Tabbanni katika Hizb ut Tahrir

Baada ya kusoma, kutafakari na kuchunguza kuhusu hali ya sasa ya Umma huu na kiwango ulichofikia, na hali katika zama za Mtume (saw), na katika zama za Makhalifah wanne walioongoka na katika zama za waliofuata baada yao, na kupitia kuregelea seerah na njia ambayo yeye (saw) alibeba da’wah kutoka wakati alipoanza mpaka alipo simamisha dola Madina. Baada ya kusoma namna ya utendakazi wake (saw) ulivyo kuwa mjini Madina na kupitia kuregelea kitabu cha Allah (swt) na Sunnah za Mtume wake (saw) na yale yaliyo ashiriwa na jumuiko la Maswahaba (Ijma’ as-Sahaba) na njia ya uvuaji hukmu za kisheria (Qiyas), na rai angavu za Maswahaba na waliofuata baada yao, na rai za mujtahidina, baada ya yote haya. Hizb ut Tahrir hatimaye ikatabanni fikra, rai na hukmu zinazo husiana na fikra na njia yake. Si chengine isipokuwa ni fikra, rai na hukmu za Kiislamu, hakuna yoyote iliyo ya kikafiri, wala inayo athiriwa na ukafiri; bali zote ni za Kiislamu na wala hazitegemei chochote isipokuwa machimbuko ya Uislamu. Chama hiki kimejifunga na njia ya tafakari katika kutamatisha fikra, rai na hukmu hizi.

Hizb imetabanni fikra, hukmu na rai ambazo ni muhimu kwake katika kuendelea na kazi ya kuregesha maisha kamili ya Kiislamu na kubeba da’wah ya Kiislamu kwa ulimwengu mzima kupitia kusimamisha dola ya Khilafah na kuteua Khalifah.

Chama hiki kimekusanya yote kilicho tabanni na yote kilicho toa katika fikra, hukmu na rai ndani ya vitabu vyake na ndani ya matoleo yake mengi kilicho chapisha na kutoa kwa watu. Hivi ni vitabu ambavyo chama kimetoa:

Nidhamu ya Uislamu
Nidhamu ya Utawala Katika Uislamu
Nidhamu ya Kiuchumi Katika Uislamu
Nidhamu ya Kijamii Katika Uislamu
Muundo wa Chama
Fahamu za Hizb ut Tahrir
Dola ya Kiislamu
Shakhsiyya ya Kiislamu (katika mijeledi mitatu)
Fahamu za Kisiasa za Hizb ut Tahrir
Rai za Kisiasa za Hizb ut Tahrir
Utangulizi wa Katiba
Al-Khilafah
Vipi Khilafah Ilivyo Angamizwa
Nidhamu ya Kuadhibu
Hukmu za Dalili
Ukanushi wa Ukomunisti wa Kimarxi
Tafkiri
Uwepo wa Akili
Fikra ya Kiislamu
Ukanushi wa Nadharia ya Dhima Katika Sheria ya Kimagharibi
Mwito wa Harara
Sera Halisi ya Kiuchumi
Hazina Katika Dola ya Khilafah

Chama pia kimetoa maelfu ya matoleo, ukumbusho na vijitabu vya kifikra na kisiasa.

Chama hiki kinapo beba fahamu na hukmu hizi kwa watu, kinazibeba kisiasa. Yaani, kinazibeba fahamu hizi kwao ili watu wazitabanni, kuzitekeleza na kuzibeba katika kuziasisi ndani ya serikali na katika mambo ya kimaisha. Hii ni kwa sababu hili ni jukumu juu ya Waislamu, kama lilivyo jukumu juu ya chama hiki kama chama cha Kiislamu, na wanachama wake kama Waislamu.

Chama hiki kinategemea katika kutabanni kwake fikra na hukmu za Kiislamu Qur’an, Sunnah, Ijma’ as-Sahabah na Qiyas pekee, kwa sababu machimbuko haya manne ndio machimbuko pekee ambayo kuthibiti kwake ni kupitia dalili zilizo katikiwa.