Uzushi wa Gazeti la Al-Sharq Al-Awsat Dhidi ya Hizb ut Tahrir

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
(Imetafsiriwa)

Shukrani ni kwa Allah kwamba mzozo baina ya haki na batil umefichuka. Hakuna udhuru kwa gazeti la Al-Sharq Al-Awsat, linalochapishwa na Kampuni ya Utafiti na Uchapishaji ya Saudi, kupigia debe urongo wa vyombo vya udhalimu vya serikali ya Putin ya Urusi, uliopitiliza zaidi ya serikali ya Kistalini katika uhalifu.

Gazeti hili haliku nukuu tu pekee Taarifa ya Afisi ya Hudumu ya Usalama ya Kifederali ya Urusi (FSB) juu ya ukamatwaji wa mwanachama wa Hizb ut Tahrir katika eneo la Waislamu la Tatarstan, (katika toleo lake Na. 14563, Ijumaa 2/Safar 1440H – 12/Oktoba 2018M), bali liliongeza tuhuma zaidi dhidi ya chama hiki, na kuchapisha uzushi kuwa “kinatumia vitendo vya kigaidi kufikia lengo lake”, likiongeza, “Ni wazi kuwa Hizb ut Tahrir mbali na juhudi zake za kusajili Waislamu zaidi nchini Urusi na kuandaa halaqaat zilizounganishwa na miundo ya ngazi za uongozi, imekuwa ikiyasaidia mashirika na makundi haramu ya kigaidi eneo la Mashariki ya Kati kwa watu wenye kujitolea muhanga baada ya kuwakinaisha kutekeleza vitendo vya kigaidi”. Gazeti hili pia lilizuia maoni juu ya ripoti hii katika tovuti yake, tulipotaka kuweka maoni yetu, kama tulivyo fanya kwa tovuti zote zilizo chapisha ripoti hii, lakini hatukuweza kutuma maoni yoyote kwa tovuti ya Al-Sharq Al-Awsat!!

Sasa basi tunajiuliza je tupambane na askari wahalifu wa serikali ya Putin, wanaojitolea kikamilifu kuzima nuru ya Allah, asubuhi na jioni, na kutekeleza msako wa kinyama juu ya Waislamu, na kuyachukulia matakwa yao ya kutekeleza sheria ya Allah kuwa uhalifu unaostahiki adhabu kadha wa kadha AU tufichue urongo na kupinga uzushi wa Kampuni ya Utafiti na Uchapishaji ya Saudi inayo milikiwa na msaliti wa Misikiti Miwili Mitukufu, anayetumia mwito kalima ya ‘La ilaha illa Allah’!   kufichia kihyana yake.

Hakuhitajiki juhudi kubwa kupinga tuhuma za urongo za gazeti hili na uzushi wa wazi kuwa Hizb ut Tahrir inatumia ugaidi kufikia lengo lake. Chama hiki kiko wazi katika ulinganizi wake wa neno la haki, bila ya kuogopa serikali ya Putin na wenzake, serikali dhalimu katika biladi za Waislamu. Kuanzia kuasisiwa kwake chama hiki kimetangaza kuwa kinatafuta kurudisha maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamisha dola ya Khilafah, kwa kufuata njia ya Utume iliyo jengwa juu ya msingi wa mvutano wa kifikra na wa kisiasa, na kufanya kazi na Umma na kuusihi kufanya kazi ili kutekeleza sheria ya Allah. Hili si jipya, wala kufeli kwa serikali zote za kihalifu kukivunja moyo kutokana na kazi yake, licha ya juhudi kubwa na za kuendelea zinazo fanywa. Hii ni kwa sababu ya kazi ya waumini wanaume wanao muamini Allah na Mtume Wake, walio amua kubeba mzigo huu wa amana, ambao Allah ameukirimu Waislamu kwao, yaani ulinganizi wa Dini Yake na utekelezwaji wa sheria Yake, na kuchukua dori ya kuwa mashahidi wa wanadamu kupitia kulingania ulinganizi wa Uislamu kama ilivyo elezwa katika maneno ya Allah (swt):

وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطاً لِّتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ وَيَكُونَ الرَّسُولُ عَلَيْكُمْ شَهِيداً﴿

“Na vivyo hivyo tumekufanyeni muwe Umma wa wasitani, ili muwe mashahidi juu ya watu, na Mtume awe ni shahidi juu yenu.” [Al-Baqara: 143]

Kwa kuwa jukumu liko kwa mwenye kutuhumu kutoa ushahidi wake, tunatoa changamoto kwa Al-Sharq Al-Awsat kuwasilisha ushahidi wake kuthibitisha madai yake ya urongo kuwa Hizb ut Tahrir inatekeleza vitendo (vya kigaidi), ikiwa halitafanya hivyo, na wala halitafanya, basi tunawalingania waumini mukhlisina kuwahisabu wahariri wa gazeti hili linalo eneza urongo kuhusu wabebaji Da’wah na kupigia debe urongo wa maadui wa Dini hii. Gazeti hili lilisema kuwa eneo la Waislamu la Tatarsatan kama la “Urusi”! ikiwanyima watu wake hadhi ya Uislamu! Ardhi hii na watu wake walioingia katika Uislamu kwa ari ni waumini wanao shikamana na Dini yao, wakiihami kwa kila walicho nacho. Tunamuomba Allah (swt) atulipizie kisasi gazeti hili, na mifano yake, ambayo ndiyo midomo ya uovu wote dhidi ya Uislamu na Waislamu. Tunasadiki na kuiamini nusra ya Allah hata kama makafiri na wanafiki, maadui wa Umma huu ambao ni miongoni mwa watoto wa Umma huu, wanachukia hili. Sifa njema zote ni za Allah aliye kidhia nusra kwa waumini, na kwa Allah tunategemea, Yeye ndiye msaidizi bora.

إِنَّا لَنَنْصُرُ رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ يَقُومُ الأَشْهَادُ﴿

“Hakika bila shaka, Sisi tunawanusuru Mitume wetu na walio amini katika uhai wa duniani na siku watakapo simama Mashahidi.” [Ghafir: 51]

وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ﴿

“Na siku hiyo Waumini watafurahi. Kwa nusra ya Allah humnusuru amtakaye.” [Ar-Rum: 4-5]

 Dkt. Osman Bakhach
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir