Wajumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Kenya Wakutana na Wanazuoni Mashuhuri wa Kiislamu

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

(Imetafsiriwa)

Wajumbe kutoka Hizb ut Tahrir/Kenya wakiongozwa na Ustadh Mahd Ali – Mkuu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir nchini Kenya akifuatana na Ustadh Yusuf Ghasani na Ali Mwangi ambao wote ni wanachama wa Hizb ut Tahrir, walikutana na viongozi kadhaa mashuhuri wa Kiislamu walioko Mji Mkuu wa Kenya Nairobi miongoni mwao:

Naibu Kadhi Mkuu wa Kenya Sheikh Sukyan Hassan Omar

Sheikh Juma Amir Imam Msaidizi wa Msikiti wa Jamia, Nairobi

Daktari Mbarak Ahmed Awes Imam Msikiti wa Al-Hudaa South B Nairobi

Wajumbe hao wa Hizb walipokelewa kwa mapokezi mazuri. Mkuu wa wajumbe hao, Ustadh Mahd Ali aliweza kushiriki majadiliano yenye maana na viongozi hao kuhusu LGBT na Da’wah ya Kiislamu kwa jumla. Aliwapa nakala ya kitabu, Khilafah, chapisho la Hizb ut Tahrir kinachoelezea ufaradhi juu ya Waislamu wa kusimamisha tena Khilafah.

Twamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu azifungue nyoyo za Maulamaa wafanye kazi na Hizb ut Tahrir katika kufikia lengo la kurudisha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu kwa kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa Njia ya Utume.

 

Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir
Kenya