Wala Msiwe Katika Washirikina Katika Wale Walioitenga Dini Yao Na Wakawa Makundi Makundi Kila Kikundi Kinafurahia Kilicho Nacho

Taarifa kwa Vyombo Vya Habari

Hatua ya mahakama ya juu kuamuru marudio ya uchaguzi Oktoba 26, 2017 imezusha fukuto la kisiasa nchini. Baada ya kuubatilisha uchaguzi wa mwezi Agosti 2017, kumeshuhudiwa vuta ni kuvute juu ya usimamizi wa uchaguzi mpya baina ya mirengo miwili ya kisiasa (Jubilee na Nasa). Jubilee inaonekana kutokuwa na wasiwasi juu ya tume ya IEBC; imezama katika kampeni za kuwataka watu kushiriki katika uchaguzi. Kinara wa Nasa Raila Odinga ambaye aliyejitoa kwenye uchaguzi amekuwa akiwasihi wafuasi wake kususia kura kwa msingi kuwa IEBC kattu haiwezi kuendesha uchaguzi wa huru na haki. Huku haya yakijiri, wabunge wa Jubilee ambao ndio wengi bungeni tayari wamependekeza marekebisho ya kanuni za kiuchaguzi yanayolenga kuzuia mahakama kubatilisha matokeo ya kura. Aidha, merekebisho hayo ni kuwa mgombezi yoyote atakayejitoa kwenye marudio ya uchaguzi basi aliyebaki atangazwe mshindi moja kwa moja.

Harakati ya Kiislamu ya Hizb ut Tahrir Kenya ingependa kusema yafuatayo:

Malumbano haya baina ya wanasiasa hayafaidishi mwananchi wa kawaida kwa hali yoyote ile isipokuwa kumzidishia kero baada ya kero. Haya ni mashindano baina yao  juu ya kufikia uwezo wa kisiasa na hata wa kiuchumi  kwa lengo  la kupata  maslahi tu baina yao wala sio kwa maslahi ya raia walala hoi.  Vinara wa mirengo yote hii sio wageni machoni mwa raia bali wote wemehudumu katika serikali zilizopita na wakapora mabilioni ya pesa za umma. Hakuna miongoni mwao walio na nia kweli ya kutatulia raia matatizo msingi licha ya Kenya kuwa moja wapo ya nchi duniani zilizo na pengo kubwa baina ya matajiri na masikini.

Mzozo huu unadhihirisha kushindwa kwa mfumo wa kibepari na siasa yake ya kikoloni ya Kidemokrasia. Isitoshe, hali hii imefichua kasoro kubwa ya asasi kuu za tawala za Kidemokrasia ikiwemo katiba na mahakama. Wanademokrasia baada ya kudharau sharia za Mwenyezi Mungu hujitungia katiba kisha wenyewe huzidharau huku kila mmoja akiifasiri atakavyo ili kuridhisha upande wa kisiasa! Na mgongano baina ya Bunge na Mahakama kama ilivyodhihirika pale wabunge wa mrengo wa Jubilee kupendeza marekebisho ya kanuni za uchaguzi za kudhoofisha uwezo wa mahakama! Kisha pasina na hata chembe ya haya wanademokrasia hudai kuwa mahakama ni huru hazifai kuingiliwa! La hatari zaidi, ni mahakama ya juu kutofautiana katika uamuzi wa kesi huku majaji wakitoa hukumu zinazogongana! Licha ya aibu na fedheha zote hizi bado mataifa ya kimagharibi kupitia mabalozi wao kwa jeuri na kiburi chao hawasiti kuingilia masuala ya ndani ya Kenya na kujifanya wanahuruma nayo ilhali ukoloni wao mambo leo ikiwemo Demokrasia yao ndio chanzo cha majanga yote kote.

Masikitiko ni kuwaona wasomi na wadadisi nchini Kenya hadi sasa bado wanaendelea kutekwa na urongo wa Demokrasia. Na lakutia machungu zaidi ni kuwaona viongozi wa Kiislamu wakijigawa kimakundi kila kundi la masheikh likisherehekea na kufurahia urongo wa Demokrasia na wanasiasa wake.

Mwisho twaonya jamii ya Kenya na hasa ya Kiislamu kutekwa na miito ya chuki ya wanasiasa ya kugawanya raia kwa lengo la kufikia maslahi yao ya Kisiasa. Huu ni wakati mwafaka wa jamii ya Kiislamu kuonyesha uwezo wa Uislamu na mafundisho yake ya kutatua matatizo yanayokumba Kenya bali dunia nzima.

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari Hizb ut Tahrir Kenya

KUMB: 01 / 1439 AH

Jumanne, 04 Safar 1439 H

24/10/2017 M

 

Simu: +254 707458907

Pepe: mediarep@hizb.or.ke