Wakoloni wa Magharibi Kufadhili Elimu ili Kuendeleza Utumwa wa Kifikra

Habari:

Mnamo Ijumaa, 11 Juni 2021 Rais Uhuru Kenyatta alimpongeza Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson kwa kuahidi milioni £430 (takribani bilioni Ksh65) kwa kampeni ya Ushirikiano wa Kimataifa kwa ajili ya Elimu. Rais alisema kwamba Kenya inamshukuru Waziri Mkuu Boris Johnson na Uingereza kwa kuongoza mwito wa kufadhili elimu na kuwaunganisha viongozi wa dunia katika G7 na wengineo ili kuwekeza zaidi katika elimu kama njia ya kuongoza katika afueni na kujenga ubora wa kimataifa baada ya janga la Covid-19. [The Star, 11/06/2021]

Maoni:

Kwa hakika elimu ni moja katika zana msingi ambazo wakoloni wa Magharibi wanaendelea kuipatiliza katika kuyatia minyororo makoloni yao ya zamani. Ni kupitia elimu ndipo wakoloni wa Magharibi wanaendelea kutawala nchi za ulimwengu wa tatu kwa njia isiyokuwa ya moja kwa moja. Ili kuwadhibiti na kuwakoloni watu wa kiasili, wa Magharibi walianzisha utaratibu wa mchakato wa kuwaunganisha na moyo wake ukiwa ni elimu ya kisekula. Kuwaunganisha ilimaanisha wanaokoloniwa kulazimishwa kuendana na thaqafa na desturi ya wa Magharibi wakoloni.

Kilele cha uunganishaji kilikuwa ni udhibiti wa kithaqafa. Uthibiti wa kithaqafa umebakia ni mbinu ya kisiasa iliyo na ufanisi hadi sasa. Kwani inafanyakazi kwa kuridhia na aghalabu hutangulia uvamizi wa kinguvu. Hivyo basi, tawala za kikoloni za Magharibi zilipata nguvu kubwa sio kupitia udhibiti wa kimwili, bali kupitia udhibiti wa kifikra. Walisonga mbele na kutekeleza udhibiti huu hadaifu kupitia eneo la kujumuisha kifikra linalojulikana kama utaratibu wa shule.

Utaratibu wa shule unaendelea hadi sasa kutumika kuwaandaa watawala vibaraka wa kikoloni ambao wanapewa madaraka kupitia mlango wa nyuma kwa jina la ‘uhuru bandia wa bendera!’  kwa sharti kwamba watekeleze vipaumbele vya mabwana zao. Kwa hiyo, watawala vibaraka watiifu wa kikoloni wanaendelea kufuata nyayo za mabwana zao wa kikoloni wa Magharibi kwa kubuni sera na kanuni ambazo zinaongozwa kwa maslahi yao! Wale wanaoitwa wachache waliopendelewa na wafanyikazi wa serikali wanajivunia mabwana zao wa Magharibi kiasi kwamba wanakejeli thaqafa yao na raia wenzao!

Nia ovu kabisa ya elimu ya kikoloni ya kisekula ilifichuliwa na Thomas Babington Macaulay, pale aliposema, “Lazima hivi sasa tufanye kazi nzuri ya kubuni tabaka la watakao kuwa wakalimani baina yetu sisi na mamilioni ambao tunawatawala; tabaka la watu ambao kwa damu na rangi ni Wahindi, lakini Waingereza kihisia, kimtazamo, kimaadili na kifikra.” Kwa maneno mengine, Macaulay alimaanisha kwamba miundo ya kujifunza ya asili ibadilishwe kwa ile ya wakoloni wa Magharibi! Dhati yake ikiwa ni kukuza vitambulisho vya kisekula vya kirasilimali!

Kwa kuzingatia ufupisho huo hapo juu, hakuna kheri inayotarajiwa kutokana na ahadi ya kifedha. Kwani Kenya imebakia kuwa koloni la Uingereza kwa njia isiyokuwa ya moja kwa moja. Pasina shaka huu mzunguko mpya wa msaada wa kielimu ni mbinu nyingine ya kikoloni kuwadhoofisha na kuwafanya watumwa raia wa koloni ili kubakia ndani ya sanduku la kisekula la kirasilimali! Hivyo basi, haishangazi kattu kwamba bwana Mkoloni na meneja wake kuwa wenyeji wa kongamano la siku mbili kuhusu ushirikiano wa kimataifa kwa ajili ya ufadhili wa elimu mnamo 25 – 26 Julai 2021. [The Star].

Iko njia moja pekee ya kupambana na hii kampeni ya elimu ya kisekula ya kikoloni ya wa Magharibi.  Ni kwa kukumbatia na kufanyakazi ya mradi wa Khilafah. Mradi wa kimataifa unaongozwa na Hizb ut Tahrir. Chama cha kimataifa cha Kiislamu cha kisiasa ambacho kina jitahidi usiku na mchana ili kurudisha maisha ya Kiislamu kwa kurudiha tena Khilafah. Khilafah itatekeleza nidhamu ya elimu ambayo imechipuza kutoka kwa msingi wa itikadi (aqeedah) ya Kiislamu. Lengo la elimu ndani ya Khilafah litakuwa ni kujenga utambulisho (shaksiyyah) ya Kiislamu kifikra na kitabia. Hivyo basi, masomo yote katika mtaala yatachaguliwa kwa msingi huo. Kwa hiyo, itikadi ya kisekula, fikra za kidemokrasia, huria n.k. HAZITOKUBALIWA kama ilivyo leo ndani ya nidhamu zetu za elimu!

Elimu ndani ya Khilfah itakuwa ndio njia ya kuhifadhi thaqafa ya Ummah ndani ya mioyo ya watoto wake na kurasa za vitabu vyake, ima ni katika mtaala wa elimu uliopangiliwa. Mtaala wa elimu inamaanisha elimu iliyopangiliwa na nidhamu na kanuni ambazo Khilafah imejifunga nazo. Khilafah itakuwa na wajibu wa kuitekeleza mfano kuweka umri wa kuanza kusoma, masomo ya kufundishwa na njia ya elimu. Ilhali elimu ambayo haikuwekewa mpangilio itawachiwa Waislamu kufundisha majumbani, miskitini, vilabuni, kupitia vyombo vya habari na machapisho ya mara kwa mara. Hata hivyo, katika hali zote hizo Khilafah itakuwa na wajibu wa kuhakikisha kwamba fikra na maarifa (yanayo fundishwa) ima yanachipuza kutoka katika itikadi ya fikra ya Kiislamu au imejengwa juu yake. [Misingi ya Mtaala wa Elimu katika Dola ya Khilafah]

Imeandikwa kwa ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Ali Nassoro Ali

Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir