Tofauti kati ya Ubinafsishaji, Utaifishaji na Iqta’ (Ugavi wa ardhi)

Ufupisho wa Suali na Jawabu – 16

Suali

Nini tofauti kati ya ubinafsishaji katika mfumo wa urasilimali na Iqta’ (ugavi wa ardhi) uliotajwa katika kitabu cha Mali ya Serikali ya Khilafah?

Jibu

  1. Kuna aina tatu za umilikaji: Mali ya Ummah, Mali ya Serikali ya Khilafah na Mali ya Mtu Binafsi.
  2. Mali ya Ummah ni vitu ambavyo Muumba amevifanya umilikaji wake ni wa Waislamu wote. Na kuwaunganisha katika umilikaji na kuzuia watu binafsi kumiliki mfano vizalishavyo umeme, kawi, viwanda vya gesi, makaa na madini ambayo yako kwa wingi na hayaishi ima yaliyo imara kama dhahabu, chuma au majimaji kama mafuta, gesi mfano gesi ya kawaida, bahari, maziwa, misitu, misikiti vyote hivyo na mfano wake ni Mali ya Ummah inamilikiwa na Waislamu wote, umiliki wa pamoja na ni mapato ya Bait ul Mal ya Waislamu,wakiganyiwa na Khalifah kwa mujibu wa Shari’ah. Mali hii Khalifah haruhusiwi kumpa umilikaji mtu yeyote ima mtu binafsi au kikundi maanake ni ya Waislamu wote kwa pamoja.
  3. Mali ya Serikali ya Khilafah ni chochote katika ardhi au jengo linalohusiana na haki ya Waislamu wote; inatenganishwa na Mali ya Ummah. Mali ya Serikali inaweza kuwa ardhi, majengo, vitu vya kuhamishika ambavyo vimefungamanishwa na haki ya Waislamu jumla kwa mujibu wa Shari’ah. Khalifah ana mamlaka ya kusimamia, kuichunga na kufanya maamuzi kuhusiana na mali hiyo. Mali hii Khalifah anaruhusiwa kupeana umiliki wake mtu yeyote, kupeana hatimiliki na manufaa au manufaa bila umiliki au kuruhusu waziboreshe na wazimiliki, na anaweza kuitumia katika njia anayoona ni kwa maslahi ya Waislamu. Khalifah ameruhusiwa kupeana umilikaji wa ardhi kwa ambaye hana ardhi ya ukulima, mtu huyo ailime na iwe mali yake. “ili yasiwe yakizunguka baina ya matajiri tu miongoni mwenu.” [Al-Hashr: 7]
  4. Khalifa hana ruhusa ya kuchukua mali ya mtu binafsi na kisha kumpa mtu mwengine, lakini anweza kupeana kutoka katika Mali ya Serikali na kuwapa masikini na sio matajiri ambayo inaitwa utengaji wa ardhi. Iqta (ugavi wa ardhi) unachukuliwa kutoka katika ardhi ya Serikali na sio kutoka katika ardhi ya mtu binafsi na pia sio kutoka katika Mali ya Ummah.
  5. Mali hizi zimewekwa na Shari’ah hairuhusiwi kubadilisha mpangilio wake, kiasi kwamba Mali ya Ummah kubadilishwa na kuwa Mali ya Mtu Binafsi. Mfano kupeana haki za kutafuta na kuchimba mafuta kwa kampuni binafsi inayoitwa “ubinafsishaji” huku ni kuibadilisha Mali ya Ummah na kuifanya kuwa ya Mtu Binafsi. Vivyo hivyo hairuhusiwi kuhamisha umiliki wa Mali ya Mtu Binafsi na kuifanya kuwa Mali ya Serikali. Mfano kutumia nguvu kuchukua duka la mtu na kulifanya la Serikali inayoitwa “utaifishaji”

Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye Hekima.

Link ya Kiengereza: http://hizb-ut-tahrir.info/en/index.php/qestions/jurisprudence-questions/12193.html

30 Shaaban 1439 Hijria                                     

16 Mei 2018 Miladi                              Chanzo: Hizb ut Tahrir Kenya