بسم الله الرحمن الرحيم
Silsila ya Majibu ya Mwanachuoni Mkubwa Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah Amiri wa Hizb ut Tahrir “Juu ya Maswali ya Wanaozuru Ukurasa Wake wa Facebook wa “Kifiqhi”
Jibu la Swali
Kwa: Ashraf Bader
(Imetafsiriwa)
Swali:
Assalamu Alaikum Wa Rahmatullahi Wa Barakaatuh Ewe Amir wetu mtukufu.
Namuomba Mwenyezi Mungu aliye juu na muweza muwe na siha na afya, na pia namuomba Mwenyezi Mungu awasaidie na awathubutishe.
Naomba kuleta maudhui -namuomba Mwenyezi Mungu aniafikie ndani yake – na itapendeza sana kama mutaitizama na mtoe uamuzi juu yake.
Imetajwa katika kitabu cha “Shakhsiya ya Kiislamu” Juzuu ya Kwanza, katika mlango: “Haja ya Umma leo kwa wafasiri” tulipozungumzia kuhusu Waarabu kuacha kutumia baadhi ya matamshi kwa kutosheka na visawe ama matamshi yanayokaribiana nayo, maadamu maana yaliyokusudiwa yamenyooka.
Na kwenye maudhui ya “visomo” tulileta mfano katika ukurasa wa 309, na naona hapo tulikosea. Pale Mwenyezi Mungu aliposema: “لنبوئنهم من الجنة غرفا” “bila ya shaka tutawaweka katika maghorofa ya Peponi” [Al-Ankabūt: 58] Wakati tulipoisoma kwa kisomo cha Abu Jaafar kutokana na mapokezi yake, “لنبوينهم من الجنة غرفا” ” bila ya shaka tutawaweka katika maghorofa ya Peponi” [Al-Ankabūt: 58]
Na hili ni kwa njia mbili:
Kwanza: ni sawa kwamba Abu Jaafar anaisoma kwa kubadilisha “hamza” na kuwa “yaa” ila yeye husoma kwa kuunganisha “mimu” ya wengi kwa kauli moja [husoma hivi] لَنُبَوِّيَنَّهُمُ مِنَ…”….” (li nubawwiyannahum) hivyo haipatikani kuingiza mimu ya لَنُبَوِّيَنَّهُم (nubawwiyannahum) ndani ya mimu ya “مِنْ” kama ilivyopigwa mfano kwenye kitabu ukurasa wa 309. Na ama kisomo kwa kubadilisha pamoja na kufanya idghaam [kuingiza herufi moja ndani ya herufi nyengine] hilo halikuja katika visomo vya mutawaatir [vilivyopokewa na wengi kutoka kwa watu wengi].
Na jambo jengine, ni kuwa hukmu ya “ibdaal” [kubadilisha] haiathiri katika maana ya neno, nayo ni katika hukmu za kimsingi. Na maadamu maudhui kuhusu Waarabu kutosheka na matamshi badala ya visawe au matamashi yanayokaribiana nayo, kwa hiyo huo haufai kuwa ni mfano [mzuri] kwa sababu, maana ya “بَوَّأَ “ na “بَوَا” haitofautiani, kwa kuwa maana ni hiyo hiyo lakini kwa hukmu ya ibdaal [kubadilisha]
Pili: Mfano utakuwa sawa tukibadilisha kisomo cha hamza au kisaai au baada ya [msomaji] wa kumi kwa kisomo cha Abu Jaafar. Na hilo kwa sababu wao wanasoma “لَنُثْوِيَنَّهُمْ من الجنة غرفا” na neno “thawaa” latafautiana na “tab-wi`ah” kimsingi, na hili ndilo linaloendana na mtiririko [wa maneno].
Ewe Mola, kama nimepatia basi ni kutokana na wewe, na kama nimekosea basi ni kutokana na nafsi yangu. Na namuomba Mwenyezi Mungu atujaalie miongoni mwa wale wanaochangia hii thaqafa [elimu] kubakia ikiwa safi. Na Mwenyezi Mungu awalipe kheri, awasaidie, na awape thabaat.
Jibu:
Wa Alaikum Salaam Wa Rahmatullahi wa Barakaatuh. Mwenyezi Mungu akubariki kwa kutuombea dua nzuri…
Bila shaka swali lako, ama tuseme maoni yako ni kuhusu sehemu ifuatayo katika kitabu cha “Shakhsiyyah ya Kiislamu” Juzuu ya Kwanza:
[… ama kwa namna ya kuitumia misamiati ikiwa ndani ya sentensi zake, au kubadilisha sentensi: katika hayo mambo bila shaka Qur`an itaenda kama ilivyozoeleka kwa Waarabu ambao Qur`an ilishuka kwa lugha yao. Na pamoja na kwamba Qur`an iliwashinda Waarabu lakini haikupatikana ndani yake kutoka nje ya mazoea yao ya kuendelea katika matumizi ya maneno, na uhalisia wake [Qur`an] kiupande huo ni sawa tu na mazoea ya Waarabu katika hayo…
Na kwa hakika, hayo yamepatikana ndani ya Qur`an kwa kutosheka na baadhi ya matamshi na kuacha visawe [matamshi yenye maana sawa] au matamshi yanayokaribiana nayo, mfano wa qiraa`aat [visomo] kwenye Qur`an. Mfano:
﴾مَٰـلِكِ يَوۡمِ ٱلدِّينِ﴿، “Mwenye kumiliki siku ya malipo” [Al-Faatihah: 4] ﴾مَلِكِ يَوۡمِ ٱلدِّينِ﴿، “Mwenye kumiliki siku ya malipo” [Al-Faatihah: 4] ﴾وَمَا يَخۡدَعُونَ إِلَّآ أَنفُسَهُمۡ﴿، “lakini hawadanganyi ila nafsi zao; nao hawatambui” [Al-Baqarah: 9] ﴾وَمَا يُخۡادِعُونَ إِلَّآ أَنفُسَهُمۡ﴿، “lakini hawadanganyi ila nafsi zao; nao hawatambui” [Al-Baqarah: 9] ﴾لَنُبَوِّئَـنَّهُم مِّنَ ٱلۡجَنَّةِ غُرَفاً﴿، ” bila ya shaka tutawaweka katika maghorofa ya Peponi” [Al-Ankabūt: 58] ﴾لَنُبَوِّيَـنَّهُم مِّنَ ٱلۡجَنَّةِ غُرَفاً﴿ ” bila ya shaka tutawaweka katika maghorofa ya Peponi” [Al-Ankabūt: 58] Na mifano mengineyo kulingana na visomo ] Mwisho wa Nukuu.
Na wewe waona kwamba kwenye kitabu cha “Shakhsiya ya Kiislamu” kuna makosa sehemu mbili:
Kwanza: herufi “miim” kwenye neno “لَنُبَوِّيَنَّهُمْ “ kuwekwa sakna katika kitabu, jambo linalopelekea hiyo “miim” iingizwe ndani ya “miim” inayofuatia kwenye herufi “مِنْ” hivyo basi ikadhihirika “miim” ya herufi “مِّنْ “ hivi ikiwa na shadda kwenye kitabu, kwa hiyo itajulisha kuwa kuna idghaam, na hilo kulingana na rai yako sio sawa, kwa sababu neno (لَنُبَوِّيَنَّهُمْ) na hicho kisomo cha Abu Jaafar, wakati kwake ilivyo ni kwa kuunganisha “miim” ya wingi, kwa hiyo hapo itakuwa hakuna cha idghaam.
Pili: mfano ulioletwa kwa kisomo cha (لَنُبَوِّيَنَّهُمْ) pia haufai. Kwa kuwa hili tamko (لَنُبَوِّيَنَّهُمْ) ni kama (لَنُبَوِّئَنَّهُم) kwa upande wa kimaana, kikubwa kilichopo ni kubadilisha [herufi] hamza na mahali pake kuwekwa [herufi] yaa, na hilo kulingana na maoni yako haliendani na kitu kilichotakiwa kupigiwa mfano!.
Na majibu ya hayo ni kama ifuatavyo:
1. kuhusu angalizo lako la kwanza -yaani kudhihirika shadda juu “miim” katika herufi (مِنْ) na hilo lamaanisha kwamba “miim” iliyopo kwenye (لَنُبَوِّيَنَّهُمْ)) imeingizwa ndani ya “miim” iliyopo kwenye (مِنْ) na hilo ni kinyume na kisomo kilichotajwa ambacho ni cha Abu Jaafar, kwa kuwa yeye husoma kwa kuunganisha “miim” ya wingi… yaani anasoma hivi (لَنُبَوِّيَنَّهُمُ مِنْ…) hivyo hakuna kuingiza “miim” ya mwanzo ndani ya “miim” ya pili -… hili angalizo ni sahihi. Kwani imekuja kutoka kwa kisomo cha Abu Jaafar: kitabu (النشر في القراءات العشر (1/ 273):
[ Na wametofautina kuhusu kuunganisha “miim” ya wingi na “waaw” na kuitia “sakna”. Na ikiwa kabla ya herufi yenye “harakah” mfano:
(أَنْعَمْتَ عَلَيْهِمْ غَيْرِ الْمَغْضُوبِ عَلَيْهِمْ) “Njia ya ulio waneemesha, siyo ya walio kasirikiwa” [Al-Faatiha: 7] (وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنْفِقُونَ)، “…na hutoa katika tuliyo wapa.” [Al-Baqara: 3] (عَلَيْهِمْ أَأَنْذَرْتَهُمْ أَمْ لَمْ تُنْذِرْهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ)، “kwao ukiwaonya au usiwaonye, hawaamini.” [Al-Baqara: 6] (عَلَى قُلُوبِهِمْ وَعَلَى سَمْعِهِمْ وَعَلَى أَبْصَارِهِمْ غِشَاوَةٌ وَلَهُمْ عَذَابٌ) “Mwenyezi Mungu amepiga muhuri juu ya nyoyo zao na juu ya masikio yao, na juu ya macho yao pana kifuniko. Basi watapata adhabu kubwa” [Al-Baqara: 7] huwekwa “dhamma” miim zote katika sehemu zote hizo, na ibn Kathir na Abu Jaafar wao wameziunganisha [hizo miim] na waaw.
Rejea: Faridat Al-Dahr Fi Ta’seel wa Jamm’ Al Qiraat **(73/4) (2) Abi Jaafar akiisoma (li nubawwiyannahum) kwa kubadilisha Hamzah kwa -ya (yenye Fat’ha) na kuiunganisha -meem.)
Kwa hiyo, ilivyo kwenye hicho kitabu ni kosa la kimaandishi, na haikuwa hivyo katika machapisho yaliyotangulia ya “Shakhsiya ya Kiislamu” Juzuu ya Kwanza. Kwa mfano: chapa ya tatu haikuwa na “harakaat” juu ya herufi, na ilikuwa aya ndani yake ziko kulingana na kisomo cha Abu Jaafar hivi (لَنُبَوِّيَنَّهُمُ مِنَ الْجَنَّةِ غُرَفًا) ” bila ya shaka tutawaweka katika maghorofa ya Peponi” [Al-Ankabūt: 58] bila ya “shadda” yaani bila ya idghaam. Lakini baadaye zilipowekwa aya za Qur`an kwenye kitabu kwa maandishi ya “Uthmaaniy” na kwa “tashkiil” basi Qiraa cha kwanza kikawa kwa namna sahihi kulingana na ilivyo kwenye misahafu ﴾لَنُبَوِّئَـنَّهُم مِّنَ ٱلۡجَنَّةِ غُرَفاً﴿، ” bila ya shaka tutawaweka katika maghorofa ya Peponi” [Al-Ankabūt: 58] Na ilipopigwa mfano kwa kisomo chengine -kisomo cha Abu Jaafar – basi yadhihirika kwamba mpangiliaji alibadilisha herufi “hamza” kwenye maandishi ya kisomo cha kwanza na akaweka herufi “yaa” mahali pake kulingana na kisomo cha Abu Jaafar bila ya kuzingatia maudhui ya kuunganisha “miim” ya wingi, hivyo akabakisha tashkiil kama ilivyo: ﴾لَنُبَوِّيَـنَّهُم مِّنَ ٱلۡجَنَّةِ غُرَفاً﴿ ” bila ya shaka tutawaweka katika maghorofa ya Peponi” [Al-Ankabūt: 58] na ndipo ilipodhihirika “shadda” juu ya herufi “miim” kwenye neno “مِنْ “ na hilo ni kosa la uchapishaji…
2. Ama kuhusu angalizo lako la pili: kwamba kupigwa mfano wa kisomo cha Abu Jaafar (لَنُبَوِّيَنَّهُمْ) ” bila ya shaka tutawaweka katika maghorofa ya Peponi” [Al-Ankabūt: 58] sio sahihi kwa kuwa “maana ya “بَوَّأَ “ na “بَوَا” haitofautiani, kwa kuwa maana ni hiyo hiyo lakini kwa hukmu ya ibdaal [kubadilisha] “ hili si angalizo la kina. Kwa sababu, mfano uliopigwa hii sehemu kwenye kitabu cha “Shakhsiya ya Kiislamu” ni kwa ajili ya [kupigia mfano] kutumika matamshi mawili ambayo yana maana sawa, kwa hiyo kutotafautiana maana hakuathiri usahihi wa mfano, bali ni kwa kinyume chake! Kwani ilitakiwa maana iwe ni moja au yenye kukaribiana ili mfano uwe sahihi! Kwa sababu [kitabu] chasema: (…na kwa hakika, hayo yamepatikana ndani ya Qur`an kwa kutosheka na baadhi ya matamshi na kuacha visawe [matamshi yenye maana sawa] au matamshi yanayokaribiana nayo, mfano wa qiraa`aat [visomo] kwenye Qur`an…) yaani… kilichotakiwa ni maana yawe moja au kukaribiana ingawa matamshi ni tofauti… na kupigwa mfano kwa visomo viwili tofauti kwa sababu ya ibdaal, huko ni kupigia mfano matamshi mawili tofauti japo maana ni sawa kabisa. Kwa sababu, matamshi ambayo yanaingiliwa na ibdaal ni matamshi tofauti na sio tamshi moja… na As-Suyutwi ameliashiria hili katika kitabu chake (Al-Mizhar) alipokuwa akizungumzia ibdaal akasema: “Aina ya thalathini na mbil ni: kujua kubadilisha (ibdaal).
Amesema Faaris katika [kitabu cha] “Fiqh ul-Lugha”: miongoni mwa kawaida za Waarabu ni kubadilisha herufi na kuweka baadhi yake mahali pa herufi zengine, [mfano] : مَدَحَه ومَدَهَه ، “amemsifu” وفرس رِفَلّ ورِفَنّ“Farasi mwenye mkia mrefu”… na mifano ni mingi na mashuhuri, na wanazuoni wamezitungia vitabu… na kati ya waliotunga katika aina hii ni ibnu Sakkit, na Abu Twayib Al-Lughawiy.
Amesema Abu Twayib katika kitabu chake: “ibdaal makusudio yake sio kwamba Waarabu wanafanya makusudi kubadilisha herufi kwa herufi, bali [makusudio ya ibdaal] hizo ni lugha tofauti zenye maana zinazokubaliana, yanakaribiana matamshi mawili katika lugha mbili zenye maana moja, hadi [wakati mwengine] hayatafautiani isipokuwa katika herufi moja. Amesema: na dalili juu ya hilo ni kwamba, kabila moja huzungumza neno wakati fulani likiwa na hamza, na wakati mwengine bila hamza, na mara nyengine likiwa na siin, hivyo hivyo kubadilisha “laam” ya taarif kuwa “miim” na hamza iliyo mwanzo kuwa “ain” kama kusema kwao mfano: أنْ – عَنْ, Waarabu hawashirikiani katika chochote katika haya matamshi, wengine husema hivi na wengine vile…] Mwisho wa nukuu.
Kwa hiyo, kubadilisha herufi kwa herufi nyengine katika neno moja hufanya matamshi mawili kuwa tofauti hata kama maana [ya hayo matamshi] ni moja. Na hilo ni kwa kuwa kila tamshi kati ya hayo ni lugha kwa Waarabu: baadhi ya Waarabu husema kuhusu kusifu (مَدَحَ) na wengine husema (مَدَهَ) wakati zote maana ni sawa. Na baadhi yao husema: ((سَقْرٌ kwa “siin” na wengine ((صَقْرٌ kwa “swaad”, na baadhi yao husema: (نبوئهم) kwa hamza na wengine husema: (نبويهم) kwa “yaa” na zote maana ni sawa… na Qur΄an tukufu katika baadhi ya hali imetumia matamshi tafauti tafauti kuzungumzia maana moja katika aya moja pale visomo vya Qur΄an vinapokuwa vingi kwa sababu ya lugha za Waarabu kuwa nyingi. na katika hilo, ni lugha kuwa nyingi kwa sababu ya ibdaal kama ilivyo katika ile sehemu iliyozungumziwa kwenye “Shakhsiya ya Kiislamu” Juzuu ya Kwanza, kwa sababu tamshi hili (لنبوئنهم) sio sawa na tamshi la (لنبوينهم) kwa sababu ya ibdaal ingawa maana ni moja, lakini baadhi ya Waarabu husema (لنبوئنهم) na wengine husema (لنبوينهم) na Qur΄an imetumia hii lugha na ile, na hilo ni pale visomo vilipokuwa vingi, baadhi wakasoma (لنبوئنهم) na kisomo cha Abu Jaafar kikawa ni (لنبوينهم).
Kwa hayo maelezo yadhihirika wazi kwamba sisi hatukukosea tulipotaja kisomo cha Abu Jaafar (لنبوينهم) kando na kisomo cha (لنبوئنهم) kwa sababu kilichotakiwa kimetimia kwa kujata visomo viwili, ambapo kumetumika matamshi mawili tofauti kwa kuwa ni lugha mbili kwa Waarabu kwa ajili ya kuelezea maana hiyo hiyo.
Lakini pia kupiga mfano wa kisomo chengine cha (لنثوينهم) kwa “thaa” mahali pa “baa” yaweza kuwa mbali sana isiweze kukanganya, na itakuwa wazi zaidi katika kudhihirisha yanayotakikana katika maandishi yaliyotajwa ndani ya “Shakhsiya”, kwa hiyo tutarekebisha maandisha kwa kuweka (لنثوينهم) kwa “thaa” mahala pa (لنبوينهم) kwa “yaa”.
Bila shaka hiki kisomo kimekuja kwenye hiyo hiyo aya kama ilivyo katika kitabu cha “النشر في القراءات العشر”: {na wametafautiana katika kusoma (لَنُبَوِّئَنَّهُمْ مِنَ الْجَنَّةِ) [wasomaji] hamza, kisaai, na khalaf wao wamesoma kwa “thaa” yenye vidoti vitatu ikiwa na sakna baada ya “nuun”, na kubadilisha “hamza” na kuwa “yaa” kutokana na neno “الثَّوَاء” lenye maana ya kutulia mahali. Na wasomaji wengine walibakia wamesoma kwa “yaa” yenye doti moja na “hamza” kutokana na neno (التَّبَوُّءِ) maana yake “mahali pa kushukia” na imetangulia kubadilisha “hamza” yake kwa Abu Jaafar na kuwa hamza moja]” Mwisho wa nukuu.
Na imekuja katika tafsiri ya Twabari: (لَنُبَوِّئَنَّهُمْ مِنَ الْجَنَّةِ غُرَفاً) ” bila ya shaka tutawaweka katika maghorofa ya Peponi” [Al-Ankabūt: 58 “Asema Mwenyezi Mungu: tutawashukisha kwenye pepo za juu. Wasomaji wametofauatiana katika kuisoma, wengi katika wasomaji wa Madina na Basra na baadhi ya watu wa mji wa Kufa: {لَنُبَوِّئَنَّهُمْ} kwa “baa”. Na wasomaji wengi wa mji wa Kufa wamesoma hivi: (لَنُثوِيَنَّهُمْ). kwa “thaa” na kauli ya sawa kwangu ni kwamba zote mbili ni visomo mashuhuri kwa wasomaji wa miji, visomo vyote vimesomwa na wanazuoni katika wasomaji, na maana zakaribiana. Hivyo basi, vyovyote atakavyosoma msomaji atakuwa amepatia, na hilo ni kwa sababu kusema kwake {لَنُبَوِّئَنَّهُمْ} kwatokana na kitendo بَوَّأْتُهُ مَنْزِلاً yaani: nimemshukisha mahali, hivyo hivyo pia kusema ““لَنُثوِيَنَّهُمْ yatokana na (أَثْوَيْتُهُ مَسْكَناً) ikiwa na maana: nimemshukisha mahali, kutokana na neno (الثَّوَاء) nayo ni kutulia mahali.] “ Mwisho wa nukuu.
Ndio hivyo, visomo mutawaatir vya Qur`an -ambapo haiswihi kusoma Qur`an kwa visomo visivyokuwa mutawaatir – kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, visomo hivyo havitoki nje ya lugha za Kiarabu ﴾قُرآنًا عَرَبِيًّا غَيْرَ ذِي عِوَجٍ﴿ “Qur’ani ya Kiarabu isiyo na upogo” [Az-Zumar: 28]. Pia kauli yake: ﴾إِنَّا أَنزَلْنَاهُ قُرْآنًا عَرَبِيًّا لَّعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ﴿ “Hakika Sisi tumeiteremsha Qur’ani kwa Kiarabu ili mpate kuzingatia” [Yusuf: 2]. Yaani: imeteremka kwa lugha za Waarabu.
Na mwisho: kwa hakika mimi naheshimu pupa yako na kushughulika kwako na elimu ya visomo, na pia naheshimu kuchunga kwako undani wa mambo, na nakuombea kheri kutoka kwa Mwenyezi Mungu mtakatifu.
Ndugu Yenu,
Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah
23 Rabi’ ul-Akhir 1443 H
28/11/2021 M
Link ya jibu hili katika ukurasa wa Amiri wa Facebook