Chochote Kinacholevya ni Tembo na Kila Tembo ni Haramu

Habari na Maoni

Habari:

Mnamo Mei 22, 2024, kupitia agizo kuu, Gavana wa Mombasa Abdul Swamad Shariff Nassir alipiga marufuku uingiaji, usambazaji, uuzaji na unywaji wa muguka (aina ya kichocheo maarufu kinachojulikana kama Khat au Miraa) au bidhaa zake Mombasa. Agizo sawia na hilo lilitolewa na magavana wa kaunti za Kilifi na Taita Taveta ambao waliapa kukabiliana na uuzaji na matumizi yake. Baadaye, Rais William Ruto alibatilisha marufuku ya kutatanisha iliyowekwa katika baadhi ya maeneo ya nchi. Ulaji wa machipukizi mapya na majani laini yamelaumiwa kwa kuongezeka kwa masuala ya afya ya akili na kuongezeka kwa matatizo ya kijamii, ikiwa ni pamoja na uhalifu.

Maoni:
Kupigwa marufuku kwa mogukaa kumeibua hisia kali katika kaunti inayolima muguka ya Embu, huku wakulima na wafanyibiashara wakilaani ilani hiyo ya kufunga biashara kutokana na marufuku hiyo. Hata hivyo, marufuku hiyo imepata uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa mashirika ya kidini huku viongozi wa dini ya Kiislamu wakitaka Mugokaa kuainishwa kama dawa za kulevya. Kichocheo hicho ni zao halali chini ya Sheria ya Mazao ya 2013 na Kanuni za Miraa 2023. Rais Ruto amesema Serikali yake imetenga $3.7m (Β£3m) katika mwaka huu wa kifedha ili kupanua kilimo cha mirungi nchini.
Katika mtazamo wa kisekula na kibepari, hakuna sababu kwa serikali yoyote kupiga marufuku mugokaa na vileo vyote. Maadamu viwanda vya kilimo cha mirungi na vileo vinazingatia sheria, basi vinahimizwa kujitanua ili viweze kuchangia maendeleo ya kiuchumi. Kwa vile ukulima wa Khat na mugokaa ni halali katika nchi hii, basi biashara, pamoja na matumizi yake inaruhusiwa kupanuka kama viwanda vingine mradi tu yazingatie masharti yote ya kisheria yanayohusiana nayo. Ni katika muktadha huu, viongozi kutoka maeneo ya kilimo ya Mugokaa wamelia kwa kupigwa marufuku! Hili linaonyesha kipimo kibovu cha mfumo wa kibepari linapokuja suala la wema na ubaya kwani mfumo huo unazingatia tu faida inayozaa. Hivyo kwa muktadha huu, mugoka ni hatari kwa maisha ya binadamu lakini mfumo wa kibepari unaruhusu kilimo na biashara yake kustawi kwa njia inayowezekana kwa njia rahisi zaidi. Kinyume na Uislamu, mtazamo na kipimo cha matendo ya mwanadamu kinategemea ima halali au haramu. Katika hali hii, ikiwa kitu ni haramu, basi kinaharamishwa kabisa bila kujali manufaa ambayo yanaweza kutoka kwayo.
Wengi wa wanaotafuna mugokaa na kunywa pombe ni miongoni mwa maskini na hata matajiri wanadai kufanya hivyo ili kupunguza msongo wa mawazo. Ingawa sababu hii haihalalishi binadamu mwenye akili timamu kujihusisha na vitendo hivyo, ni kweli kwamba Wakenya wengi maskini hujiingiza katika unywaji wa vileo kama β€˜njia ya kutoka’ kutoka kwa matatizo ya kiuchumi. Hii ni natija ya kutabikishiwa kwao kwa itikadi mbovu ya kibepari yenye mfumo mbovu wa kiuchumi unaotazama tu uzalishaji wa rasilimali na kuzifanya kuishia mikononi mwa watu wachache wenye nguvu hivyo kuwaacha wananchi wengine wakisota kwa umaskini. Uislamu, kwa upande mwingine, umekataza wanadamu kupoteza matumaini ya maisha na mfumo wake wa kiuchumi unahakikisha mgawanyo sahihi na sawa wa rasilimali kwa wote na wengine na kutoruhusu watu wachache tu wenye nguvu kunufaika.
Kwa kumalizia, suluhisho la uovu huu liko katika Uislamu. Uislamu kama itikadi unakataza ulaji au matumizi ya kitu chochote kinachoathiri jamii ya wanadamu kiwe cha kiafya au kijamii. Kwa mujibu wa Uislamu, unywaji wa kilevi chochote yaani vileo ni haram na huhesabiwa kuwa ni miongoni mwa matendo ya Shetani yanayopelekea kuchukiza katika jamii bila kusahau kuwapeleka wanadamu mbali na njia ya haki ya kufuata matamanio. matakwa ya Muumba wetu.

Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir
Kenya