بسم الله الرحمن الرحيم
Habari:
CHRISTCHURCH, NEW ZEALAND- Mshangao, afueni na mchanganyiko wa hisia ulihanikiza taarifa ya habari siku ya Alhamisi pale Brenton Tarrant jamaa aliyetekeleza mauwaji ya kinyama kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha amani ya muda mrefu nchini New Zealand, alivyobadili ombi lake la awali la kutokuwa na hatia na kupatikana na hatia ya makosa yote yaliyowasilishwa kortini. Tarrant aliwauwa waislamu 51 na kujeruhi kadhaa katika misikiti miwili huko Christchurch mnamo Machi 15 mwaka jana. Shambulio la kwanza lilionyeshwa moja kwa moja kwenye wavuti. Raia huyo wa Australia alishtakiwa kwa idadi kubwa zaidi ya makosa ya mauaji kuwahi kuwasilishwa dhidi ya mtu katika historia ya New Zealand, ambapo kosa la ugaidi na makosa mengine 40 ya kujaribu kuua yaliongezwa. Sababu za uamuzi huo wa kushangaza wa Tarrant kubadili ombi lake na kukiri kuwa ana hatia hakujabainika; hapo awali alikuwa amekataa kuwa na hatia, na kesi yake ilikuwa imepangwa kusikizwa mwezi Juni. Habari hizo ziliibuka wakati New Zealand ilipoifunga(lockdown) nchi nzima ili kuzui kuenea kwa maradhi ya Corona. (Chanzo: Reuters)
Maoni:
Mwaka mmoja baada ya tukio la kigaidi la Christchurch, ustaarabu wa ulimwengu wa Magharibi ulianikwa hadharani katika madai yake yote kuwa ni mfumo wa kiulimwengu. Mfumo huu wa kibepari wa kimagharibi wenye msingi wake katika itikadi fisidifu ya kirasimali ndiyo iliokuwa kichocheo na kiini kilichosababisha tukio hili la kigaidi la Christchurch. Baada ya kuanguka kwa USSR zamani mnamo 1991, mfumo wa Kikomunisti haukuwa tishio tena kwa mfumo wa kibepari wa kimagharibi. Kwa hivyo, George W. Bush Sr. alitangaza mpango mpya wa ulimwengu ambao uliheshimiwa na wasomi wa kimagharibi kama Fukiyama katika kitabu chake, The End of History and the Last Man. Mhemko wa maadhimisho ya mpango huu hata hivyo uliisha kwa muda mfupi kwani changamoto mpya na tishio kwa Ubepari haikuepukika. Tishio hili ni Uislamu, mfumo ambao ulitekelezwa kwa zaidi ya karne kumi na tatu, uliongoza wanadamu, ukawatoa katika kiza hadi kwenye nuru. Leo Uislamu hauna serikali, lakini hali zote zinaonyesha kurudi kwake. Tishio hili ndio sababu ya tuhuma ya nchi za Kibepari na vyombo vikuu vya habari, vikilenga kutia hofu na chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu.
Brenton Tarrant, ni natija ya propaganda za kimagharibi na chuki zake, ingawa vilevile wanajitenga na tukio hilo kama la mtu binafsi kando na sera mbovu za kigeni dhidi Uislamu na Waislamu. Kwa kweli Tarrant alizua mapambano ya kiitikadi na mzozo wa kisiasa kati ya Uislamu na Ubepari. Hili linaweza kushuhudiwa kutokana na jinsi vyombo vikuu vya habari vilivyowasilisha tukio hili ovu kama tukio la kipekee, Tukio la kibinafsi lisilo ambatana na propaganda nzima ya sera ya kimagharibi dhidi ya Uislamu. Kwa kutumia maneno kama “mshukiwa”, “kupiga risasi”, na waumini kuficha na kupotosha raia kufahamu uhakika na kujua ukweli wa mambo.
Hata huko kubadilisha ombi la kuwa na hatia kumefanyika katika kipindi ambacho ulimwengu unashughulishwa na janga la Covid-19. Kesi hiyo itakuwa na athari ndogo kwa umma. Mabadiliko haya ya ombi la kuwa na hatia ni uamuzi wa kimakusudi, kisha kwa wakati na kwa njia ya pamoja, kinyume kabisa na dhamira ya jamaa huyu mwovu, Brenton Tarrant.
(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا بِطَانَةً مِّن دُونِكُمْ لَا يَأْلُونَكُمْ خَبَالًا وَدُّوا مَا عَنِتُّمْ قَدْ بَدَتِ الْبَغْضَاءُ مِنْ أَفْوَاهِهِمْ وَمَا تُخْفِي صُدُورُهُمْ أَكْبَرُ ۚ قَدْ بَيَّنَّا لَكُمُ الْآيَاتِ إِن كُنتُمْ تَعْقِلُونَ)
“Enyi mlioamini, msiwafanye vipenzi vyenu wengine isipokuwa nyinyi wenyewe, kwa maana hawatawaepusheni na uharibifu wowote. Wanatamani lau mngekuwa katika dhiki. Chuki zao tayari zimeonekana kutoka katika vinywa vyao, na yale yaliofichwa katika vifua vyao ni makubwa zaidi. Hakika tumekuonyesheni ishara zetu, ikiwa mutatumia akili.’’ [Al-i-Imran: 118]
Enyi! Umma wa Muhammad (saw)! Dola kubwa za Kimagharibi hivi leo zinaonyesha waziwazi uadui halisi dhidi ya Deen ya Haqq. Ni wakati muafaka wa kutambua hili kwani ulimwengu unashuhudia anguko la Ubepari na kusimama kwa Uislamu. Ili kuelekeza juhudi zote na kutambua kuinuka huku kusikoweza kuepukika na kurudisha maisha ya Dini hii tukufu ya Uislamu, kwa kusimamisha serikali ua Uislamu. Serikali ambayo inastahili kulipiza kisasi na kudhamini haki kwa maisha ya watu wote wasiokuwa na hatia ambayo yalipotezwa kwa njia mbaya sana.
(وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بنصر الله)
“Na siku hiyo waumini watafurahi kwa ushindi kutoka kwa Allah.’’ [Ar-Rum: 4-5]
Kutoka kwa ofisi kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir.
Ali Omar Albaity,
Mwanachama wa Ofisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kenya