Hizb ut Tahrir/ Kenya Yafanya maandamano baridi kutoa mwito wa Hatua ya Kijeshi dhidi Umbo la Kiyahudi
Taarifa kwa Vyombo Vya Habari
Kufuatia mauaji ya halaiki yanayoendelea kufanywa na umbo la Kiyahudi dhidi ya watu wa Gaza, Hizb ut Tahrir/Kenya siku ya Ijumaa tarehe 18 Aprili, ilifanya maandamano baridi baada ya Swala ya Jumaa katika miji ya Mombasa na Nairobi. Katika Jiji la Pwani, maandamano haya yalifanyika nje ya Masjid Nur, huku Nairobi yakafanyika katika Masjid Hidaya mtaani Eastleagh. Malengo makuu kwenye maandamano hayo ilikua ni kutoa mwito kwa Majeshi katika nchi za Kiislamu kuvunja minyororo ambayo watawala wao wamewaweka katika ngome zao ili mara moja waende kuukomboa watu wa Gaza na Al-Aqsa kutoka katika makucha ya Mayahudi walioukalia kwa mabavu.
Maandamano hayo baridi yalimalizika kwa kufanya mkutano mfupi na waandishi wa habari juu ya mashambulizi yanayoendelea dhidi ya watu wa Gaza na Filastin ardhi iliobarikiwa. Katika majumuisho hayo, Shabani Mwalimu (Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari Hizb ut Tahrir Kenya), Ustadh Mahad Ali -Mwenyekiti wa CCC pamoja na Ali omar Mjumbe wa Ofisi ya Vyombo vya Habari walikariri kuwa serikali pekee inayoweza kuhamasisha jeshi la Waislamu dhidi ya jeshi la Jumuiya ya Kiyahudi ni Dola ya Khilafah (Ukhalifa) kwa njia ya Utume; ina uwezo wa kukomesha kiburi na ubakatili wa Wayahudi
Kwa ujumla Ummah ulikumbushwa juu ya kazi yao tukufu ya kurudisha mfumo wa maisha wa Kiislamu kwa kusimamisha tena dola ya Khilafah kwa njia ya Utume ambayo itayakusanya majeshi ya Kiislamu dhidi ya umbo la Wayahudi linaloungwa mkono na Magharibi.
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari Hizb ut Tahrir
Kenya