Fikra ya Hizb ut Tahrir
Fikra ambayo juu yake imebuniwa Hizb ut Tahrir, inayo wasilishwa katika wanachama wake na ambayo inafanya kazi kuuyeyusha Umma kwayo, ili uichukue kama kadhia yake, ni fikra ya Kiislamu, yaani, ‘Aqeedah ya Kiislamu pamoja na sheria zinazotokamana nayo na fikra zilizo jengwa juu yake.
Kutokana na fikra hii chama hiki kimechukua (tabanni) kiwango fulani kinacho hitaji kama chama cha kisiasa kinacho fanya kazi kuuleta Uislamu katika mujtama, yaani, kuuwasilisha Uislamu katika utawala, mahusiano na mambo kadha wa kadha ya kimaisha. Chama kimeeleza kila kitu kilicho tabanni kwa ufafanuzi ndani ya vitabu na matoleo yake ambao imechapisha, pamoja na dalili fafanuzi kwa kila hukmu, rai, fikra na kila fahamu.