HAUNA SATUWA

Hunu urasilimali, hauna kattu satuwa,

Ni mfumo ulofeli, ungatumia vifuwa,

Yaliyopo mashakili, ushindwile kutatuwa,

Sasa uwile mabuwa, hunu urasilimali,

 

Hautoki kwa Jalali, ni watu wameuzuwa,

Kwa kutumia akili, pamwe na matamaniwa,

Haramu kwao halali, ilokanywa na Moliwa,

Ni sumu siyo haluwa, hunu urasilimali,

 

Viongoziwe machali, hawana dira ya sawa,

Ni walafi, matapeli,  na umimi wamejawa,

Kupora za umma mali, ni silika yao huwa,

Kattu si waaminiwa, hawa warasilimali,

 

Imekuwa ni muhali, raiya kusimamiwa,

Wawile ni mahamali, wa mazito kutukuwa,

Wamefanywa madhalili, kura zao zawauwa,

Waja si wahudumiwa, kwenye urasilimali,

 

Machafu yana kibali, yani yanadhaminiwa,

Kuoana marijali, ni tendo lilolaniwa,

Demokrasiani bali, hilino laruhusiwa,

Mawi yote hunadiwa, kwenye urasilimali,

 

Umezorotesha hali, waminya na kukamuwa,

Seraze za kikatili, kwa watu zapangiliwa,

Zahilikisha nasili, na mimea ya kuliwa,

Ni miba siyo maua, hunu urasilimali,

 

Maisha siyo sahali, watu wanakamuliwa,

Gharama yake I ali, itowekele afuwa,

Urasilimali kweli, kabisa umeishiwa,

Kabisa umeishiwa, hunu urasilimali,

 

Mfumo ulokamili, ni uisilamu juwa,

Watoka kwa Mutaali, na wala hauna dowa,

Ujile na maadili, yalomema na  usawa,

Uisilamu ni dawa , ya hu urasilimali,

 

Khilafah ni sirikali, ambayo niyakishuwa,

Aloitaja Rasuli, watu inayokombowa,

T’ini ya chakwe kivuli, Mola atawahidiwa,

Khilafah itakoboa, wote urasilimali,

 

Kwa ya Mtumi sabili, ja ya mwanzo ilokuwa,

Khilafah itawasili, pasi shaka kutiliwa,

Hiyo ni yakwe kauli, Rasuli mswadikiwa,

Khalifah kubaiiwa, ni faradhi jambo hili,

 

Hapano natuwa tuli, ukingoni nimetuwa,

Hayano naliyokuli, yapawe mazingatiwa,

Kwa waisilamu hili, hili kwao latakiwa

Khilafah kuifufuwa, ziwaepukie dhili,

 

 

MTUNZI – MOHAMMED BAKARI

 

ALMUFTI

 

MOMBASA — KISAUNI