Taarifa kwa Vyombo vya Habari
(Imetafsiriwa)
Kwa mujibu wa ripoti ya UN ya hivi karibuni zaidi ya raia 350 wameuliwa ndani ya Idlib na watu 330,000 wamelazimishwa kukimbia nyumba zao tangu kuzidi kwa mapigano kuanzia 29 Aprili. Lakini takwimu hizi zimebadilishwa kwa mujibu wa afisaa mkuu wa UN. Aliongezea kwamba vifo 103 vilitokea ambavyo vilijumuisha watoto 26 kwa mashambulizi ya angani kwa hospitali, shule, soko na viokaji mikate ndani ya kaskazini magharibi ya Syria zaidi ya siku 10 zilizopita na alikadiria zaidi ya watu 400,000 wamefurushwa…
Mbele ya macho na masikio ya dunia yote na uangalizi mkubwa, vita viinaendelea kwa kudumu na pamoja navyo raia wanaendelea kuuliwa ndani ya Idlib na kuwalenga watoto wasiokuwa na hatia hata wakiwa shuleni. Mashambulizi yanaendelea dhidi ya huduma zote msingi zikijumuisha hospitali na shule. Shirika la Okoa Watoto lilionya kwamba idadi ya watoto wanaouliwa ndani ya Idlib zaidi ya wiki nne zilizopita imepita idadi ya vifo katika eneo hilo ndani ya mwaka mmoja uliopita.
Maangamizi ya kupangiliwa na ya kimakusudi yanalenga raia wasiokuwa na hatia ndani ya Idlib, ambayo ni eneo la mwisho kukombolewa kutoka kwa utawala na likiwa na idadi kubwa ya watu waliofurushwa inaonyesha kwamba vita dhidi ya watoto havijaisha na havitosita licha ya maombi ya mashirika haya na ripoti mtawalia na licha ya makongamano au njama za wanasiasa wa Kimagharibi kwa sababu ni vita dhidi ya Uislamu na Waislamu ambao wamenyanyua bendera ya Tawhid. Ni vita vilivyo tangazwa na wale ambao hawatambui ubinadamu na ambao wanaitizama damu ya watoto wetu ni duni thamani na wanaitumia ili kujadiliana namna ya kuwaangamiza wanamapinduzi ili kupitisha mikataba ya aibu na udhalilishaji ili kuondosha maeneo yote yaliyo kombolewa. Haya yanafanyika ilhali watu wanekwenda mbio kuuangusha utawala ambao hauwezi kuanguka isipokuwa kwa kuunganisha ngome zote kwa muungano wa viongozi wa makundi na kukataa ahadi duni na kunyanyua mwito wa kwanza wa mapinduzi “ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.”
Mpaka lini, Enyi mashirika tathmini zenu zitaendelea kupunguza na kuongeza nambari kila siku, mwezi na mwaka katika takwimu za vifo vya watoto wasiokuwa na hatia ndani ya Syria?!
Mpaka lini, Enyi watawala na vibaraka, macho yenu yataendelea kuwa na upofu kutokana na picha za mabaki ya watoto wetu?! Na masikio yenu yamekuwa viziwi hamusikii maombi na mayowe yao? Na ndimi zenu zimenyamazishwa ili msiwanusuru mayatima na wanaokandamizwa? Haya ni maswali ya balagha ya kuwalaani! Inawezekanaje kutarajia mema kutoka kwa watu waovu?! Inawezekanaje wakandamizaji kupeana haki?
Kwanza tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) ili kuondosha hili wingu jeusi kutoka kwa wetu wa Ash-Sham na kisha kutoka katika Ummah huu mtukufu na kuunganisha tena na kuurudisha kuwa mwili mmoja na kuunganisha majeshi na kuwa na usimamizi wa mambo yao.
Hii ndio hali yetu ambapo hatuna dola inayotulinda na kuangalia mambo yetu…Hii ndio hali yetu pasina kuweko Khalifah anayetuongoza na kutunusuru…Hii ndio hali ya maadui wa Uislamu na Waislamu ambayo Mwenyezi Mungu (swt) ameielezea:
﴾وَلَا يَزَالُونَ يُقَاتِلُونَكُمْ حَتَّى يَرُدُّوكُمْ عَن دِينِكُمْ إِنِ اسْتَطَاعُوا﴿
“Wala hawatoacha kupigana nanyi mpaka wakutoeni katika Dini yenu kama wakiweza.” [Al-Baqara: 217].
Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
H. 5 Dhu al-Hijjah 1440 | Na: 1440 A / 039 |
M. Jumamosi, 10 Agosti 2019 |