Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi

(مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ
وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلاً)

“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Al-Ahzaab: 23]
(Imetafsiriwa)

Tunaomboleza kwa masikitiko na huzuni kubwa kifo cha ndugu yetu mpendwa Aliyev Sharifullah, ambaye alibeba ulinganizi bila kuchoka na kwa hiari kuuamsha Umma wa Kiislamu na kutumia maisha yake kubeba ulinganizi huu.

Aliyev Sharifullah, ambaye alizaliwa katika mji wa Khujand, mji mkuu wa jimbo la Tajik la Sughd, mnamo 1978, alipata ufahamu wa maoni ya Hizb ut Tahrir mnamo 1998, na akaanza kufanya kazi kwa bidii kurudisha tena mfumo kamili wa maisha ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume.

Kazi ya ndugu yetu katika safu za Hizb ut Tahrir haikuwa mbali na macho ya serikali dhalimu ya Tajik, iliyo ongozwa na Imam Ali Rahmon. Alikamatwa mnamo 2000 kwa mashtaka ya uongo ili kuzuia shughuli zozote za Dawah. Sherifullah hakuacha shughuli yake hata baada ya kutumikia kifungo chake gerezani chini ya hali za kinyama. Hakujali hata kidogo juu ya ukandamizaji wa mkandamizi, wala kulaumiwa na watu kwa ajili ya ulinganizi. Hii ndiyo sababu, serikali hii dhalimu ilimfunga mara mbili pia baada ya kuachiliwa kwake kutoka gerezani. Ndugu yetu alitumia miaka 13 na nusu ya maisha yake katika magereza ya kikatili ya serikali ya Tajik. Lakini mashtaka yake hayakuvunja azimio lake, badala yake. Ndugu yetu aliendeleza shughuli zake kwa ujasiri na dhamira baada ya kutumikia kifungo chake chengine gerezani mapema mwaka wa 2020.

Cha kusikitisha, mateso ya kikatili katika magereza ya dhalimu, na ukosefu wa huduma ya kutosha ya afya ya kibinadamu imeathiri afya ya ndugu yetu. Sharifullah alifariki mnamo 1/1/2021.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) ammiminie ndugu yetu Aliyev Sharifullah, rehema zake pana, na kwamba aingie Peponi pamoja na Manabii, Wakweli, Mashahidi, Wema, na wao ndio wandani bora. Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) aipe familia yake uvumilivu na faraja.

Licha ya huzuni yetu kubwa kwa kifo cha ndugu yetu mheshimiwa, Sharifullah, tunasema tu yale yanayomridhisha Mola wetu Mtukufu, (إِنَّا للهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ) “Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [al-Baqara: 156].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kyrgyzstan