Mashambulizi ya Mabomu Somalia: Umma unaendelea kuwa kafara kwa Majeshi ya Kigeni

Habari na Maoni

Habari:

Takriban watu 100 wameuwawa na wengine mia 300 kujeruhiwa kwenye shambulizi la mabomu yaliyotegwa kwenye magari mawili mji mkuu wa Somalia Mogadishu, Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mahmoud alisema. Akililaumu kundi la wapiganaji la Al-Shabab kwa mashambulizi hayo, Mahmoud aliwaambia wanahabari siku ya Jumapili kwamba anatarajia idadi ya vifo kuongezeka kwenye milipuko hiyo miwili. Wakuu serikalini walisema kwamba shambulizi la siku ya Jumamosi lililofanywa katika soko la Sobe lenye shughuli nyingi lililenga jengo la wizara ya elimu ya Somalia na shule.

Maoni:

Shambulizi hili limeonesha wazi kudorora kwa hali ya usalama nchini Somalia dalili tosha ya kufeli kwa vyombo vya usalama vya serikali ya  Somalia katika kulinda usalama wa raia wake. Mara kwa mara mashambulizi haya yanapofanywa popote duniani kinachofuata ni kashfa kutoka kwa wakuu wa kiserikali na watawala wa kimagharibi kama ilivyokua hali ya Somalia. Kwa upande mwengine la kuhuzunisha zaidi, ni kusikika kwa makundi yenye silaha kukiri kwao utekelezwaji wa mashambulizi haya ya mabomu. Hivi kuna uhalali wowote wa kutekeleza mauaji kama haya? Kiukweli hakuna uhalalisho wowote ule kwa serikali yoyote ile au kundi lolote kuuwa raia waso na hatia mahala popote pale kwani kitendo hiki kimekatazwa na Uislamu MwenyeziMungu SWT anasema:

وَلَا تَقْتُلُوا النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّهُ إِلَّا بِالْحَقِّ ۗ

Wala msiuwe nafsi ambayo MwenyeziMungu Amekataza ispokuwa kwa haki

[Isra’i:34]

Mauaji haya sio mara ya kwanza na wala hayotukuwa ya mwisho madamu kuna majeshi ya mataifa ya kigeni ndani ya Somalia. Marekani ilituma tena idadi ndogo ya wanajeshi wake mwezi Mei 2022 ambapo mashambulizi yake ya angani imekuwa ikiyatekeleza kwa kipindi kirefu. Tokea Januari mwaka 2007, Taifa hili likaanzisha mashambulizi ya kutoka angani takriban 234 nchini Somalia yaliodaiwa yakilenga Alqaeda na kundi la Islamic State hii ni Kulingana na dara za shirika la FDD Long War Journal. Kwa miaka 15 Serikali ya Marekani imekua ikikana kwamba kwenye mashambulizi hayo hayakuwa yakilenga na kujeruhi raia na ati kwa kipindi chote hiki ni watu watano pekee ndio waliuwawa! Hii ni lugha ya kivita ambayo haikisi uhalisia wa mambo nao ni kwamba raia wengi wameuwawa nchini Somalia kutoka na mashambulizi ya angani ya Marekani.

Serikali  za kimagharibi zinazojifanya kulia machozi ya mamba vifo ya watu nchini Somalia huku damu za mamilioni ya wanawake, watoto na wazee  kote duniani zinatiririka mikononi mwao. Marekani kwa upande wake hasa ndio inayoongoza na kuruhusu vibara wake katika biladi za Kiislamu kutumia silaha za kemikali dhidi ya umma kama hali ya Bashar-Al-Asad wa Syria.

Mapigano nchini Somalia yamekua yakizidi kila uchao na umma unabakia muathiriwa wa majeshi ya kigeni. Ongezeko la wanajeshi wa Marekani linaigeuza Somalia kutoka eneo la dharura na janga la kibinadamu kuwa “eneo la uhasama mkali” na watu hawatasalimika na milipuko ya mabomu inayowaacha wazee, wanawake na watoto kuwa wahanga wa mashambulizi haya.

Kama hali ya  biladi yoyote ile ya Kiislamu, Somalia itaendelea kukumbwa  na umwagaji wa  damu miongoni mwa migogoro mingine inayosababishwa na utiifu wa  viongozi wa Kiislamu kwa mabwana zao wa nchi za magharibi. Migogoro mingi katika biladi hizi  inatokana moja kwa moja na ushawishi wa kigeni na uingiliaji kati masuala yake. Kwa vile ulimwengu wa Kiislamu unaongozwa na watawala wanaoungwa mkono na nchi za magharibi, ummah uko katika msukosuko. Na kwa vile hakuna Khilafah – serikali huru ya Kiislamu  basi migogoro ndani ya Somalia itakuwa ni yenye kuendelea. Ni Khilafah inayotekeleza sheria za MwenyeziMungu na hapo ndio mambo ya umma yatatatuliwa mara moja na kwa wote

Imeandikwa kwa Niaba ya Ofisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Shabani Mwalimu

Mwakilishi Kwa Vyombo Vya Habari Hizb ut Tahrir Kenya.