Habari:
Baada ya kutangazwa matokeo ya mtihani wa KCSE mnamo Disemba 2017, vyombo vya habari nchini Kenya vimeangazia sura tatanishi ya shule, wazazi, wanafunzi na vyama vya wafanyikazi wa sekta ya elimu ambayo mwanzoni katika miaka ya 2015 na kwenda chini ili kuwa ni sura ya bashasha. Ambao leo wako kwenye huzuni na kuitisha uchunguzi wa jinsi mchakato wa usahihishaji mitihani ulivyo fanywa. Kwa upande mwengine, Waziri wa Elimu amesisitiza kuwa matokeo hayo aliyo yatangaza ni yalikuwa ni mmuliko wa hali halisi ilivyo.
Maoni:
Watahiniwa wa KCSE wa 2017 ni kipote cha nne cha elimu ya msingi bila malipo iliyo anza mwaka wa 2003, ambayo ni kilele cha uchaguzi wa kihistoria wa Mwai Kibaki kama Raisi wa tatu wa Kenya baada enzi ndefu ya miaka 24 ya Moi. Alitimiza ahadi ya kampeni yake iliyopokewa vizuri na watu lakini iliyo tokelezwa ovyo na waundaji sera, hii ikiwemo kashfa kubwa za kifedha katika wizara ya elimu iliyokuwa ikikabiliwa na shinikizo kubwa kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi waliojiunga na shule za msingi ambayo haijawahi kushuhudiwa katika historia ya Kenya. Kenya inateseka kutokana na mgogoro hatari wa kielimu ambao umepelekea vyuo vikuu na vyuo vyengine vya wastani kuzalisha wanao hitimu huku kukiwa hakuna fursa za kutosha za kazi, na hizo chache zilizoko hupatikana kupitia ukabila au hongo nk. Hili limesababisha machafuko ya kijamii ambayo hayajawahi kushuhudiwa huku vijana wakiamua kuchukua hatua zilizopitiliza mipaka ili kujikimu, ikiwemo ukahaba na uigizaji filamu za ngono, ujambazi, kiwango kikubwa cha msongo wa mawazo kwa pupa ya kutaka maisha ya kifahari nk. Hizi ni baadhi tu ya hatua hizo. Huku wale walioko katika ngazi za utawala wakishughulishwa na ufujaji mali ya umma kujibinafsisha kwa gharama ya raia kutaka mabadiliko.
Kenya kama nchi nyengineyo ya kisekula-kirasilimali ulimwenguni sera yake ya imeundwa kuweka misingi ya utumwa mambo leo katika mustakbali kwani shina lake ni ukoloni wa kimagharibi unaowatazama watu masikini kama mashini za kufanya kazi katika makampuni yao kwa mishahara na marupurupu duni. Hivyo basi, nidhamu ya elimu iliundwa kuhadaa watu kuwa wanaelimishwa kuboresha maisha yao; lakini hasha, walikuwa wakikuzwa kuwa wazuri katika kuwahudumia warasilimali matajiri na badali yake walipwe kwa kujitolea kwao katika huduma! Kwa upande mwengine warasilimali walihakikisha kuwa kujimudu kwa mtu kutategemea kudumu kuwahudumia wao.
Warasilimali walitaka watumishi wasomi na walio na stakabadhi za masomo. Lengo la elimu halikuwa tu elimu iliyo lenga kujenga na kuimarisha namna ya kufikiri na kukabili mambo kisomi katika kadhia za kijamii, bali msingi wake ulikuwa juu ya umuhimu wa kuunda fursa za kazi pekee! Kwa msingi kama huu ukiongezewa na maadili ya kimagharibi ya ukombozi na uhuru, tumeona idadi kubwa ya wasomi ambao moja kwa moja waliajiriwa katika taasisi za kirasilimali kuendeleza ajenda ya kirasilimali. Kiwango cha elimu na hususan kiwango cha chuo kuu huamua mafanikio ya mtu. Hii ilipelekea kuwepo kwa msemo maarufu “tafuta stakabadhi” kama ilivyo thibitishwa na vyuo tapeli vinavyo julikana kama vituo vya kuunda stakabadhi kutokana na kuhitajiwa sana na taasisi za kuajiri ambazo zimevutiwa zaidi na stakabadhi kuliko ‘ujuzi’ katika kipimo chao cha kuajiri. Hivyo basi, wakaanzisha mfumo wa utoaji alama katika usahihishaji mitihani na wenye kufaulu huchukuliwa ni wale wenye kupata alama za juu kwa kutumia mbinu yoyote ile iliyoko mikononi mwao hata kama itamaanisha kudanganya katika mitihani ni sawa! Kupita mitihani ni dhamana ya maisha yenye mafanikio kupitia kuajiriwa siku za mbeleni na hivyo kuifanya kuwa kadhia ya uhai au kifo.
Suluhisho ya zogo hili liko katika mfumo badili safi wa Uislamu chini ya serikali ya Khilafah ambayo chimbuko lake ni Allah (swt) Muumba wa viumbe. Anayejua lililo zuri na baya kwa viumbe vyake. Hivyo basi, itikadi ya Kiislamu ndio msingi ambao juu yake imejengwa sera ya elimu. Mtaala wa elimu na mbinu za ufundishaji zote zimeundwa kukinga kupotoka kutokana na msingi huu. Lengo la elimu ni kuzalisha shakhsiyya ‘utambulisho’ ya Kiislamu katika fikra na tabia.
Thaqafa ya Kiislamu ni lazima ifunzwe katika viwango vyote vya elimu. Katika elimu ya juu, vitengo vyapasa kubuniwa kwa kila fani ya Kiislamu kama itakavyo fanywa kwa fani ya utabibu, uhandisi, fizikia nk. Sanaa na ufundi huenda zikahusishwa na sayansi, kama biashara, unajimu na usanii na ufundi wa ukulima. Katika hali kama hizo, husomwa bila ya kikwazo wala masharti. Wakati mwengine, lakini, sanaa na ufundi zinaunganishwa na thaqafa endapo zinaathiriwa na mzatamo fulani wa kimaisha, kama vile upigaji picha na uchongaji vinyago. Ikiwa mtazamo huu wa kimaisha unagongana na mtazamo wa kimaisha wa Kiislamu, sanaa hizo na ufundi huo hauta tabanniwa. Mtaala wa elimu wa dola ni mmoja. Hakuna mtaala mwengine wa elimu utakao ruhusiwa kufunzwa isipokuwa mtaala wa dola pekee. Shule za kibinafsi zitaruhusiwa maadamu tu zitatabanni mtaala wa elimu wa dola na kubuniwa kwa msingi wa sera ya elimu ya dola na kutimiza lengo la elimu lililo wekwa na dola.
Ufunzaji shuleni humo hauruhusiwi kuwa wa mchanganyiko baina ya wanaume na wanawake, iwe kwa wanafunzi au walimu; na shule zisiwe maalumu kwa watu wa dini fulani, dhehebu fulani, tabaka fulani au rangi fulani. Ni wajibu juu ya dola kumfunza kila mtu, mwanamume au mwanamke, vitu ambavyo ni muhimu katika maisha ya kawaida. Hili lapaswa kuwa wajib na bila ya malipo katika viwango vya elimu ya shule za msingi na upili. Dola inapaswa, kwa kadri ya uwezo wake, kutoa fursa kwa kila mmoja kujiendeleza na elimu yake ya juu bila malipo. Dola itapeana maktaba na maabara na kila njia ya elimu nje ya mashule na vyuo vikuu, kuwawezesha wale wanaotaka kuendelea na utafiti wao katika nyanja tofauti tofauti za elimu, kama fiqh, Hadith na Tafsir ya Qur’an, fikra, utabibu, uhandisi na kemia, uvumbuzi, utambuzi, nk. Hili linafanywa ili kuzalisha ndani ya Umma idadi kubwa ya Mujtahidina, wanasayansi na wavumbuzi mahiri.
Ali Nassoro Ali
Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kenya