Mnamo Jumatatu, 23 Septemba 2019, vyombo vya habari vikuu viliripoti habari za kuporomoka kwa Shule ya Precious Talent huko Eneo Bunge la Dagoretti ndani ya Kaunti ya Nairobi, mji mkuu ambao ni kitovu cha uchumi wa Eneo la Afrika Mashariki na Kati! Katika tukio hilo wanafunzi wanane walifariki na wengi kujeruhiwa. Kilichofuatia ni kulaumiana kwa washikadau katika elimu! Ni miezi michache iliyopita vyombo vya habari viliripoti mkanganyiko kuhusiana na utekelezaji wa Mtaala mpya wa elimu unaojulikana maarufu kama CBC. CBC inalenga kuondosha mpangilio wa 8-4-4 na kuleta 2-6-3-3-3 huku washikadau katika elimu wakitofautiana wengine wakitaka utekelezaji kamili wa mtaala mpya na wengine wakitaka mtaala huo mpya ufanyiwe majaribio kwanza miongoni mwa masuala mengine!
Sintofahau ni jambo la kawaida katika utawala wowote wa kisekula wa kirasilimali pasina na kuzingatia sehemu ilipo katika ramani ya dunia! Kwa kuwa itikadi ya kisekula inatenganisha dini na serikali; hivyo basi inaipa kipaombele akili katika usimamizi wa mambo ya watu. Kwa kuongezea, mfumo wa kirasilimali unachukua manufaa na maslahi kuwa ndio kipimo cha vitendo vya watu na kufaulu kwao ni kulimbikiza madaniya! Kuwepo kwa itikadi ovu na mfumo muovu ikitawala dunia basi mwanadamu daima ameangamia kwa tabu hapa katika dunia ya muda mfupi na yanayomsubiri akhera ni mabaya zaidi! Nidhamu ya elimu katika utawala wowote wa kisekula wa kirasilimali imesimama juu ya lengo moja pekee nalo ni kulinda hali iliyoko kwa maana nyingine kuendeleza mfumo wa kisekula wa kirasilimali na nidhamu zake zinazonuka kama demokrasia, nidhamu ya mujtama wa kihuria, uchumi uliosiamam kwa riba, sera ya kigeni ya kikoloni miongoni mwa nidhamu nyingine. Ili kuifkia lengo hilo, nidhamu ya elimu inakwenda mbio kujenga utambulisho wa kisekula wa kirasilimali (kiakili/aqliyyah na kihisia/nafsiyyah) kwa kupandikiza thaqafa ya kisekula ya kirasilimali (itikadi, mawzo na tabia) katika akili na hisia za wanafunzi. Yafuatayo ni baadhi ya athari za Utekelezaji Nidhamu ya Elimu ya Kirasilimali:
- Uzalishaji idadi kubwa ya ‘raia’ waliolemaa kisiasa, wenye kujisalimisha, mabwege, wasio jitolea pakubwa mbali na miaka 15 na zaidi ya ‘elimu’ yao, kutafiti kwa kina matatizo msingi ya mujtama zao. Baada ya hapo, kusoma sana katika mazingira ya kiimla hivyo basi huachia usimamizi wa mujtama zao kwa uongozi na ujuzi uliopo. Kamwe hawaoneshi hamu ya kuchukua udhibiti wa hatma yao jumla na wala hawaulizi wala hawapingi dhulma za kisiasa, kijamii na kiuchumi wanazofanyiwa!
- Uzalishaji wafanyi kazi. Wamefunzwa ujuzi na cha muhimu zaidi, ujenzi wa nafsiya inayohitajika kwa wafanyikazi wawe kama mashini za viwanda kwa utiifu, kujitolea na wawe wafanyikazi wenye ujuzi watakao kubali uongozi na mamlaka, kuchunga wakati, kuwa na bidii, kufanya wanacho ambiwa, kutumia na kutotarajia kuwa na udhibiti kwa hali yao!
- Kuhalalisha msimamo wa kijamii na ubaguzi. Wale wanaofeli shuleni huona kuwa hawana ‘akili’ na hivyo hawastahili kazi na fursa nzuri za maisha. Hii inachangia kufanya ubaguzi ndani ya jamii kuwa usiokuwa na budi na halali!
- Uzalishaji wa washindani, watu wanaoamini na kupenda ushindani hivyo, washindi huuteka mujtama wote. Hujiona kama wanaostahili fursa walizozichuma kwa tabu. Huku washindwa wakionekana kama wanaostahili hatma yao. Huangazia namna ya kuendeleza maslahi yao binafsi bila ya kutilia maanani manufaa jumla ya watu hivyo kuhalalisha nidhamu inayo pendelea matajiri wakubwa kujitanua!
- Uzalishaji watumizi wenye ari. Watu, wanaojali tu kusonga mbele, kufanikiwa na kutajirika, pamoja na kutafuta maendeleo ya kisasa, kujitanua kwa nidhamu za kimagharibi kama lengo la maisha; na wanao kubali mfumo wa masoko na kudhani kuwa weledi wa kiteknolojia ndio utakao tatua matatizo yao. Kama walivyo lemazwa na utekelezaji vitendo vyao, kufanya kazi kwao, na maamuzi yaliyo wasilishwa kwao na walimu wao hivyo, pia wamelemaa katika utumizi wao wa bidhaa, huduma na maamuzi yaliyo wasilishwa kwao na serikali, mashirika na mabwenyenye wataalamu!
- Viwango vya kushtua vya ukosefu wa ajira kutokana na masomo yanayo endekeza shahada, ambapo wengi wa wanafunzi wamejifunga tu na kuangazia namna ya kupata shahada hizi kama njia ya kuhalalisha uwezekano wa kuajiriwa kinyume na masomo yanayo elekeza katika ujuzi na thamani yake ambayo yamekosekana katika taasisi nyingi za masomo!
Kinyume chake ni nidhamu ya elimu ya Khilafah, imesimama juu ya msingi wa Aqeedah ya Kiislamu na si chengine. (وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الإِسْلاَمِ دِينًا فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ) “Na anayetafuta dini isiyokuwa Uislamu haitakubaliwa kwake. Naye Akhera atakuwa katika wenye kukhasiri.” [Al-e-Imran: 85] Hivyo basi, nidhamu ya elimu ndani ya dola ya Khilafah imeundwa kwa ukamilifu wa hukmu za Kisheri’ah na kanuni za kiidara zinazo husiana na mtaala wa elimu. Hukmu za Kisheri’ah zinazo husiana na elimu zimechipuza kutokana na itikadi ya Kiislamu na zina dalili zake za Kisheri’ah, kama vile masomo yanayo someshwa na kutenganishwa baina ya wanafunzi wa kiume na wa kike. Ama kuhusu kanuni za kiidara zinazo husiana na elimu, ni mbinu na miundo inayojuzu, ambayo Khalifah (mtawala) aliye mamlakani huzikadiria zenye manufaa katika utekelezaji nidhamu na kufikia malengo yake. Ni miongoni mwa mambo ya kimadania yanayo hitajika kwa ajili ya maendeleo na hubadilika kulingana na yale yanayo onekana kuwa muhimu katika utekelezaji wa hukmu za Kisheri’ah zinazo husiana na elimu na mahitaji msingi ya Umma. Vile vile, yanaweza kutabanniwa kutokana na majaribio, ujuzi na utafiti unaojuzu kutoka kwa mataifa mengine. Hivyo basi, ndani ya nidhamu ya elimu ya Khilafah kuna malengo matatu muhimu:
- Uundaji Utambulsisho (Shakhsiya) wa Kiislamu:
Hili hupatikana kupitia kukuza Itikadi, fahamu na tabia za Kiislamu ndani ya wanafunzi ili wawe ni Waislamu wanaouchukua Uislamu kuwa ndio msingi wa pekee wa fikra, maamuzi, matamanio na vitendo vyao vyote na kuunda maisha yao yote kwa mujibu wa Dini yao. Lengo hili litasaidiwa na mazingira ya Kiislamu ya Khilafah ambapo vyombo vyake vya habari, misikiti na taasisi zote nyengine hazitapigia debe chochote isipokuwa fahamu safi za Kiislamu.
- Ufundishaji Ujuzi na Elimu ya Kivitendo kwa Ajili ya Maisha:
Wanafunzi watafundishwa wanachohitaji katika ujuzi na elimu ya kuingiliana na mazingira yao ili kuwatayarisha kuingia katika mzunguko wa maisha ya kivitendo, kama vile hesabu, sayansi jumla na elimu na ujuzi wa kutumia ala na uvumbuzi, kwa mfano vifaa vya umeme na elektroniki, tarakilishi, vifaa vya nyumbani, ala za ukulima na viwanda, na kadhalika. Pia watafunzwa michezo yenye manufaa kama vile kuogelea na ulengaji shabaha, na baada ya kubaleghe watapewa mafunzo ya kijeshi chini ya uangalizi wa jeshi.
- Utayarishaji Wanafunzi Kuingia Vyuo Vikuu:
Wanafunzi watatayarishwa kwa ajili ya kuingia vyuo vikuu kupitia kuwafundisha sayansi msingi zinazo hitajika – iwe za kithaqafa kama Fiqh, Lugha ya Kiarabu, au Tafsiri ya Qur’an, au sayansi za kiutafiti – kama vile hesabu, kemia, bayolojia au fizikia. Lengo ni kuunda shakhsiya, wanazuoni, wanasayansi, na wataalamu wa kipekee katika kila nyanja ya maisha ili kuimakinisha Khilafah kama dola kuu, yenye ushawishi, inayo ongoza duniani. Mbinu za ufundishaji zinazo shajiisha tafakari ya kina zitatumiwa. Sayansi za kiutafiti kwa mfano zitafundishwa kwa njia inayo jenga ujuzi wa kutathmini, na ambapo mada zitatumiwa ili kutatua matatizo halisi ya kimaisha na kufanyiwa utafiti ili kuvua manufaa kutokana nazo ili kutumikia maslahi ya Ummah na kadhia zake nyeti.
Daraja za usomaji shule zitapangiliwa kwa kutegemea Aqeedah ya Kiislamu kwani zimefungwa kwa msingi wa dalili za Kisheria zinazo husiana na hukmu, majukumu, na adhabu tofauti tofauti za Kiislamu zinazo tekelezwa juu ya mtoto katika umri tofauti tofauti. Hivyo basi, daraja za usomeshaji shule ndani ya Dola ya Khilafah zinagawanyika juu ya msingi wa umri wa mwanafunzi na wala sio masomo yanayo someshwa na shule. Shule zinagawanyika aina tatu katika mpangilio ufuatao: mfumo wa 4-4-4, ambayo ni miaka 4 ya kiwango cha msingi (baina ya umri wa miaka 6 – 10), miaka 4 ya kiwango cha shule ya wastani (baina ya umri wa miaka 10 – 14) na miaka 4 ya kiwango cha shule ya upili (baina ya umri wa miaka 14 – 18).
Zaidi ya hayo ni jukumu la Kiislamu juu ya Khilafah kutoa ubora wa hali ya juu wa elimu kwa kila mmoja wa raia wake kama haki msingi – bila ya kujali dini, tabaka, jinsia au kiwango chao cha utajiri. Inawajibishwa kuweka shule za kutosha za msingi na upili na kuajiri walimu wa kutosha kwa raia wote wa dola na kuwapa vifaa vyote wanavyo hitaji ili kufikia malengo ya sera ya elimu bila ya malipo. (Kifungu cha 178, Kielelezo cha Katiba ya Al-Khilafah cha Hizb ut Tahrir). Uwekezaji katika elimu utakuwa ndio kipaumbele cha Khilafah. Kama dola inayo tafuta kuongoza dunia na kuwatumikia watu wake na wanadamu wote kwa jumla kwa ikhlasi, haitakubali nidhamu yoyote ya elimu ya daraja ya pili kutokana na ukosefu wa ufadhili. Bali, itatafuta kuunda wingi wa walimu na wahadhiri walio funzwa vyema na wenye kulipwa vizuri, pamoja na shule, vyuo, vyuo vikuu, vituo vya utafiti, maktaba, maabara na nyengine zaidi za kisasa, zenye vifaa vya kutosha, kwa kutumia mali ya Hazina yake Kuu (Bait ul-Mal), ambayo mali zake zitakuwa nyingi mno kutokana na umbile sahihi la nidhamu ya kiuchumi ya Khilafah. Dola itamsaidia kila mwanafunzi wa kiume na wa kike kufikia uwezo wake kamili bila ya kujali utajiri wao na kuwasaidia kufika kiwango cha juu zaidi cha usomi na ubunifu ili kuzalisha wingi wa mujtahidina, wanasayansi, na wavumbuzi wa kipekee. (Kifungu cha 179, Kielelezo cha Katiba ya Al-Khilafah cha Hizb ut Tahrir)
Utekelezaji wa Shari’ah kwa ukamilifu utapelekea kurudiwa tena kwa ushuhudiaji wa miaka elfu moja iliyo pita, vyuo vikuu maarufu vilikuwepo mjini Gundishapur, Baghdad, Kufah, Isfahan, Cordoba, Alexandria, Cairo, Damascus, na katika miji kadhaa mengine ya biladi za Kiislamu. Elimu ya juu nje ya Dola ya Khilafah wakati wa zama hizo ilikuwepo pekee kostantinia, Kaifeng (Uchina), na Nalanda (India). Na hata zama hizo, Chuo Kikuu cha kostantinia kilikuwa kikiiga vyuo vikuu vya Baghdad na Cordoba. Katika Ulaya Magharibi, zama hizi, hakukuwa na hata chuo kikuu kimoja. Chuo kikuu cha zamani zaidi nchini Italy ni chuo kikuu cha Bologna kiliasisiwa mnamo 1088. Chuo Kikuu cha Paris na Chuo Kikuu cha Oxford viliasisiwa baina ya karne ya 11 na 12, na hadi kufikia karne ya 16 vilikuwa vikiagiza vitabu kutoka kwa ulimwengu wa Kiislamu.
Kozi nyingi za elimu ya juu ndani ya Dola ya Kiislamu ya Khilafah zilichangia katika kuinua hadhara ya Kiislamu. Maelfu ya miaka kabla ya zama za ‘Wright Brothers’, Abbas ibn Firnas alifanya majaribio kadhaa ya kuunda mashini inayo paa. Katika mwaka wa 852, aliruka kutoka juu ya mnara wa msikiti wa Cordoba, akiwa amejitatia nguo iliyo kazanishwa na papi za mbao. Ibn Ismail ibn al Razzaz Al-Jazari, alikuwa mwanasayansi na mhandisi aliyefaulu kuunda robot wa kwanza duniani katika karne ya 12. Aliishi eneo la Mesopotamia na kufanya kazi kwa miaka 25 katika kasri la Sultan Nasir Al-din Mahmoud. Mbali na kufaulu kuunda teknolojia ya robot, pia aliunda vifaa vilivyo rahisisha kazi za mwanadamu, kwa kuziunda ili kutumika kiotamatiki kwa juhudi ndogo za mwanadamu. Mbali na hili, kulikuwa na tafiti na uvumbuzi mwingi zaidi katika zama za Khilafah zilizo badilisha sura ya ulimwengu.
Ali Nassoro Ali
Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kenya
Makala Na.63: Ijumaa, 28 Muharram 1441 | 2019/09/27