Afisi Kuu ya Habari: Kampeni ya Kitengo cha Wanawake katika Kumbukumbu ya Karne Moja ya Kuvunjwa Khilafah
بسم الله الرحمن الرحيم
Mwezi wa Rajab mwaka huu ni kumbukumbu ya tukio la kusikitisha katika historia ya Ummah wa Kiislamu, miaka 100 ya Hijria tangu kuanguka kwa dola yake tukufu na uongozi wake wa Kiislamu: Khilafah mikononi mwa adui wa Uislamu Mustafa Kemal na serikali za kikoloni za Magharibi. Tukio hili baya lilikuwa na athari mbaya kwa maisha ya wanawake wa Kiislamu, watoto wao na familia zao, kwani walipoteza dola ambao daima ilikuwa mchungaji na mlinzi wa haki zao na mdhamini wa furaha na ustawi wao. Katika kipindi cha miaka 100 iliyopita, kukosekana kwa Khilafah, maisha ya wanawake wa Kiislamu yamekuwa na alama ya kifo, uharibifu, aibu, huzuni na kukata tamaa.
Katika muktadha wa kampeni ya kiulimwengu iliyozinduliwa na Hizb ut-Tahrir chini ya uongozi wa amiri wa Hizb, mwanachuoni mkubwa Ata bin Khalil Abu Al-Rashtah, Mwenyezi Mungu amhifadhi, kwa anwani “Juu ya karne moja ya kuvunjwa kwa Khilafah. .. isimamisheni enyi Waislamu!”, Kitengo cha wanawake katika afisi kuu ya habari ya Hizb ut Tahrir katika Rajab hii chazindua kampeni yake ya kiulimwengu kwa anwani [Miaka 100 ya dhulma, udhalilishaji na kukata tamaa ambayo wanawake wa Kiisilamu wameishi bila ya mlinzi wao na mchungaji wao “Khilafah”] ili kutoa mwanga juu ya athari chungu na za uharibifu wa kuvunjwa kwa Khilafah juu ya maisha ya wanawake wa Kiislamu ulimwenguni, na vile vile kuwasilisha ruwaza ile ambayo haki, majukumu na hadhi halisi ya wanawake yatakuwa chini ya kivuli cha utawala wa Kiislamu pamoja na da’wah ya kusimamisha kwa dharura dola ya Uislamu (Khilafah Rashida). Pia, katika kampeni hii, tutazivunja fahamu nyingi potofu na za kirongo juu ya ukandamizaji wa wanawake chini ya kivuli cha Khilafah. Katika kampeni hii, kwa sifa yetu kama wanawake wa Hizb ut-Tahrir, tunasema: Imetutosha miaka 100 ya mateso yasiyovumilika, udhalilifu na hasara! Tunahitaji kumaliza sura hii nyeusi kabisa katika historia ya Umma wa Kiislamu!
Dkt. Nazreen Nawaz
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Jumamosi, 01 Rajab 1442 H sawia na 13 Februari 2021 M
– Ili Kufuatilia Kampeni Hii kwa Lugha Nyenginezo –
Kalima ya Dkt. Nazreen Nawaz
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Kwa mnasaba wa Kumbukumbu ya Karne Moja ya Kuvunjwa kwa Dola ya Khilafah
Jumamosi, 01 Rajab 1442 H sawia na 13 Februari 2021 M
– Alama Ishara za Kampeni –
#أقيموا_الخلافة
#ReturnTheKhilafah
#YenidenHilafet
#خلافت_کو_قائم_کرو
#TurudisheniKhilafah
Ili Kusoma Taarifa ya Kitengo cha Wanawake
Ambayo ilitangaza ndani yake uzinduzi wa kampeni yake katika kumbukumbu ya karne moja ya kuvunjwa kwa Dola ya Khilafah na athari yake kwa mwanamke na familia ya Kiislamu
Jumamosi, 01 Rajab 1442 H sawia na 13 Februari 2021 M
Bonyeza Hapa
Mkusanyiko wa Picha