Taarifa kwa Vyombo Vya Habari
Huku Kenya ikigubikwa na mrundiko wa deni la jumla ya Sh. 10 trilioni, Rais William Ruto amawataka wakenya wawe wakilipa ushuru vilivyo. Kulingana na rais, serikali inanuia kukusanya sh.2 trillioni kwa mwaka ujao. Rais amewataka raia wawe na tabia ya kulipa ushuru ipasavyo ili kusaidia serikali kulipa deni lake na kuikomboa kutokana na zigo hili. Kwa sasa Serikali inatumia sh.1 trilioni kulipia mikopo
Hizb ut-Tahrir Kenya ingependa kubaini yafuatayo:
Deni la kitaifa lililokopwa kutoka mashirika ya kifedha ya Kimataifa linazidi kuongezeka kila mwaka. Kenya inahitaji kwa sasa kukopa kitita cha sh.900 bilioni kugharamikia mahitaji yake ya kifedha hatua ambayo ni suluhisho la muda ambalo kiuhalisia wake litaletea nchi masharti magumu yatakayodhalilisha zaidi na kujipata kwenye madeni zaidi hali itakayopelekea nchi kufilisika hatimaye kujihatarisha zaidi. Ni bayana kwamba sera kandamizi zinazochukuliwa na serikali kutoka kwa shirika la IMF na benki ya Dunia hubebesha raia mzigo mzito wa kiuchumi.
Chanzo muhimu cha kukusanya mapato ya serikali ndani ya Ubepari ni utozaji ushuru na ukopaji. Kulipisha ushuru matumizi na mapato ndio hufanya raia wa kawaida kulemewa katika harakati zao za kiuchumi siku baada ya siku kwani haya ndio mahitaji muhimu kwa maisha ya kila siku. Kama zilivyo tawala za kirasilimali, Kenya inafuata kila kiitwacho mfumo wa utozaji ushuru uliojikita zaidi kwenye utozaji wa ushuru kwenye mapato ya wafanyakazi na wafanyabiashara. Ni wazi kwamba bajeti za kuendesha gharama za serikali ndani ya mfumo wa kibepari hutegemea pakubwa utozaji mkubwa wa ushuru huku nakisi kwenye bajeti ikisimamiwa na Mikopo na ruzuku.
Tunasema majiribio na juhudi za serikali ya sasa yatazalisha madeni hivyo na kuzalisha majanga na kuwafanya raia wazidi kuumia kiuchumi.
Uislamu ndio suluhisho pekee la kumkomboa mwanadamu kwenye masaibu haya ya kiuchumi yaliyosheheni katika mfumo wa kirasilimali, hii ni kuwa Uislamu huhakikisha kwamba mali yote ya umma hutumika katika kuwahudumikia umma. Kipengele hiki kimsingi kinaondoa kodi kama chanzo kikuu cha mapato hivyo kuacha matumizi na mapato yakisukumwa tu na nguvu za soko ( mahitaji na usambazaji). Na kwa msingi huu, Serikali ya Khilafah (Ukhalifa) juu ya utaratibu wa Utume ndio itakayo kuwa na uchumi wakipekee utakaoweza kuwanasua wanadamu kwenye utumwa wa kiuchumi wa kikoloni wa madola ya Magharibi.
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari
Hizb ut Tahrir in Kenya