Njia ya Mtume (saw) Kuleta Mageuzi

بسم الله الرحمن الرحيم

Halaqah 11: Mivutano ya Kifikra Katika Da’wah ya Mtume (saw)

Katika halaqah hii tunaendelea na hatua ya tatu katika njia ya Mtume (saw) kuleta mageuzi. Leo tutazungumzia kuhusu mivutano ya kifikra ndani ya da’wah ya Mtume (saw)

Mvutano wa kifikra katika Aqeeda

Ili iwe hukmu ni ya Allah pekee, na kupwekeshwa katika ibada, Alikuwa Rasul (saw) akipambana na imani za kikafiri na za kishirikina za waliokuwa wakiabudu masanamu. Akawa anawasomea kauli ya Allah (swt):

وَلَقَدْ ءَاتَيْنَا إِبْرَٰهِيمَ رُشْدَهُۥ مِن قَبْلُ وَكُنَّا بِهِۦ عَٰلِمِينَ

Na hakika tulikwisha mpa Ibrahim uwongofu wake zamani na tulikuwa tunamjua.

إِذْ قَالَ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِۦ مَا هَٰذِهِ ٱلتَّمَاثِيلُ ٱلَّتِىٓ أَنتُمْ لَهَا عَٰكِفُونَ

Alipomwambia baba yake na watu wake: Ni nini haya masanamu mnayo yashughulikia kuyaabudu?

قَالُوا وَجَدْنَا ءَابَاءَنَا لَهَا عَٰبِدِينَ

Wakasema: tumewakuta baba zetu wakiyaabudu.

قَالَ لَقَدْ كُنتُمْ أَنتُمْ وَءَابَاؤُكُمْ فِى ضَلَٰلٍ مُّبِينٍ

Akasema: Bila ya shaka nyinyi na baba zenu mmekuwa katika upotofu ulio dhaahiri.

[Al-Anbiya: 51-54]

Na (saw) akawasomea:

قالَ أَفَتَعبُدونَ مِن دونِ اللَّهِ ما لا يَنفَعُكُم شَيئًا وَلا يَضُرُّكُم

Akasema: Basi nyinyi mnawaabudu asiye kuwa Mwenyezi Mungu wasio kufaini kitu wala kukudhuruni?

[Al-Anbiya: 66]

Na (saw) akawasomea:

إِنَّكُم وَما تَعبُدونَ مِن دونِ اللَّهِ حَصَبُ جَهَنَّمَ أَنتُم لَها وارِدونَ

Hakika nyinyi na hao mnao waabudu badala ya Mwenyezi Mungu ni kuni za Jahannamu; huko mtaingia tu.

[Al-Anbiya: 98]

Mvutano wa Kifikra Katika Mila na Mazoea

Ili kubainisha uadilifu wa nidhamu ya Kiislam, alikuwa Rasul (saw) alipambana na fikra za watu wajinga zinazofungamana na mila na mazoea ambazo zilikuwa zimetanda wakati huo, ikawa ni kwa njia ya kuzihujumu mila. Mfano ni kuzika watoto wa kike wakiwa hai; akawa (saw) anawasomea kauli ya Allah Ta’ala:

وَإِذَا المَوءودَةُ سُئِلَت

Na msichana aliye zikwa hai atapo ulizwa,

بِأَيِّ ذَنبٍ قُتِلَت

Kwa kosa gani aliuliwa?

[At-Takwir: 8-9]

Na (saw) akawasomea:

وَإِذا بُشِّرَ أَحَدُهُم بِالأُنثىٰ ظَلَّ وَجهُهُ مُسوَدًّا وَهُوَ كَظيمٌ* يَتَوارىٰ مِنَ القَومِ مِن سوءِ ما بُشِّرَ بِهِ ۚ أَيُمسِكُهُ عَلىٰ هونٍ أَم يَدُسُّهُ فِي التُّرابِ ۗ أَلا ساءَ ما يَحكُمونَ

Na mmoja wao akibashiriwa kwa msichana, uso wake unasawijika, naye kajaa chuki. Anajificha asionekane na watu kwa ubaya wa aliyo bashiriwa! Je, akae naye juu ya fedheha hiyo au amfukie udongoni? Tazama uovu wa wanavyo hukumu!

[An-Nahl: 58-59]

Mvutano wa Kifikra Katika Maisha

Ili kubainisha ukubwa wa nidhamu ya kiuchumi ya kiislamu, alikuwa Rasul (saw) alipambana na nidhamu ya kiuchumi ya kijahilia iliokuwa ikiendelea zama hizo. Akawa anahujumu muamala wa riba, Na kazi ya kupunja vipimo; Na alikuwa (saw) akiwasomea:

وَما آتَيتُم مِن رِبًا لِيَربُوَ في أَموالِ النّاسِ فَلا يَربو عِندَ اللَّهِ ۖ وَما آتَيتُم مِن زَكاةٍ تُريدونَ وَجهَ اللَّهِ فَأُولٰئِكَ هُمُ المُضعِفونَ

Na mnacho kitoa kwa riba ili kiongezeke katika mali ya watu, basi hakiongezeki mbele ya Mwenyezi Mungu. Lakini mnacho kitoa kwa Zaka kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu, basi hao ndio watao zidishiwa.

[Ar-Rum: 39]

وَيلٌ لِلمُطَفِّفينَ

Ole wao hao wapunjao!

الَّذينَ إِذَا اكتالوا عَلَى النّاسِ يَستَوفونَ

Ambao wanapo jipimia kwa watu hudai watimiziwe.

وَإِذا كالوهُم أَو وَزَنوهُم يُخسِرونَ

Na wao wanapowapimia watu kwa kipimo au mizani hupunguza.

أَلا يَظُنُّ أُولٰئِكَ أَنَّهُم مَبعوثونَ

Kwani hawadhani hao kwamba watafufuliwa

لِيَومٍ عَظيمٍ

Katika Siku iliyo kuu,

يَومَ يَقومُ النّاسُ لِرَبِّ العالَمينَ

Siku watapo msimamia watu Mola Mlezi wa walimwengu wote?

[Al-Mutaffifin: 1-6]

Akawa Rasul (saw) anawasomea:

كَلّا ۖ بَل لا تُكرِمونَ اليَتيمَ

Sivyo hivyo! Bali nyinyi hamuwakirimu mayatima,

وَلا تَحاضّونَ عَلىٰ طَعامِ المِسكينِ

Wala hamhimizani kulisha masikini;

وَتَأكُلونَ التُّراثَ أَكلًا لَمًّا

Na mnakula urithi kwa ulaji wa pupa,

وَتُحِبّونَ المالَ حُبًّا جَمًّا

Na mnapenda mali pendo la kupita kiasi.

[Al-Fajr: 17-20]

Itaendelea katika UQAB Toleo 16…In Shaa Allah.