Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu, na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu wote, Muumba wa wanadamu na Mtumaji wa manabii pamoja na risala, Mshindi wa wenye nguvu na Mtawala juu ya waja, na rehma na amani zimshukie bwana wa viumbe na mbebaji ujumbe, yule aliyetumwa na Wahyi wa kusimamisha nidhamu ya Khilafah, yule ambaye alionya juu ya kuvunjwa kwake na kutoa bishara njema za kurudi kwake, bwana wetu Muhammad na juu ya familia yake na maswahaba zake wote.
Al-Bukhari amepokea katika Sahih yake kutoka kwa Muhammad bin Ziyad, aliyesema: Nilimsikia Abu Hurairah, radhi za Mwenyezi Mungu ziwe pamoja naye, amesema: Mtume (saw) amesema, au alisema Abu Al-Qasim (saw) amesema,
«صُومُوا لِرُؤْيَتِهِ وَأَفْطِرُوا لِرُؤْيَتِهِ فَإِنْ غُبِّيَ عَلَيْكُمْ فَأَكْمِلُوا عِدَّةَ شَعْبَانَ ثَلَاثِينَ»
“Fungeni kwa kuonekana kwake (mwandamo wa mwezi wa Ramadhan), na fungueni kwa kuonekana kwake (mwandamo wa mwezi wa Shawwal), na ikiwa mawingu yametanda juu yenu (kiasi cha kutouona) basi kamilisheni hesabu ya (siku) thalathini za Sha’aban.”
Baada ya kuutafuta mwandamo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan usiku huu, mkesha wa Jumatatu, kuonekana kwa mwandamo wa mwezi hakukuthubutu kwa mujibu wa masharti ya kisheria, hivyo basi kesho, Jumatatu, inakamilisha mwezi wa Sha’aban, na Jumanne itakuwa ndio siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhan ya mwaka 1442 Hijria.
Kwa mnasaba huu, nawasilisha salamu zangu na pongezi za Mkuu wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na wale wote wanaofanya kazi ndani yake, kwa Amiri wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, nikimuomba Mwenyezi Mungu kumnusuru na kuharakisha ushindi kwetu na tamkini kupitia mikono yake.
Ramadhan mwaka huu inatutembelea na huku ulimwengu unaongezeka kuchanganyikiwa na kushughulishwa na majanga. Kushindwa kwa mfumo wa kirasilimali imekuwa ni jambo linaloonekana wazi miongoni mwa ya duara za watawala na watoaji maoni katika miji mikuu ambayo mfumo wa kirasilimali ulianzia. Watu wa nchi za Magharibi wanatazama kwa tashwishi tabia zote za serikali zao, huku nchi zinazokaliwa na Magharibi – kwa njia ya moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja – zinatumbukia kwenye majanga, ukosefu wa utulivu na hata ghasia. Na watu wa nchi za Kiislamu haswa wanalipia gharama maradufu kwa kipindi cha miaka mia moja iliyopita, kwa pamoja.
Gharama ya kwanza ni kuendelea kudhalilishwa kimataifa kwa Umma wa Kiislamu tangu Khilafah ilipo vunjwa. Ishara ya udhalilishaji huu ilianza wakati Jenerali Gouraud alipolipiga teke kaburi la Salahuddin, Mwenyezi Mungu amrehemu, na sio la tukio la mwisho Ufaransa yaendelea na kumtukana bwana wetu Muhammad (saw). Mwenyezi Mungu (swt) asema:
]قَدْ بَدَتِ الْبَغْضَاء مِنْ أَفْوَاهِهِمْ وَمَا تُخْفِي صُدُورُهُمْ أَكْبَرُ]
“Imekwisha fichuka chuki yao katika midomo yao. Na yanayo ficha vifua vyao ni makubwa zaidi.” [Aal-i-Imran: 118].
Ama gharama ya pili, ni kuishi maisha yaliyojaa migogoro na misiba. Chini ya utawala wa mfumo wa kirasilimali, nchi nyingi za Kiislamu zimekuwa chini ya mzigo wa migogoro mibaya sana. Hivyo basi migogoro ya kiuchumi, usalama na kijamii imeathiri viwango vya maisha vya mamia ya mamilioni ya Waislamu. Leo, uhamiaji na kukimbia nchi imekuwa mwenendo kwa watu wa Umma wa Kiislamu!
Miaka mia moja iliyopita imethibitisha kuwa mkoloni kafiri Magharibi haitaondoa udhalilishaji na mateso haya kutoka mabegani mwa Umma wa Kiislamu maadamu inadhibiti hatma yake. Mwenyezi (swt) asema:
]وَإِن يَظْهَرُوا عَلَيْكُمْ لاَ يَرْقُبُواْ فِيكُمْ إِلاًّ وَلاَ ذِمَّةً]
“… Nao wakikushindeni hawatazami kwenu udugu wala ahadi?” [At-Tawba: 8].
Kuanzia mateso ya Wauyghur na mauwaji ya Rohingya, hadi uharibifu wa Ash-Sham na ukaliaji wa Al-Aqsa; mwanzo wa mizozo hii yote ilikuwa kupoteza uwezo wa Waislamu kusimamia mambo yao kwa sababu ya kukosekana kwa dola inayowakilisha maslahi haya.
Lakini maumivu haya ya miaka mia moja, pamoja na uwepo wa wabebaji wa Dawah, yameufanya Ummah kutambua, kwa busara na kwa dhahiri, kwamba ulipoteza fahari yake wakati ulipo poteza Khilafah yake, na utambuzi huu uliifanya Khilafah kuwa ndio rai jumla ya umma miongoni mwa Waislamu, wakiangalia na kutamani kurudi kwake.
Pia, matokeo ya maumivu hayo, ni kwamba Ummah ilifahamu juu ya kujitiisha kwa watawala wake na kuusaliti kwao. Hamu yao ni kutumikia maslahi ya mkoloni kafiri Magharibi, na wameisaidia kupora utajiri wa Ummah, kuangamiza ardhi zake na kuua watoto wake. Hii iliufanya Umma utambue kuwa nguvu zake zilinyang’anywa na unahitaji kukombolewa. Leo, watu wake wamekasirika na kulipuka, tayari kutoa damu yao ili kurudisha tena mamlaka yao.
Ama kuhusu ubwana wa Shariah, Umma bado haujaamua juu ya faradhi hii. Tunauona katika hali na matukio mingi ukisita kuufanya ubwana huo kuwa kwa Sharia pekee, kwa hivyo unaleta sheria zengine pamoja na Shariah ya Kiislamu katika suala la utawala. Sababu ya hili ni kukosa ujasiri katika uwezo wa Shariah kutawala maisha, kwa kuongeza kujisikia duni dhidi ya nguvu ya mkoloni kafiri Magharibi.
Hapa inakuja dori ya wale Waislamu ambao wanahusika na mimbari, mabaraza, vikundi, majukwaa na vyombo vya habari, na wale Waislamu ambao Mwenyezi Mungu (swt) amewawezesha kuwa katika nafasi za mamlaka na ulinzi katika Umma wa Kiislamu.
Enyi Wamiliki wa Mimbari, Majukwaa, Mabaraza na Vikundi … Enyi Waja wa Mwenyezi Mungu:
Mumekubali jukumu la kuunda rai jumla ya umma, na Mwenyezi Mungu atawauliza juu ya kile alichowakabidhi na hivyo kuufanya Umma kuwa thabiti katika imani yake juu ya sheria ya Kiislamu na uwezo wake wa kusimamia maswala ya maisha ni jukumu lenu, na pia kuufundisha juu ya uharamu wa kuchanganya sheria zengine na sheria ya Mwenyezi Mungu ni jukumu lenu. Mwenyezi Mungu (swt) asema:
]وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَمْرًا أَن يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ]
“Haiwi kwa Muumini mwanamume wala Muumini mwanamke kuwa na khiari katika jambo, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapo kata shauri katika jambo lao. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake basi hakika amepotea upotofu ulio wazi.” [Al-Ahzab: 36].
Enyi Watu wa Nguvu na Ulinzi … Enyi Waja wa Mwenyezi Mungu:
Tunawasihi, katika mwezi huu mtukufu, mutimize wajibu wenu mliopewa na Mwenyezi Mungu (swt) wa nguvu na ulinzi, na mutekeleze kwa vitendo ili kusimamisha sheria ya Mwenyezi Mungu. Kwa kutoa nusra kwa Hizb ut Tahrir, kiongozi asiyewadanganya watu wake, utawala wa Magharibi utaondolewa kutoka nchi za Kiislamu, na mamlaka ya Ummah yataregeshwa. Mwenyezi Mungu (swt) asema:
]إِن تَنصُرُوا اللَّهَ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ]
“Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.” [Muhammad: 7].
Mwezi wenu uwe wenye Baraka, Wassalamu Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh.
Mkesha wa Jumatatu unakamilisha mwezi wa Sha’aban ya mwaka 1442 H.
Mh. Salah Eddine Adada
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir