Njia ya Mtume (saw) Kuleta Mageuzi

بسم الله الرحمن الرحيم

Halqa 13: Mivutano ya Kifikra na Mapambano ya Kisiasa Walioyafanya Maswahaba (ra)

Katika Halaqa hii tutaangalia mvutano wa kifikra na mapambano ya kisiasa walioyafanya maswahaba (ra).

Msimamo wa maswahaba (ra) ulikuwa imara pasi na kuyumba katika kupambana na kila yanayokhalifu Uislamu na kuyakabili ili kubainisha uongo wake. Hawakujali yatakayotokea wala hali itakavyokuwa katika kushikamana kwao na mfumo (Uislamu) pekee, pasi na kuingiza mahisabu yoyote ila mfumo (Uislamu). Wakimtegemea Allah juu ya hilo, Wakiamini nusra kutoka kwake, wakimuamini kwa imani ya hali ya juu…!

Na ili kuyabainisha hayo tutataja mwenendo mmoja na kugusia msimamo katika misimamo ya kimfumo waliosimama kwayo maswahaba (ra) wakiwa wamezama katika mvutano wa kifikra na mapambano ya kisiasa…!

Huu msimamo ni kwa njia ya mfano tu wala sio kutaja misimamo yote ya maswahaba (ra), kwani misimamo yao ya kimfumo ni mingi Haiwezi kuhifadhika, wala hayatoshei Maqam haya kuyataja, kuitaja inahitaji msururu wa vitabu/mijeledi…!

Msimamo wa swahaba Uthman Ibnu Madh’un (ra) katika kuvumilia shida na maudhi katika Njia ya Allah:

Amepokea Abu Nuaym katika hulya kutoka kwa Uthman asema: Alipoona Uthman Ibnu Madh’un (ra) yanayowapata maswahaba (ra) wa Mtume (saw) kutokana na mitihani naye anatembea kwa amani ya Walid bin Mughera, alisema: “Wallahi hakika kutembea kwangu kwa amani katika hifadhi ya mtu mshirikina, na wenzangu watu wa dini yangu wanapata mitihani na maudhia katika njia ya Allah nami hayanipati, ni upungufu mkubwa katika nafsi yangu! Akamwendea Walid bin Mughera akamwambia: “Ewe Aba Abdi Shams! Umetekeleza dhima yako, nimekurudishia hifadhi yako!” Akasema: “Kwa nini ewe mtoto wa ndugu yangu?! Huenda kuna mtu amekuudhi katika jamaa zangu?” Akasema: “La, lakini mie naridhia hifadhi ya Allah azza wa jalla, wala sitaki hifadhi ya mwengine asokuwa yeye…! Akasema: “Twende msikitini, unirudishie hifadhi yangu waziwazi, kama nilivyo kuomba hifadhi waziwazi”. Asema: Wakaondoka mpaka walipofika msikitini, akasema Walid bin Mughera: “Huyu hapa Uthman, amekuja kunirudishia hifadhi yangu, akasema Uthman (ra): “Amesema kweli, Nimependa nisiwe na hifadhi isiokuwa ya Allah, nimeshamrudishia hifadhi yake!”

Kisha akaondoka Uthman (ra), na mshairi Labid bin Rabia’h yuko katika mkao wa Maqureysh anawaimbia. Uthman akaketi nao, akasema Labid: “Jueni na mtambue kila kinachoabudiwa asokuwa Allah Ni batil”. Akasema Uthman: “Swadaqta”. Akasema Labid: “Na kila neema lazima zitaondoka” Akasema Uthman: “Umesema uongo Hakika Neema ya watu wa Jannah itabakia”. Akasema Labid bin Rabia’h: “Enyi mkusanyiko wa Maqureysh, Wallahi hiki kikao chenu hakikuwa na maudhi! Haya yamezuka lini?”  Akasema mmoja katika Jamaa: “Hakika huyu ni safihi ana wenzake masafihi, walioacha dini yetu, usipate tabu na maneno yake”. Uthman akamrudishia majibu mpaka maneno yakawa makubwa kati yao. Yule bwana akamwenukia akamtia kofi Uthman mpaka macho yakabadilika rangi kwa kipigo kizito. Na Walid bin Mughera yupo karibu anaona yaliomfika Uthman. Akasema Walid: “Ama Wallahi ewe kijana cha ndugu yangu! Jicho lako lilikuwa na hifadhi kwa yalolipata, ulikuwa katika hifadhi nzuri”, akasema Uthman: “Bali Wallahi! Hakika hili jicho langu zima lahitaji haya yaliolipata hili mwenzake! Na mimi niko katika hifadhi ya Mwenyezi Nguvu na uweza zaidi ewe Aba Abdi Shams!” Kisha akasema Walid: “Njoo ewe mtoto wa ndugu yangu urudi katika hifadhi yako”, Akasema: “Laa”

Na Uthman Ibnu Madh’un (ra) alikuwa ni mshairi akasema kwa yale yaliolipata jicho lake:

Ikiwa jicho langu liko katika radhi za Allah linapatwa na mkono,

Wa anaepinga dini ambaye sie muongofu,

Basi Rahmani amenipa badali yake thawabu,

Na yule aliyeridhiwa na Rahmani enyi jamaa zangu atapata Raha,

Hakika yangu mimi hata mkisema amepotea mjinga yuko katika dini ya Mtume (saw)

Namtaka kwa hilo Allah na haki ni dini yetu

Kusudi kwa atakaye vuka mipaka na kutufanyia uadui

 

Itaendelea katika UQAB Toleo 18…In Shaa Allah.