Hizb ut-Tahrir
Hizb ut Tahrir ni chama cha kisiasa ambacho mfumo wake ni Uislamu, kwa hiyo siasa ndiyo kazi yake na Uislamu ndiyo mfumo wake. Kinafanyakazi ndani ya Ummah na pamoja nao, ili uweze kuubeba Uislamu kama kadhia yake na kuuongoza katika kurudisha Khilafah na hukmu za Allah (swt) alizoteremsha. Hizb ut Tahrir ni kundi la kisiasa na sio la kiroho. Wala sio kundi la kiusomi, kielimu au msaada. Fikra ya Kiislamu ndiyo roho ya mwili wake, msingi wake na siri za maisha yake.