Ziara ya Ujumbe kutoka Hizb ut-Tahrir / Wilayah ya Lebanon Kwenda kwa Kadinali wa Patriaki Mar Bechara Boutros al-Rai Na Kumkabidhi Barua ya Wazi

Taarifa ya Habari

(Imetafsiriwa)

Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Lebanon, ukiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Mawasiliano, Dkt. Muhammad Jaber, na wanachama walijumuisha Mhandisi Salah al-Din Adada, Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir, na ndugu Swaleh Salam na Bilal Zidan, ambao wote ni wahandisi na Dkt. Muhammad al-Buqai, ​​wanachama wa Kamati kuu ya Mawasiliano, na mwanachama wa Hizb, Ahmed Al-Abdullah; ulimzuru Kadinali wa Patriaki, Mar Bechara Boutros Al-Rai, adhuhuri ya Jumanne, 28 Jumada Al-Awwal 1442 H, sawia na 12/1/2021 M.

Ujumbe huo uliwasilisha kwa Kadinali wa Patriaki na waliohudhuria barua ya wazi, yenye anwani tatu kuu:

Kwanza: Uislamu na Wakristo baina ya maandiko ya Sharia na utendaji wa kihistoria, ambapo kwayo ilihakiki uhusiano na wasiokuwa Waislamu, haswa Watu wa Kitabu, kama inavyoona Hizb ut-Tahrir kutoka katika maandiko ya sheria ya Kiislamu, na utabikishaji wake kivitendo katika kipindi chote cha historia, kupitia watawala, wanachuoni na viongozi wa Dola ya Kiislamu, ambayo Hizb inaifuata ili kunali lengo lake la kusimamisha dola ya uadilifu na mwongozo, Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume.

Pili: Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Lebanon, amali zake na kazi yake, ambapo iliwasilisha ufafanuzi wa Hizb ut-Tahrir / Wilayah ya Lebanon kuanzia ilipo asisiwa ndani yake tangu miaka ya hamsini ya karne iliyopita, ambapo Hizb ilijitenga na vita vya wenyewe kwa wenyewe, kutokana na kushiriki kwa dola fisadi katika utawala, na kuifunga kazi yake katika mvutano wa kifikra na mapambano ya kisiasa dhidi ya mamlaka, iliyafanya maslahi ya watu wa Lebanon na eneo hilo kipaumbele chake, na kumakinika juu ya fikra na njia yake, ikituliza macho yake juu yake, na Hizb ikategemeza yote haya juu ya Aqeeda na Sheria ya Kiislamu.

Tatu: Hizb ut-Tahrir / Wilayah ya Lebanon, mtazamo wake na maono ya uhalisia wa kisiasa wa Lebanon, ambapo iliwasilisha maoni ya Hizb ut-Tahrir / Wilayah ya Lebanon – kama chama cha kisiasa ambacho kinatabanni itikadi ya Kiislamu kama msingi wa fikra yake – hali ya kisiasa nchini Lebanon, maoni yake juu ya masuluhisho yaliyowasilishwa, na mtazamo wake wa suluhisho msingi kwa kadhia ya Lebanon mkabala na masuluhisho ya viraka yaliyo peanwa.

Yote haya yamefafanuliwa kwa kina katika barua hiyo ya wazi, ambayo ujumbe uliiwasilisha kwa Kadinali na, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, itawasilishwa kwa waandishi wa habari na kuwekwa kwenye tovuti rasmi za Hizb ut Tahrir.

Barua hiyo ya wazi, ambayo mwisho wake ilikuwa na nukta vifupisho, kama ifuatavyo:

Kwanza: Wito kwa Kadinali Uislamu kulingania kwa kutegemea maneno ya Mwenyezi Mungu (swt):

[قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ تَعَالَوْا إِلَى كَلِمَةٍ سَوَاءٍ بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ أَلَّا نَعْبُدَ إِلَّا اللَّهَ وَلَا نُشْرِكَ بِهِ شَيْئاً وَلَا يَتَّخِذَ بَعْضُنَا بَعْضاً أَرْبَاباً مِّن دُونِ اللَّهِ فَإِن تَوَلَّوْا فَقُولُوا اشْهَدُوا بِأَنَّا مُسْلِمُونَ]

“Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Njooni kwenye neno lilio sawa baina yetu na nyinyi: Ya kwamba tusimuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote; wala tusifanyane sisi kwa sisi kuwa Waola Walezi badala ya Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka basi semeni: Shuhudi- eni ya kwamba sisi ni Waislamu.” [Al-i-Imran: 64].

Pili: Kutosimama kama kikwazo mbele ya kukamilika kwa haiba ya Waislamu nchini Lebanon na kwengineko, kukamilika kunakowakilishwa na kuibuka kwa dola ya Uislamu katika nchi za Waislamu, ikiwemo Lebanon, dola ya uadilifu na mwongozo, Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Tatu: Kutoburuzwa nyuma ya wimbi la hofu ya Uislamu wa kisiasa, unaowakilishwa na Hizb ut Tahrir, na ambao unachochewa na magharibi ya kisekula ambayo haijui thamani yoyote ya dini, iwe ni Uislamu, Ukristo au Uyahudi.

Nne: Utambuzi kwamba Hizb ut Tahrir ni mradi wa serikali na mfumo kamili wa maisha katika nyanja zake zote za kisiasa, kiuchumi na kijamii. Siasa huonekana kama ni kuchunga mambo, na haiwezi kwa vyovyote vile kuwa kama chama cha kipeke yake kinachofanya kazi ya kusimamisha dola kwa wote kama ilivyokuwa kwa miaka yote.

Tano: Kuonya dhidi ya miradi ambayo Magharibi inaipigia debe nchini Lebanon, baada ya fukwe za Lebanon kuelea juu ya utajiri mkubwa wa mafuta na gesi, na kuifanya Lebanon kuwa lengo la matamanio katika utajiri wake, na pia tahadhari ya kutembea katika udhibiti wa Amerika wa Lebanon, au Ufaransa matata, kama upanuzi wa mapambano juu ya utajiri mkubwa wa gesi Mashariki Mediterania.

Sita: Onyo dhidi ya kuvutwa kwenye mchezo wa kisiasa ambao unataka kuiunguza nchi na kuwasha machafuko kati ya watu wake, kwa kutumia migogoro, ambayo tunaona kwamba vyama vingi vya siasa vinahusika ndani yake.

Saba: Jihadharini kwamba ikiwa kuna ukiukaji katika utabikishaji ambao Uislamu unataka, basi hii inachukuliwa kuwa ni unyanyasaji katika utabikishaji wa wale ambao wamekosea pekee, na Mwenyezi Mungu atamhesabu mkosaji kwa kitendo chake Siku ya Kiyama, kulingana na maandiko ya hadith ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw):

«أَلَا مَنْ ظَلَمَ مُعَاهِداً، أَوْ انْتَقَصَهُ، أَوْ كَلَّفَهُ فَوْقَ طَاقَتِهِ، أَوْ أَخَذَ مِنْهُ شَيْئاً بِغَيْرِ طِيبِ نَفْسٍ، فَأَنَا حَجِيجُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ»

“Tahadhari, yeyote anayemdhulumu mtu aliyehifadhiwa kwa mkataba (Mu’ahid), au akamkalifisha zaidi ya uwezo wake, au akachukua kitu kutoka kwake pasi na ridhaa ya nafsi yake, basi mimi nitakuwa mtetezi wake Siku ya Kiyama.”

Na hatuwezi kumalizia, isipokuwa kwa kumshukuru Kadinali wa Beatitude Mar Bishara Boutros Al-Rai kwa kukubali kwake ziara hii na mapokezi mazuri, tukitumai kuwa huu utakuwa mlango wa mawasiliano ya kida’wah ya kifikra yatakayokuwemo ndani yake maslahi ya Lebanon na watu wake, bali pia maslahi ya kanda na eneo.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Lebanon