Hizb ut Tahrir /Kenya Ilifanya Maandamano Baridi Kulikumbuka Tukio la Kiza la Kuanguka kwa Khilafah yetu
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ikiwa ni ukumbusho wa 98 H (95 M) wa kuanguka kwa Khilafah, Hizb ut Tahrir /Kenya ilifanya maandamano baridi baada ya swalatul Dhuhur siku ya Jumatano, 3 Aprili 2019 ikiwa ni sawa na 27 Rajab 1440 H katika miji mikuu miwili ya Kenya katika Nairobi na Mombasa. Maandamano baridi yaliongozwa na Shabani Mwalimu –Mwakilishi Kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya miongoni mwa wazungumzaji waliowakumbusha Ummah mtukufu wa Waislamu moja ya matukio yenye kiza katika historia yake; ambalo ni Kuanguka kwa Khilafah mnamo 28 Rajab 1342H sawa na 3 Machi 1924 M.
Ummah wa Waislamu ulikumbushwa kuhusu hali yake inayokumbana nayo tangu kuvunjwa kwa Khilafah. Ummah wa Waislamu umezungukwa kutoka pande zote na tawala ovu za kisekula za kimagharibi na ambazo zinawatishia kifo kutokana na sera na sheria zao kuhusiana na misimamo mikali na ugaidi. Ukiwa na idadi ya watu zaidi ya bilioni moja, Waislamu wamekuwa sawa na povu katika bahari kwa sababu ya kukosekana kwa Khilafah kama mlinzi na ngao yake! Ukumbusho wa mwaka huu umekuja wakati ambapo ni wiki chache tu baada ya shambulizi la New Zealand ambapo maisha ya Waislamu 50 wasiokuwa na hatia walipoteza maisha yao! Ukumbusho huu unakuja wakati ambapo uhalifu wa utawala wa Uchina unaendeleza ukandamizaji wa Waislamu wa Uyghur kwa kutumia kila njia za kinyama. Kwa kukosekana Khilafah na Khalifah, Ummah wa Waislamu umepoteza hadhi, heshima na mlinzi. Ummah wa Waislamu umepoteza Palestina na Al-Aqsa, Ardhi Tukufu ya Israa wal Mi’raj na kibla chetu cha kwanza. Na ni Khilafah pekee ndiyo ambayo itaweza kuirudisha pamoja na ardhi zote za Waislamu zilizovamiwa.
Tuna hakika kuwa kurudi kwa Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume kwamba wakati wake umefika. Hivyo basi, Ummah wa Waislamu utailinda Dini, maisha na matukufu yake siku hiyo, utakuwa mshindi kutokana na ushindi wa Mwenyezi Mungu (swt).
﴾لِلَّهِ الْأَمْرُ مِن قَبْلُ وَمِن بَعْدُ وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ﴿
“Amri ni ya Mwenyezi Mungu kabla na baada yake. Na siku hiyo Waumini watafurahi.” [Ar-Rum: 4]
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya
KUMB: 1440 / 09
Alhamisi, 28 Rajab 1440 H /
04/04/2019 M
Simu: +254 707458907
Pepe: mediarep@hizb.or.ke