Hizb ut Tahrir /Kenya Uzinduzi Rasmi wa Kampeni Maalumu chini ya mwito: Kuzidi Kwa Gharama za Maisha: Uislamu Ndio Tiba

Taarifa Kwa Vyombo vya Habari

Hizb ut Tahrir /Kenya inafuraha kuzindua rasmi kampeni maalumu itakayoendelea kwa miezi mitatu kwa mwito “Kuzidi kwa Gharama za Maisha: Uislamu Ndio Tiba” itakayoanza Jumapili, 13 Januari 2019 na kuisha mnamo Ijumaa, 5 Aprili 2019.

Lengo la kampeni ni kufichua dori ya ukoloni urasilimali katika kuendeleza matatizo ya kiuchumi kwa ujumla ambayo yanaendelea kulisakama taifa la Kenya ikijumuisha madeni makubwa kufikia Trilioni Ksh.5.7 na raia wakiendelea kuishi maisha magumu na duni. Kampeni hii pia inatarajia kuwasilisha suluhisho la Kiislamu katika kutatua changamoto za kiuchumi kama mfumo kamili ulio na sheria za kutatua matatizo yote yanayowakumba wanadamu.

Ili kufaulisha Kampeni hii, Hizb ut Tahrir /Kenya itaandaa msururu wa matukio ikijumuisha darasa/mihadhara, ziara kwa wasomi wakijumuisha wakiuchumi ndani ya taifa hili pamoja na amali nyinginezo.

Kampeni hii ni moja ya kazi za Hizb ut Tahrir katika kujenga rai jumla kwa kuwasilisha mtizamo safi wa kiuchumi kwa msingi wa Uislamu ambao ulitekelezwa kwa karne 13 na Dola ya Kiislamu ya Khilafah na kutatua kivitendo matatizo ya kiuchumi. Tunaamini kuwa kuvunjwa kwa Khilafah kutokana na mikono ya wamagharibi mwaka 1342H sawia na 1924M ndiyo chanzo cha changamoto za kiuchumi na matatizo jumla yanayoukumba ulimwengu leo. Pia, tuna yakini kuwa suluhisho la kuzidi kwa gharama za maisha na maovu yanayo waandama wanadamu ni kwa kuondosha mfumo wa dhuluma wa kirasilimali na kuweka mahala pake mfumo wa Kiislamu chini ya kivuli cha Khilafah kwa njia ya Mtume Muhammad (saw). Kurudi tena kwa Maisha ya Kiislamu kupitia kusimamisha tena Khilafah ndio itawakomboa tena wanadamu kutoka katika majanga ya kiuchumi na maovu ya kila aina kwa kuutekeleza kikamilifu mfumo wa Uislamu na nidhamu zake ikijumuisha ile ya nidhamu ya kiuchumi wa Uislamu pamoja na sera yake bora iliyomo ndani yake.

Kwa kutamatisha, tunatoa mwito kwa Ummah jumla hususan Ummah wa Waislamu washiriki nasi katika kampeni hii adhimu ambayo inatarajia kuzindusha mengi na ambayo yatatufaa hapa Duniani na Akhera.

Fuatilia Hashtags Zifuatazo:

Kiengereza: #IncreasedCostOfLiving_IslamIsTheSolution

Kiswahili: KuzidiKwaGharamaZaMaisha_UislamuNdioTiba

 

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya

KUMB: 1440 / 03

Jumamosi, 06 Jumada I 1440H

12/01/2019 M

Simu: +254 707458907

Pepe: mediarep@hizb.or.ke