Taarifa kwa Vyombo vya Habari
(Imetafsiriwa)
Mnamo 18 Julai, katika mji wa St.Petersburg, mwanamke wa Kiislamu Jannat Bespalova (Alla Bespalova) alipatikana na hatia kwa kushiriki shughuli za Hizb ut Tahrir kutokana na kukiri kwa Bespalova juu ya mashataka hayo dhidi yake na kunyimwa haki ya kupinga uamuzi huo na mahakama haikuutilia maanani ushahidi wake na badala yake kumfunga kifungo cha miaka mitano gerezani.
Jannat alisikiza hukumu hiyo akiwa mtulivu na kupatliza nafasi ya kuwepo kwa wanahabari na kutoa shukrani zake kwa wale wote waliomuunga mkono na kumtetea katika kesi yake na kusema: “Mwenyezi Mungu awalipe khair.”
Kwa upande mwingine, tunawashukuru Waislamu wote ulimwenguni kote waliomuunga mkono dada yetu Muislamu na kupinga dhidi ya kushikwa kwake na sera mbaya ya Urusi dhidi ya Uislamu.
Mwaka uliopita, mumewe Jannat, Issa Rahimov, alishikwa kwa mashtaka ya kuandaa shughuli za Hizb ut Tahrir. Alihukumiwa kifungo cha miaka 12 gerezani pamoja na kazi ngumu, na hivi sasa mkewe naye amefungwa. Hii inaonyesha sura halisi ya Urusi ya zama hizi ambapo mambo yamebadilika; wahalifu walivyo na nguvu za kupindukia na wanalindwa na sheria, ilhali Waislamu mukhlisina wanatupwa magerezani kwa sababu ya kutaka kuishi kwa mujibu wa neno la “La ilaha illa Allah” (hakuna mungu isipokuwa Allah).
Mwenyezi Mungu yuasema:
﴾وَمَا نَقَمُوا مِنْهُمْ إِلَّا أَنْ يُؤْمِنُوا بِاللهِ الْعَزِيزِ الْحَمِيدِ﴿
“Nao hawakuona baya lolote kwao ila kuwa wakimuamini Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Msifiwa,” [A-Buruj: 8]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Urusi
H. 5 Dhu al-Qi’dah 1439 | Na: 1439 AH/12 |
M. Jumatano, 18 Julai 2018 |