Njia ya Mtume (saw) Kuleta Mageuzi

بسم الله الرحمن الرحيم

Halaqa 10: Kuvumilia Shida na Maudhi kwa Abubakar Swidiq (ra), Umar Ibnul Khatwab (ra) na Uthman Ibnu Affan (ra) Katika Da’wah

Katika halaqa hii tutaendelea na mbinu ya nne na ya mwisho ambayo wameitumia Maquresh dhidi ya da’wah ya Mtume (saw). Na leo tutazungumzia maudhi na adhabu ambazo wamezipata baadhi ya Maswahaba Radhi za Allah ziwaendee.

Thabat ya Swidiq رضي الله عنه

Kutoka kwa Aisha (ra) asema: Walipokusanyika Maswahaba wa (saw) na wakawa wanaume 83. Abubakar alimkokoteza Mtume (saw) watoke wazi.

Akasema: “Ewe Abubakar! Sisi ni wachache”, basi Abubakar hakuacha kumkokoteza Mtume (saw) watoke mpaka Rasul akatoka wazi. Waislamu wakajigawanya katika vipembe vya msikiti kila mmoja akakaa, ikawa Abubakar ndio mzungumzaji wa kwanza aliyelingania kwa Allah.

Mushrikina wakamshambulia Abubakar na Waislamu, wakapigwa kipigo kikali na Abubakar akakabwa koo kwa nguvu sana na mushrik Utbah Ibnu Rabia’h. Akamsongelea akawa anampiga kwa viatu na kumfutia usoni mwake. Akapigwa Abubakar mpaka pua yake isitambulikane usoni mwake; wakaja Banu Taym na nguo wakamtia nyumbani kwake, wakiamini atakufa…!

Kisha wakarudi Bani Taym wakaingia msikitini Wakasema: “Wallah akifa Abubakar tutamuua Utbah Ibnu Rabiah…! Wakamrudia Abubakar, ikawa Abu Quhafa na Banu Taym wanamzungumzisha Abubakar mpaka akawajibu; alizungumza jioni akauliza: “Mtume (saw) yuko vipi? Hakufanywa kitu Mtume wa Allah?!”

Wa Kwanza Aliye Tangaza Uislamu Wake

Amesimulia Is’haaq kutoka kwa Ibnu Umar (ra) asema: Alipo silimu Umar (ra) alisema: “Qureyshi gani nitampelekea maneno haya?”Akaambiwa: Jamil Bin Muammir, Akamwendea, asema Abdullah ibn Umar, nami nikawa namfuata athari yake, na kuangalia anachokifanya na ilhali mimi ni kijana ninaye fahamu kila ninachokiona mpaka alipomfikia. Akasema:  “Je unajua ewe Jamil kuwa mimi nimesilimu na nikaingia katika dini ya Muhammad (saw)?” Akasema: Wallahi hakumjibu bali aliinuka na kukiburuta kishale cha umar (ra) na Umar akamfuata, nami nikamfuata mpaka aliposimama katika mlango wa msikiti na kupiga kelele kwa sauti ya juu:

“Enyi Maquresh (wakiwa wako katika shughuli zao); Tambueni Ibnul Khattab amewacha dini ya mababu zake…!” Asema: anasema Umar akiwa nyuma yake, amesema uongo, mimi nimesilimu, nikashudia LAA ILAAHA ILLA-LLAH MUHAMMAD RASULU-LLAH! wakamvamia huku wanampiga, basi hawakuacha kupigana mpaka jua likawa utosini mwao!

Asema: Umar alichoka, mwisho akakaa wakamsimamia kichwani naye anasema: “Fanyeni mnachokitaka, naapa kwa Allah lau tungekuwa waume 300, tungewaachia mji ama mtuachie…!” Asema: Walipokuwa katika hali hiyo akatokea mzee wa kiquresh (Al-Aas bin Waail As-Sahmiy) Akiwa na vazi zuri, na kanzu nyeupe akawasimamia na akasema: “Mna nini?” Wakasema: “Umar amewacha dini ya wazee wake”, akasema, “Nyamaza…! Mtu amejichagulia jambo kwa nafsi yake mwataka nini? Mnadhani Baniy Adiy watawaacha mumuuwe huyu mwenzenu?Mmwacheni huyu mtu…!” Asema: Naapa kwa Allah kana kwamba walifunuliwa pazia.

Thabat ya Dhin-Nurayn / Uthman

Amepokea Saa’d kutoka kwa Muhammad Ibnu Ibrahim At-Taymiy asema:  Aliposilimu Uthman ibnu Affanرضي الله عنه , Alichukuliwa na ami yake al-Hakam bin Abi al-Aas Ibnu Umayyah, akamfunga kamba. Akasema: “Unaacha Mila za wazazi wako unafuata dini ya mzushi? Wallahi sitakufungua kabisa mpaka uwache haya uliyo nayo kutokana na hii dini…!”Akasema Uthman:  “Wallahi sitoiwacha milele …!” Al-Hakam alipoona misimamo yake katika dini yake Alimuacha…!

Itaendelea katika UQAB Toleo 15…In Shaa Allah.