sharti ya qiyaas (ya kisheria) ni kuwepo (illah) ambayo itakusanya baina ya hukmu iliyokuja na dalili na baina ya kitendo ambacho kinatakiwa kufanyiwa qiyaas.

Kwa hiyo, mgonjwa huswali kwa kukaa ni kwa ajili ya (sabab) wala sio kwa ajili ya (illah). na (sabab) yenyewe ni ugonjwa, na hii ni (rukhsa), hivyo basi hakuna budi kutofautisha kati ya (sabab) za (rukhsa) ambazo ni fupi, na (illah) za hukumu zinazoenea na wanazuoni wa usul wametafautisha kati ya (sabab) fupi na isiyokuwa fupi ambayo yaweza kuwa (illah) yaani, wametafautisha kati ya (sabab) na (illah).

(Kwa mfano) kupunguza swala ni rukhsa na (sabab) yake ni safari. Kwa hiyo, safari ni (sabab) wala sio (illah) ndio maana, haifai kufanyiwa qiyaas. na kuswali kwa kukaa ni ruhsa ambayo (sabab) yake ni ugonjwa. na ugonjwa ni (sabab) wala sio (illah) kwa hivo, haifanyiwi qiyaas. Hila kwanza.

Ama la pili: ni kuwa, qiyaas huwa ni kukutanisha (far-i) tawi na asli(aswl)  kwa sababu ya kushirikiana katika (illah) moja. yaani, kwa kushirkiana kwao katika hukumu na maudhui. Kwa mfano: neno lake Mtume (S.W.A):

لاَ يَقْضِيَنَّ حَكَمٌ بَيْنَ اثْنَيْنِ وَهُوَ غَضْبَانُ»[رواه البخاري]

“Asitoe hukumu hakimu hali ya kuwa ana hasira”

Kwa hiyo, kadhi aliye na hasira, na kadhi aliye na msongo kwa ajili ya kupatwa na msiba, Wote wawili hawafai kutoa hukumu, kwa sababu ya kushirikiana katika (illah) moja, nayo ni akili kukosa utulivu. maudhui ni: kutoa hukumu, na hukmu ni: uharamu wa kuhukumu. na (illah) ni: hasira, au msongo wa mawazo. Hivyo basi, (illah) ya hasira na msongo wa mawazo zote maudhui yake ni “Kutoa hukumu” na hukumu itazunguka pamoja na hii (illah) kwa sababu ndio msukumo wake. Na hukumu hii haihusiani na mtu atakayeuza au kununua akiwa na hasira. Kwa sababu, (illah) ilikuja tu kwa utoaji hukumu wala sio kwa uuzaji na ununuzi, ambapo maudhui ni tafauti. Hivyo hivyo, swala ya jamaa na swala ya mgonjwa, kwani hizo ni maudhui mbili tofauti kwa kuwa swala ya jamaa ni maswala mbali yenye hukumu yake haswa, na swala ya mgonjwa nayo ni maswala mbali yenye hukumu yake haswa, wala haiwezi kufanyiwa qiyaas kati ya hizo mbili. Mbali na yaliyopita, ongezea na kuwa (sabab) za hukumu za kisheria au (illah) zake ni wajib kuwe na dalili ya kisheria inazojulisha. Kwa hiyo, kila (sabab) ni lazima iwe na dalili, kadhalika (illah) pia.

Muhtasari:

Swala ya jamaa ina namna yake maalumu na haifai kuihalifu, nayo iko wazi katika hadithi ya Mtume (S.W.A) aliposema:”

«أَقِيمُوا الصُّفُوفَ، وَحَاذُوا بَيْنَ الْمَنَاكِبِ، وَسُدُّوا الْخَلَلَ، وَلِينُوا فِي أَيْدِي إِخْوَانِكُمْ، وَلَا تَذَرُوا فُرُجَاتٍ لِلشَّيْطَانِ، وَمَنْ وَصَلَ صَفًّا، وَصَلَهُ اللَّهُ ، وَمَنْ قَطَعَ صَفًّا قَطَعَهُ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ»

[رواه أحمد والبيهقي بسند صحيح].

“Simamisheni (nyoosheni)safu,na mlinganishe kati ya mabega, na zibeni mianya, na muwe laini mikononi mwa ndugu zenu (wakiwanyoosha) na wala msiache mianya ya shaitani, na yeyote atakayeunganisha safu naye Allah atamuunga, na yeyote atakayekata safu naye Allah mtukufu na mshindi atamkata” [imepokewa na Ahmad na Baihaqi kwa sanad sahih].

Kwa hiyo, kusimamisha swala ya jamaa kinyume na muongozo wa utume ni kufumua kamba ya swala. Ama suala la gonjwa ambukizi na kuzuia kuenea kwake, lifanywe kwa mbinu na vitendea kazi pasi na kuzua katika dini ya Allah lisilokuwemo. na kama azma ni za kweli, basi yawezekana kufanya yanayolazimu (ili kujikinga) na kutekeleza tangavu za Allah kwa namna aliyoweka Allah mtukufu na alivyobainisha Mtume wake (S.W.A).

Mwisho:

Hakika hukumu za Allah hazichukuliwi kutoka kwa utashi na dhana na shaka, bali kutoka kwa dalili zake za kisheria zinazozingatiwa, pamoja na kutumia juhudi zaidi kuzifahamu kwa mujibu wa dalili za kilugha na kanuni sahihi za namna ya kujenga hoja, na kupatikane uzito na dhana iliyoshinda huwa kulingana na kanuni sahihi za (tarjiih) na hukumu za kisheria hazichukuliwi kutoka kwa wanafiki au wanazuoni wa watawala, au waliofitiniwa miongoni mwa maimamu ambao huwafuata madhalimu bali huchukuliwa kutoka kwa wanazuoni wachamungu na wakweli, ambao husema ukweli bila kuogopa kwa ajili ya Allah lawama za mwenye kulaumu.

Na kwa fadhila za Allah na rahma zake, janga la Korona halikuwa kali mno kwa waislamu wala halikusambaa zaidi. na hili lawajibisha kumshukuru Allah kwa fadhila zake na huruma yake na katika kumshukuru ni kusimamisha amri za Allah kwa namna alivyoamrisha bila kupindisha au kubadilisha, na kujikurubisha kwake kwa mambo anayoridhia na miji mingi ya Falastin janga hili halikuenea, na maeneo mengine hayajapata hata kisa kimoja, na hili linawajibisha kusimamisha swala kwa namna yake kama alivyoitekeleza Mtume (S.W.A) ama miji ambayo imekumbukwa na baadhi ya visa, walioathirika wanapaswa kuzuiliwa ndani pamoja na waliotangamana nao kwani ndio wenye uwezekano wa kuambukiza, na walio wazima au ambao hawajaambukizwa waendelee kusimamisha swala na huu ndio mwongozo wa mtume, ambao umetajwa katika dalili za kisheria… hadith ya Mtume (S.W.A) isemayo:” hakuna kuambukizana” kuna wanaotafsiri kukanusha maambukizi … lakini lenye nguvu zaidi ni kwamba, hii ni habari kwa maana ya agizo. yaani, herufi “laa” hapa ni ya kukaza wala si ya kukanusha. na hili linamwajibisha mwenye maradhi ambukizi ajitenge mwenyewe, ili asiwaambukize wengine na hii maana imekuja katika hadith nyengine ya Mtume (S.W.A)

«لاَ تُورِدُوا المُمْرِضَ عَلَى المُصِحِّ»

“Msimchanganye mgonjwa pamoja na walio wazima” [imepokewa na Bukhari].

Pamoja na kuondolewa vikwazo na kufunguliwa maeneo jumla zikiwemo sehemu za anasa na mapumziko, kwa hiyo hakuna udhuru uliobakia kwa yeyote. Lakini hata hivyo, waziri wa wakfu na wanaomfuata miongoni mwa waliofitiniwa ambao hawajali tangavu za Allah na mipaka yake, wametoa wito wa huu uzushi na wanataka kuwalazimisha watu! Na Subhaanallah utaona watu wanasongamana masokoni na kwengine, lakini wakati wa kusimamisha swala wanatakiwa wawe mbali mbali na kuhalifu muongozo wa mtume!

Mwisho kabisa:

Tunawahusia kumcha Allah, na kutafuta haki na ukweli kwa Allah. Pia, tukiwakumbusha kauli yake Mjumbe wa Allah aliposema: 

«مَنْ أَحْدَثَ فِي أَمْرِنَا هَذَا مَا لَيْسَ مِنْهُ فَهُوَ رَدٌّ»

“Yeyote atakayezua katika dini yetu hii lisilokuwa ndani yake, basi hilo jambo atarudishiwa mwenyewe”

 

Twamwomba Allah mtukufu azikunjue nyoyo za waislamu kwa hii heri, warudi kutoka kwaheri hadi kheri nyengine. na atusaidie kuisimamisha dini yake, na atupe ushindi kwa Khilafah Rashidah kwa njia ya utume isimamishe dini juu ya heri anayoipenda Allah na kuiridhia, na itakayobeba ujumbe wa heri, huruma na uongofu kwa walimwengu wote.

 

HIZB UT TAHRIR – PALESTINE