Tanzia ya Mbebaji Daawa Kenya

Taarifa kwa Vyombo Vya Habari

إِنَّا للهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ﴿

“Hakika sisi ni wa MwenyeziMungu na Kwake Yeye ni wenye kurejea

Kwa imani thabiti na kujisalimisha kikamilifu kwa Qadhaa ya Allah (swt), Hizb ut Tahrir / Kenya inaomboleza kwa Umma wa Kiislamu kwa ujumla na watu wa Kenya hasa;

Ustadh Said Salim Ali

(MwenyeziMungu amrehemu) aliefariki siku ya Alhamisi 14th of March 2024, baada ya kushambuliwa na wahuni kwa visu.

Kama Imam na Mwalimu, Ustadh Said alijiunga na harakati ya kimfumo ya Kiulimwengu  Hizb ut Tahrir –   inayobeba ulinganiizi wa kurejesha maisha ya kiislamu, kupitia kusimamisha tena Khilafah kwa njia ya Mtume (saw). Ingawa, sisi hatusifii mbele ya Mwenyezi Mungu mtu yoyote yule lakini tunashuhudia kwamba alikuwa akitimiza majukumu yake ya Kida’awa.

Hakika nyoyo zetu zinahuzunika, macho yetu yanatokwa na machozi kwa msiba huu mkubwa wa Imam na ndugu, Ewe Mwenyezi Mungu, mrehemu na umsamehe. Ewe Mwenyezi Mungu, mkrimu mashukio yake na umkunjulie mahala pake.

Mwisho tunapenda kutuma rambirambi zetu za dhati kwa familia yake tukimuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu (swt) awalipe malipo makubwa, na awape subira, ujasiri na faraja. Tunamuomba Mwenyezi Mungu abadilishe nyumba yake kwa makazi bora, na familia yake kwa familia bora, na atukusanye sisi na yeye chini ya bendera ya Mtume (saw) Siku ya Qiyamah.

 

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari  Hizb ut Tahrir

Kenya