Mahkama ya Qadhi,yenye kufuata muongozo wa hukmu za Sharia kutoka kwa ALlah ﷻ,Alomuumba mwanadamu na Mwenye kumjua hali yake,vyema tangu shina Hadi kilele,imekalia kuti kavu,chini ya tawala za kitwaghuti.Mahkama hio,au hukmu zenye kutolewa na maqadhi wa mahkama hio,zakumbwa na hatari ya kusambaratishwa wakti wowote.Kisha kwa kalamu na karatasi,kunukuu kanuni zenye kutoka kwenye bongo finyo la mwanadamu.
Hatimae, kutolewa hukmu au maamuzi mengine yenye kwenda kinyume na yale yalotolewa na mahkama ya qadhi.Hukmu ambazo chimbuko lake,ni fikra chafu za kimagharibi,zenye kusambazwa na wakoloni,na vibaraka wenye kutawala maeneo tofauti.Kukataliwa hukmu hizo,kwa kupitia kukataa rufaa ktk mahkama ya kitwaghuti kupinga maamuzi yalokwisha pitishwa na Qadhi,au kugurishwa mzozo huo,na kupelekwa mahaka mahkama ya upeo,kutafuta utatuzi kando na mahkama hio!
Licha kuwa,hizi mahkama nyingine,ni za kitwaghuti.Hii ndio hali mbaya ya kusikutisha,yenye kuzikabili mahkama za qadhi chini ya utawala wa kidemokrasia.Sawa iwe nchini Kenya,au ulimwengu kwa jumla.
USHAHIDI WA MATUKIO
Nchini Kenya,kuna matukio kadhaa yalojiri,ambapo mahkama ya Qadhi imetoa hukmu fulani,kisha hukmu ile ikapigwa na chini na mahkama za rufaa au upeo za kitwaghuti!Hapa,tutataja matukio mawili makuu ya hivi karibuni,yenye kuthibitisha namna ya mahkama hii uamuzi wake unavyoweza kuvunjwa bila pingamizi
Kwanza;Maamuzi ya mahkama ya upeo,kupindua maamuzi ya mahkama ya Qadhi juu ya uharamu wa mtoto alozaliwa njee ya ndoa,kuwa na haki ya kumrithi babake huyo.
Pili;Tukio la kupinduliwa maamuzi ya mahkama ya Qadhi,kuhusu Muislam alosilimu;akawa aswali na Waislam.Kisha akafa akiwa Muislam na kuzikwa kwa mila na desturi za Dini ya Kiislam Kijiji cha Takaungu.
Hatimae,jamaa zake ambao si Waislam,wakapinga maamuzi hayo kwa kukata rufaa.Na mahkama ya rufaa ikapindua maamuzi ya mahkama ya Qadhi.Na kusema kuwa mahkama ya Qadhi haina mamlaka hio.
CHIMBUKO LA MZOZO HUO!
Mkwaruzano baina ya uamuzi wa mahkama hizi mbili:mahkama ya Qadhi na zile za kitwaghuti,watokamana na kuwa,chini ya nidhamu ya utawala ya kidemokrasia,Dini na hukmu zake,hazifai kuhusika kwenye kusimamia au kuendesha maisha ya mwanadamu!Sawa awe Muislam au laa!
Kwa mtazamo huu muovu wa nidhamu hii ya mfumo wa kibepari,mwanadamu kufuata Dini,ni suala na khiyari kwa mtu binafsi.Ni makosa kumlazimisha kujifunga na hukmu za Dini au hata kuamini uwepo wa ALlah ﷻ.Na iwapo Kuna watu wenye kutaka kuamini uwepo wa ALlah ﷻ,basi mafunzo ya Dini hio,lazima yabaki ndani ya pembe nne za majumba ya Ibada!
Hali hii,yafanya mahkama ya Qadhi,kuwa duni na dhaifu.Kwa sababu,maamuzi yake yaweza kuvunjwa na kukataliwa mara moja.Kando na kuhatarisha uwepo wa mahkama hio, ndani ya katiba ya kiilmaniya:yenye kubagua Dini na siasa.Ndio ilipokuwa yabuniwa katiba ya Kenya ya 2010.Na Ummah kushirikishwa kwenye kutoa maoni,kulikuwa na maoni ya kuiondoa mahkama hio na kutoitambua.
Kwa tuhma za kupendelea jamii moja ya Waislam!Na na kuwa uwepo wa mahkama yenye kuzingatia maadili na muongozo wa Dini, ni KUCHANGANYA Dini na siasa,kinyume na demokrasia. Jambo lilozua mvutano na mjadala mrefu.Na kesi hio kupelekwa mahkama ya upeo.Hatimae mahkama hio ikaamua kuibakisha mahkama ya Qadhi,kwa kisingizio cha kuenzi uhuru wa kuabudu
Maamuzi haya,huenda yalichochewa na mambo kadhaa.
Pili:Msimamo wa Waislam
Waislamu wote,bila kujali madhab zao, walisimama kidete kuitetea mahkama ya Qadhi.Wakiongozwa na harakati kadhaa ikiwemo, Hizb-ut-Tahrir Kenya ilokuwa na msururu wa darsa,kukusanya sahihi z Waislam,mihadhara nk kutetea mahkama hio ambayo,ilikuwa yakumbwa na tishio la kubanduliwa kutoka kwenye katiba mpya!Wakati huo,Kenya ilikuwa yatoka kwenye uchaguzi wa 2007.Ambao ulishihudia ghasia na fujo kubwa kabisa.
Kutuliza hali,raia walipewa nafasi ya kutoa maoni na kuchangia ktk utunzi wa katiba mpya.Na Waislam wakatulizwa kwa kuachiwa mahkama ya Qadhi .Lakini tofauti na ile ilotangulia,katiba hii ikaja kuidunisha mahkama hio na kufanya uamuzi wa maqadhi kuwa ukingoni.
2)Makubaliano ya Shamte
Makubaliano haya, yahusu makubaliano ya mwaka 1963. Ambapo Sultan wa Zanzibar:Jamshid bin Abdullah alikubali kuikabidhi Kenya,kisha bila fidia yoyote,Ukanda wa Pwani ya Zanzibar,iliogusanna na Kenya.Maafikiano haya, yalikuwa sehemu ya mazungumzo makubwa zaidi kati ya dola vamizi ya kikoloni: Uingereza,na vibaraka wake:Kenya na Zanzibar.
Pia,makubaliano hayo yalijumuisha masharti ya kulinda haki na uhuru wa Waislamu katika Ukanda wa Pwani yakiwemo:Kwanza:hifadhi wa Mahakama za Qadhi.Pili:Kutambuliwa kwa umiliki wa ardhi wa kudumu (freehold titles).Hivyo,huenda Mahkama ya upeo,ilihofu kuvunja mikataba ya kimataifa,ili kulinda hadhi ya Kenya kwenye ulingo wa kimataifa.
KUASISIWA MAHKAMA YA QADHI
Mahkama ya Qadhi,ni miongoni mwa vitengo vya muundo wa Dola ya Kiislam.Kando na Khalifah,Amir,Wali,Wasaidizi,Jeshi,majlisus shura na kadhalika.Aidha,mahkama hii ilikuwepo tangu kuanzia Dola hio ilipobuniwa na Ar Rasulﷺ mjini Madina,kuafuatia tukio la kihistoria na kiimani la Hijara.Lilo leta mageuzi makubwa ndani ya Uislam kama mfumo kamili wa Kiislam.
Mageuzi hayo,yaligusa nyanja zote za maisha:
°Uchumi
°Jamii
°Elimu
°Utawala
°Siasa za ndani na njee ya Dola hio.
Hivyo,kuwa na udharura wakuwepo kwa mtawala, jeshi,askari,mahkama,ili kutabikisha Ahkam zenye kuhusiana na nyanja hizo,na kusimamia mahusiano baina ya raia wake.Waislam na wasokuwa Waislam,walojulikana kwa fiqh ya utawala,kama madhimmi.
Hivyo basi,mahkama ya Qadhi,ni miongoni mwa mahkama kongwe zaidi miongoni mwa historia ya mahkama.Barani Afrika, mahkama hii ilikuwepo,hata kabla ya uvamizi na ugawajwi wa Afrika na wakoloni,na kuzaliwa mataifa haya yaliopo leo.
MAMLAKA NA UWEZA WAKE(JURISDICTION)
Kama inavyobainishwa kwenye mafunzo ya Qur’an,Sunnah,Ijmaai na kufafanuliwa vyema ktk fiqh ya utawala,mamlaka na uweza wake wa kisharia,utenda Kazi wake uligusa sehemu zote za maisha.Wala haukufungwa kwenye kutatua mizozo fulani; miongoni mwa watu wenye kuamini Imani ya Kiislam pekee.Kisha kwa wao kuridhika kwenda kutatua mzuzo huo kwa mahkama hio.Wasiporidhika,wana haki kutafuta uvumbuzi wa mzozo kwengine!
USHAHIDI WA KWELI WA KIHISTORIA (FACTUAL HISTORICAL EVIDENCE)
Qur’an na mafunzo yake,ni muongozo kamili wa maisha ya mwanadamu.Na imeteremshwa kumtatulia mwanadamu matatizo yake yote,atakayokukumbana nayo,ktk kila nyanja za maisha.Kuanzia muongozo wa kiroho,hadi utatuzi wa,kiuchumi,kijamii,kielimu na mizozo baina ya raia na watawala.
الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا
“Leo Nimewakamilishia dini yenu,na Nimewatimizia neema Yangu juu yenu,na Nimewaridhia Uislam kuwa ndiyo Dini yenu!”
Kwa sababu ALlah ﷻ Ameikamilisha Dini,ina maana hakuna kilichoachwa au kusahauliwa.Ndio ALlah ﷻ,Akamwambia Ar Rasulﷺ,asikubali kufuata hukmu za Kiislam zote.Lkn akaacha kufuata baadhi japo kidogo!
وَأَنِ احْكُم بَيْنَهُم بِمَا أَنزَلَ اللَّهُ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَهُمْ وَاحْذَرْهُمْ أَن يَفْتِنُوكَ عَن بَعْضِ مَا أَنزَلَ اللَّهُ إِلَيْكَ ۖ فَإِن تَوَلَّوْا فَاعْلَمْ أَنَّمَا يُرِيدُ اللَّهُ أَن يُصِيبَهُم بِبَعْضِ ذُنُوبِهِمْ ۗ وَإِنَّ كَثِيرًا مِّنَ النَّاسِ لَفَاسِقُونَ
“Hukumu baina yao kwa Alichoteremsha ALlah,wala usifuate matamanio yao. Na utahadhari nao wasikufitinishe na baadhi ya Aliyo kuteremshia ALlah. Wakikengeuka,basi jua kwamba ALlah Ataka kuwapata kwa baadhi ya dhambi zao.Na hakika wengi katika watu ni wapotofu!”
Naam. Mtume wa MwenyeziMungu ﷺ alitumia hukmu za Qur’an kuwahukumu watu wote.Bila kubagua Muislam au laa. Tukio maarufu ni pale alipohuku kwa uadilifu mkubwa baina ya myahudi alokuwa raia wa Dola ya Kiislam alotuhumiwa kuiba dir’i na Tu’ma ibn Uraiq ambae alikuwa mnafiki aloiba kisha akaificha kwa jirani yake myahudi.
Kama ilivyozungumziwa ktk Aya hii:
أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يَزْعُمُونَ أَنَّهُمْ آمَنُوا بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ يُرِيدُونَ أَن يَتَحَاكَمُوا إِلَى الطَّاغُوتِ وَقَدْ أُمِرُوا أَن يَكْفُرُوا بِهِ وَيُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَن يُضِلَّهُمْ ضَلَالًا بَعِيدًا
“Jee,hukuwaona wale wanaojidai kuwa wameamini yaliyoteremshwa kwako na yaliyoteremshwa kabla yako wataka kuhukumiwa na twaghut(kanuni za kibinadamu)na wameamrishwa kuzikataa.Na Shetani ataka kuwapoteza upotevu wa mbali.”
An Nisaai 60
Tukio jengine,lahusu kuuliwa kwa AbdaLlah bin Sahl sehemu za Khaybar;ambayo ilikuwa ngome ya Mayahudi.Kama alivyosimulia Al Imaam Malik ibn Anas,ktk kitabu chake Al Muwattwa.
Wapwa zake AbdaLlah bin Sahl,Muhayyiswa bin Masud na Huwayyiswa bin Masud wakenda kushtaki kwa Ar Rasulﷺ kuwa mtoto wa ami yao ameuliwa na mayahudi
Na Mtume wa MwenyeziMungu SAAW akawaandikia barua walipe diya au jihad.Wakajibu kuwa wao hawakumuua.Ar Rasulﷺ,akawauliza kina Muhayyiswa kama waweza kuapa.Wakashindwa kwa kuwa hawakumuona alomuua. Mtume lﷺ akaiamua kesi hiyo kwa hukmu ya Al Qasaamah:
Matukio haya,yadhihirisha kuwa Ar Rasulﷺ,aliwahukumu raia wote Waislam na wasio Waislam kwa Hukmu za ALlah ﷻ.Na kwamba hukmu hizo zilitolewa kwa uadilifu bila mapendeleo yoyote.Na Kuna mifano mengine meengi baada ya kufa kwake Ar Rasulﷺ.
Enyi Waislam!
Hadhi na hishma yetu,na walimwemgu kwa jumla,hupatikana chini ya utawala wa Kiislam Khilafah Rashidah pekee.Hakuna uadilifu wala usawa chini ya nidhamu ya utawala ya kitwaghuti demokrasia,na mfumo wake wa maisha ubepari.
Enyi Waislam!
Hukmu Za ALlah ﷻ,haziwezi kuhifadhika wala kutekelezwa kivitendo chini ya mfumo wa kikoloni ubepari demokrasia.Leo walimwemgu wapapatika.Kutafuta amani utulivu na haki.Na sisi tuna muongozo kutoka kwa Qur’an,Sunnah na ijmaai ya maswahaba.
Ni wajib wetu kiwafikishia kikamilifu,kwa kuasisi Dola ya Kiislam halisi:Khilafah Rashidah
Hussein Muhammad
Mwanachama wa Hizb-ut-Tahrir Kenya.