Mtume Muhammad ﷺ aliunda jamii moja ya Kiislam iliokuwa na mshikamano madhubuti sawa iwe ni upande wa kifikra au kihisia.Mshikamano huu ulijumuisha Ummah wote mzima:kuanzia mtawala:Khalifah hadi raia.ALlahﷻ Asema:
Hakika huu umma wenu ni umma mmoja,na Mimi ni Mola wenu,basi niabuduni.
TMQ 21:92
Ktk Ayah nyingine, ALlah ﷻ,Asisitiza kuhifadhi mshikamano huu kwa kusema:
Na mtiini ALlah na Ar Rasul wake, wala msigombane, msije mkavunjika nguvu na mamlaka yenu yakaondoka;na vumilieni.Hakika ALlah Yu pamoja na wanaovumilia.
TMQ 08:46
Na Mtume SAAW Rasul ﷺ akaupigia mifano mtungamani huo kwa mifano miwili mikuu
1)Mfano wa kwanza.
Mtume SAAW aliufananisha na jengo moja imara.Ambalo limesimama kwa kushikamana ala zote za ujenzi zilotumika kulisimamisha:
2)Mfano wa pili
Mtume SAAW alioutoa ni wa mwili mmoja wa mtu.
Ambapo maumivu yanapogusa kiungo kimoja,basi yana athari ktk mwili wote jumla,bila kujali maumivu yametoka ktk ukucha,jino,kidol au wayo!
Imepokewa kutoka kwa An-Nu’man bin Bashir akisema: Amesema Ar Rasul ﷺ:
“Mfano wa Waumini katika kupendana kwao,kuhurumiana kwao na kusikitikiana kwao,ni kama mfano wa mwili mmoja: kinapoumwa kiungo kimoja, viungo vyote vinashiriki kwa kukesha na homa.”
(Bukhari na Muslim)
HALI YA WAISLAM KWA SASA!
Tofauti kabisa na ulivyoasisi na kukusudiwa kuendelea kuwa hivyo,Waislam leo wamegawanyika ktk kila sehemu.Licha ya kuwa,wote wakiri kuwa hawafai kuwa na MWANYA au PENGO la kisiasa baina yao.Lenye kuzuia umoja wao.Na wote kwa jumla,wakubali kuwa maadui zao,hasa wakoloni wa kimagharibi,ndio wabunifu wa mwanya huo,ulovunja umoja wao!Kupitia kwa njama walizopika kuvunja Khilafah Uthmaniya,na kuzigawanya biladi za Kiislam,kwa mipaka bandia ilochorwa na wakoloni makafiri Sykes-Picot 1916.Si wakoloni tu ambao,waupanua mwanya huo.Bali hatari kubwa,washirikiana na wanasiasa vibaraka wenye kutawala kimabavu bila za Kiislam, ndio chanzo na muendelezo wa hali hii mbaya yenye kuwazonga!
JEE OMBWE AU PENGO LA KISIASA(POLITICAL VACUUN)NI UPI?!
Ombwe la kisiasa linamaanisha hali ambapo hakuna uongozi wa wazi au madhubuti wa serikali au mfumo wa kisiasa.Kutokuwepo kwa uongozi wa kati ulio thabiti na mamlaka ya pamoja isiyotetereka kunaleta ombwe la kiuongozi!
MATOKEO YA MWANYA WA KISIASA!
Mwanya huo mara nyingi husababisha hali ya kutoeleweka na ghasia.Kwa mfano:kutokuwepo kwa utulivu kama ilivyo Somalia,mashaka na hali ya uhasama kama Libya,kusambaratika kwa taifa kama Iraq,pamoja na migogoro na mivutano miongoni mwa wanachama wa familia za kifalme katika nchi za Kiislamu.Kukuzwa fikra chafu za ukabila na uzalendo naona ya Waislam.Ambazo ndio kipande cha kizuizi chenye sumu,kilopachikwa na makafiri baina ya Waislam.Na kuwafanya,licha kuwa na uwezo wote wa kiroho na kimadi,kushindwa kuzihami rasilimali zao,na kuhami ndugu zao wanapovamiwa kama hali ilivyo Falastin.Kila nchi ikitanguliza kulinda maslah ya mkoloni anaeiendesha kwa kupitia vibaraka.
Uvamizi wa njee kutoka kwa dola ghasibu za kikoloni hukithiri.Kwa kuwa,huwa zimepata fursa ya uvamizi bila pingamizi yoyote.Na kuleta fikra na thaqafa pinzani.Huku wakoloni wakikimbilia kujaza mwanya huo au kuathiri matokeo ya kujaza pengo hilo.Kila mmoja aking’ang’ania kumpachika kibaraka muafaka kwa maslah yake.
Halikadhalika,mwanya huo hutoa fursa mwanana kwa wakoloni,kupora rasilimali na malighafi kama tunavyoshuhudia ktk bila za Kiislam.Kama tunavyoshuhudia hali ilivyo ulimwenguni,na hasa ktk biladi za Kiislam na Africa.Ambapo rasilimali zimekuwa kama mali ya kutunukiwa kwa wakoloni.Hali hizi zote hupelekea kurudi nyuma kwa maendeleo katika nyanja zote za maisha.
Hali hii imewazonga Waislam,baada ya kuvunjwa kwa Dola yao mnamo machi 3 1924,nchini Uturuko.Kwa chuki na uadui ulofanywa na Ufaransa,kupitia kibaraka wao,Mustafa Kamal Ataturk.Ushirikiano uloshuhudia kuuwacha Ummah yatima bila mama:Dola yao iliokuwa ni ngao yenye kuwalinda,dhidi ya uvamizi sawa uwe wa kimadi,kifikra.Kando na kutoa mchango mkubwa,kwenye ufanisi wa maendeleo yaloshuhudiwa chini ya usimamizi wake.
Tofauti na hali ya kudumaa kithaqafa,kifikra,kihisia ambayo Waislam wapitia kwa sasa,baada ya kupigwa mafungu ya vijinchi 50.Kila nchi ikiwa na agenda zake,nidhamu ya utawala tofauti na miungano dhalili chini ya wakoloni.Zote zikifanya bidii kubwa kurudisha wakoloni,hata kuliko kumridhisha ALlah ﷻ na Ar Rasulﷺ kwa kufuata maagizo yao!
MUSTAKBAL WA UMMAH WA KIISLAM!
Ukombozi wa Waislam,hautegemei misaada na ya wakoloni.Wala maagizo dhalili ya vibaraka wenye kutawala biladi za Kiislam.Bali ukombozi halisi,utakaozaa fanisi na maendeleo,uko kwenye kuwang’oa vibaraka hawa.
Na mahali Pao kumueka Khalifah atakae kuziunganisha biladi zote chini chini ya bendera ya Tawheed ya kweli wala sio nembo tu.Kwa kuondoa mwanya wa kisiasa ulojengwa juu ya mipaka bandia na hisia duni za uzalendo na ukabila.
Hili litadhaminia kurudisha umoja wao kama ulivyoasisiwa na Ar Rasulﷺ.Ndio wema walotangulia wakawa na haya ya kutunasihi.Umar ibn Khatwab ra asema:
Hakika tulikuwa watu wanyonge kabisa, ALlah ﷻ Akatupa utukufu kwa Uislamu.Basi tutakapotafuta heshima kwa njia nyingine,ALlah ﷻ Atatudhalilisha.
Na Imaam daarul Hijra:Al Imaam Malik ibn Anas ra akamaliza kwa kutupa jibu la ufanisi wetu:
Hautotengea mwisho wa Ummah huu, isipokuwa kwa kile kilichoutengeneza mwanzo wake.
Hussein Muhammad
Mwanachama wa Hizb-ut-Tahrir Kenya
10 Safar 1447
8 August 2025