Kunyanyuka kwa Ufahamu: Uwajibu wa Kisharia Juu ya Ummah na Kubeba Majukumu

Moja miongoni mwa mbinu muafaka ya kupata mamlaka ni kujitolea kihali na mali kusambaza fikra hio miongoni mwa Ummah, hasa kwa wale walojitwika jukumu na dhima hio ya kuhakikisha kuwa watafikia malengo yao. Mfano mzuri ni vile alivyofanya Ar Rasul (saw) na Maswahaba (ra) mwanzoni mwa ulinganizi wa Uislam. Walijitolea muhanga kwa ajili ya Uislam ili kujenga ufahamu. Hawakuchoka wala kuvunjika ari, hadi walipofikia malengo yao: kudhihiri Uislam kwa kupitia kwa Dola ya Kiislam. Hivyo hivyo, hali yabaki ile ile mpaka leo.

Wavamizi mabepari wakimagharibi, wamejenga hisia ya kuvunjika moyo na kukosa ari miongoni mwa Ummah, ili waendeleze fursa ya kuwatawala na kuzipora mali zao. Japo njama hizi mpito huishia ukingoni. Ni jukumu la Kiislam na wajibu wa Kisharia juu ya Ummah kutwaa majukumu.

Qur’an tukufu na Sunnah imebainishi jambo hili dhahiri shahiri. Na mafunzo haya yatadumu milele kama nakshi ilochongwa nyoyoni mwao.

Allah (Swt) Asema:

﴿كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ ۗ وَلَوْ آمَنَ أَهْلُ الْكِتَابِ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُم ۚ مِّنْهُمُ الْمُؤْمِنُونَ وَأَكْثَرُهُمُ الْفَاسِقُونَ

Nyinyi ni Ummah bora uliotolewa kwa ajili ya watu. Mnaamrisha mema na mnakataza maovu na kumuamini Mwenyezi Mungu. Na lau kuwa Watu wa Kitabu nao wameamini ingeli kuwa bora kwao. Wapo miongoni mwao waumini, lakini wengi wao wapotovu. [Aali Imran :110]

Katika Ayah nyingine, Allah (Swt) Asema:

﴿وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا لِّتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ وَيَكُونَ الرَّسُولُ عَلَيْكُمْ شَهِيدًا ۗ وَمَا جَعَلْنَا الْقِبْلَةَ الَّتِي كُنتَ عَلَيْهَا إِلَّا لِنَعْلَمَ مَن يَتَّبِعُ الرَّسُولَ مِمَّن يَنقَلِبُ عَلَىٰ عَقِبَيْهِ ۚ وَإِن كَانَتْ لَكَبِيرَةً إِلَّا عَلَى الَّذِينَ هَدَى اللَّهُ ۗ وَمَا كَانَ اللَّهُ لِيُضِيعَ إِيمَانَكُمْ ۚ إِنَّ اللَّهَ بِالنَّاسِ لَرَءُوفٌ رَّحِيمٌ

Na hivyo hivyo tumewafanya Ummah wa kati(bora) ili muwe mashahidi juu ya watu na Ar Rasul awe shahidi juu yenu. Na hatukukifanya kibla ulicho kuwa nacho ila tupate kumjua yule anaye mfuata Mtume na yule anaye geuka akarejea nyuma. Na kwa yakini hilo lilikuwa jambo gumu isipo kuwa kwa wale alio waongoa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu hakuwa mwenye kuipoteza Imani yenu. Kwani Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa watu na Mwenye kuwarehemu. [Al Baqarah:143]

Kwa hivyo, ni jukumu la kisharia juu ya Ummah na wajibu wa Kiislam kujitolea muhanga kujitwika majukumu. Imepokewa kutoka kwa Abdullah ibn Umar kutoka kwa Ar Rasul saw asema:

عن عبد الله بن عمر رضي الله عنهما عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: »أَلَا كُلُّكُمْ رَاعٍ، وَكُلُّكُمْ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ، فَالْأَمِيرُ الَّذِي عَلَى النَّاسِ رَاعٍ، وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ، وَالرَّجُلُ رَاعٍ عَلَى أَهْلِ بَيْتِهِ، وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْهُمْ، وَالْمَرْأَةُ رَاعِيَةٌ عَلَى بَيْتِ بَعْلِهَا وَوَلَدِهِ، وَهِيَ مَسْئُولَةٌ عَنْهُمْ، وَالْعَبْدُ رَاعٍ عَلَى مَالِ سَيِّدِهِ وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْهُ، أَلَا فَكُلُّكُمْ رَاعٍ، وَكُلُّكُمْ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ« (متفق عليه).

“Kwa hakika nyote ni wachungaji na nyote mutaulizwa kwa kile mulokichunga. Mtawala alioko juu ya watu ni mchungaji na ataulizwa juu yao. Mume ni mchungaji juu ya watu wa nyumbani kwake nae ataulizwa juu yao. Mke ni mchungaji juu ya nyumba ya mumewe na watoto wake naye ataulizwa juu yao. Na mfanya kazi ni mchungaji juu ya mali ya bwana wake nae ataulizwa juu ya mali hio. Jueni nyote ni wachungaji na nyote mutaulizwa na mulichokichunga.” (Bukhari/Muslim)

Katika hadith nyingine, Ar Rasul (saw) asema katika hadith ilopokelewa na Hudhaifah:

عَنْ حُذيفةَ ، عن النَّبيِّ ﷺ قَالَ: »والَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ، لَتَأْمُرُنَّ بالْمَعْرُوفِ، ولَتَنْهَوُنَّ عَنِ المُنْكَرِ، أَوْ لَيُوشِكَنَّ اللَّه أَنْ يَبْعَثَ عَلَيْكُمْ عِقَابًا مِنْهُ، ثُمَّ تَدْعُونَهُ فَلا يُسْتَجابُ لَكُمْ« (رواه الترمذي وَقالَ: حديثٌ حسنٌ.)

“Naapa kwa Yule Mwenye kuitamalaki nafsi yangu!Mutaamrishana mema na kukatazana maovu au nachelea hivi karibuni Allah Atawaletea adhabu kisha mutamuomba Asiwajibu” (At-Tirmidhi, Hadith Hasan)

Kuhukumu kwa Ahkam Za Allah (Swt) Khilafah ni haki ya Kisharia juu ya Ummah. Kwa hivyo ni wajibu wa Kiislam juu yao kujitolea muhanga kwa jino na ukucha, usiku na mchana ili kurudisha mamlaka yao ya kihalali. Udhaifu wa fedheha uloukumba Ummah ni matokeo ya kutabikishiwa nidhamu isokuwa ya Kiislam na wakoloni na vibaraka wao. Haya yalifafanuliwa kinaga ubwaga na Umar bi Al Khataab pale aliposema:

“Sisi tulikuwa watu duni, Allah Akatupa utukufu kwa Uislam na pindi tukitafuta utukufu kando na Uislam, Allah Atatudhalilisha.

#أقيموا_الخلافة

#ReturnTheKhilafah

#YenidenHilafet

#خلافت_کو_قائم_کرو

#TurudisheniKhilafah

Written for the Central Media Office of Hizb ut Tahrir by

Hussein Mohammed

Member of the Media Office of Hizb ut Tahrir in Kenya