Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Wakati huu wa ongezeko la visa vya virusi vya Corona, wahudumu wa afya wa humu nchini katika hospitali za umma wapo kwenye mgomo unaowaacha wagonjwa wakiumia. Matakwa yao kwa serikali ni pamoja na usambazaji wa vifaa vya kawaida vya kinga ya kibinafsi (PPE), bima za matibabu , kupewa marupurupu ya mazingira magumu ya kazi, kuajiri wataalamu zaidi wa afya kwa maktaba wa kudumu na kupandishwa vyeo. Mgomo huo umewakosesha mamilioni ya wagonjwa huduma afya katika hospitali za umma!
Hizb ut-tahrir/ Kenya ingependa kubaini yafuatayo:
Hali hii ya kutamausha ni fedheha kwa serikali yoyote ile inayodai kujali maslahi ya raia wake inayowabebesha zigo la ushuru huku ikiwaacha kuumia katika hospitali za umma wakinyimwa haki msingi ya matibabu.
Sekta ya afya, kama sekta yoyote ile ya umma ndani ya tawala za Urasilimali haijasimamiwa vyema bali ni yenye kutelekezwa, ni hii inafichua wazi kuwa lengo kuu la tawala hizi ni kuangalia tu maslahi ya tabaka dogo la viongozi huku ikidharau yale ya raia. La ubaya zaidi, wakati ambapo matakwa ya madaktari yakipuuzwa vifaa vya vya kujilinda na maambukizi na fedha za kushughulikia janga la Covid 19 zimeibwa na viongozi wenye uchu wa kupapia mali.
Chanzo halisi cha masaibu haya ni mfumo wa kibebari na wanasiasa wake sawasawa wawe wako uongozini au wako kwenye safi ya upinzani wote hawajali ustawi wa wafanyikazi, bali hunyima raia wao huduma za afya. Ubepari huzaa viongozi walio na sifa ya ubinafsi wasotilia maanani maslahi ya umma, na wakati mwingi utawaona wakipitisha miswada ya kujiongozea marupurupu kama watakavyo hatakama raia ni wenye kughadhibishwa na hatua yao hio.
Wahudumu wa afya wanaogoma wanapaswa kufahamu misingi miovu ya mfumo wa kirasilimali na kuwa ndio kiini haswa cha masaibu haya. Matatizo yote yaliyoko kwenye huduma za umma yanayosababisha migomo ya mara kwa mara ya wafanyikazi wa umma yanahitaji suluhisho la kimfumo ambalo katu haliwezi kutoka kwa mfumo uliopo wa Kirasilimali.
Mfumo mbadala kwa Urasilimali sio mwengine ila ni Uislamu uliofanya matibabu kuwa ni miongoni mwa mahitaji msingi ya umma yanayohitaji uangalizi mkubwa. Uislamu hauangalii huduma ya afya na huduma nyenginezo za umma kama fadhila au ihsani bali ni jukumu la kipaumbele ambalo serikali inawajibisha kutoa huduma hio kwa raia wake wote. Isitoshe, Uislamu ukaendelea kueleza kwamba mishahara ya madaktari huchukuliwa kwa Baitul-mali (Hazina kuu ya serikali). Sio hilo tu, Uislamu ukaharamisha utozwaji wa ushuru mshahara wa wafanyikazi na hili ni hatua ya kuwawezesha wao kukimu mahitaji yao. Kwa msingi huu, tunasema bayana kwamba kusimamishwa upya tena dola ya Kiislamu leo ulimwenguni chini ya mfumo wa Mtume, sheria hizi tukufu za Kiislamu zitaweza kutekelezwa kikamilifu hivyo kutoshuhudia migomo ya mara kwa mara.
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut-Tahrir in Kenya
REF: 1442/05 AH
Jumanne 30th Rabiul Thaniy 1442 AH
15./12/2020