TILLERSON: Huna La Kutatua

TILLERSON: Huna La Kutatua Kwani Mfumo Wako Muovu Wa Kibepari Unaangamiza Taifa Lako Na Ulimwengu Kwa Ujumla

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

 Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson yupo katika ziara ya mataifa matano ya Afrika ilioanza  nchini Ethiopia siku ya Jumatano tarehe 7/03/2018.Kwa sasa yuko nchini Kenya na anatarajiwa kuzuru mataifa ya Chad, Nigeria na Djibouti. Ziara hii inatajwa kuangazia zaidi njia za kupambana na ugaidi na kustawisha usalama, biashara na suala zima uekezaji.

Tunapenda kusema yafuatayo:

Ziara ya Tillerson na waliomtangulia kabla yake inakuja ambapo taifa lake ni lenye kushuhudia mporomoko mkubwa wa  kiuchumi uliosababishwa na tamaa yake ya kibepari ya kuvamia mataifa mengine na kumwaga damu za watu.Hali hii imefanya  utawala wa Trump kukiri Marekani inaanguka hivyo ni lazima kuchukuliwe hatua za haraka na kupeana kipau mbele maslahi yake ya kiuchumi ‘America First’) dhidi ya washindani wake. Haya ni kama ilivyokuja ripoti iitwayo National Security Strategy iliochapishwa tarehe mwezi Disemba mwaka jana.

Mazungumzo kuhusu biashara na uekezaji tunayaona kama hatua ya Kiamerika kutaka kujikwamua kwake kiuchumi kupitia kupora rasilimali za mataifa ya Afrika chini ya madai ya kutaka kuiendeleza. Mataifa yenye nguvu hasa Marekani,Ulaya na China hudai kuipa Afrika mikopo na misaada wanayoitumia kama mbinu moja wapo ya kuendeleza ubeberu wao kiuchumi dhidi ya Afrika hali iliopelekea serikali nyingi za Kiafrika kujipata na  limbikizi la madeni makubwa. Kwa sasa Kenya inatumia nusu ya mapato yake kulipia deni ambalo kwa ujumla sasa limefikia trilioni Ksh 5.4! Kwa masikitiko makubwa viongozi wa mataifa wamebakia kuwa mawakala na walinzi wa kulinda maslahi ya mabeberu wa kirasilimali matokeo yake kuifanya Afrika kuonekankwa kuwa bara masikini zaidi duniani!

Kuhusu suala la usalama na  njia za kupambana ugaidi; twasema kuwa Marekani na washirika wake hawana nia ya kupambana na ugaidi kwani wao ndio wadhamini wa kuu wa ugaidi kote duniani. Majeshi ya Kimagharibi  yanaongoza mashambulizi ya angani na ardhini kuwauwa watu wa Alepo na Alghouta ndani ya Syria.. Fauka ya haya, chini ya madai ya ugaidi Amerika imetia majeshi ya serikali nyingi hapa Afrika makwapani mwake na kuweka  kambi zake za kijeshi kama mbinu yake ya kuyatoa mataifa ya Ulaya  hasa Uingereza ndani ya Afrika ili yeye apate nafasi kubwa ya kupora Afrika. Na kwa haya mara nyingi harakati za mauaji hapa Afrika hudhaminiwa na Marekani ambaye huziita harakati za kuleta mageuzi.

Mwisho tunasema Juhudi zote hizi ni jaribio la Amerika kutaka kuziba aibu za mfumo wake na si kweli kuwa Marekani, Ulaya na Uchina yanatakia Afrika mema bali yote yana ajenda ya kuididimiza kwenye dhiki zaidi. Afrika. Hivyo twakariri kuwa Uislamu pekee ndio una uwezo wa kutatua matatizo ya bara kwa kupitia dola ya Khilafah ambayo sera yake ya kigeni haisimami juu ya ukoloni na ubeberu bali imesimama juu kueneza uadilifu kwa wanadamu wote.

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya

 

KUMB: 06 / 1439 AH

Jumapili, 23 Jumada II 1439 AH/

11/03/2018 M

 

Simu: 0707458907

Pepe: mediarep@hizb.or.ke