Hizb ut-Tahrir Kenya yaandaa amali kadhaa kwenye kampeni ya kiulimwengu: Ukombozi wa Konstantinopoli bishara njema iliotimia ikifuatiwa na bishara njema nyengine.
Taarifa Kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut-Tahrir Kenya yaandaa amali kadhaa kwenye kampeni ya kiulimwengu: Ukombozi wa Konstantinopoli bishara njema iliotimia ikifuatiwa na bishara njema nyengine.
Chini ya uongozi wa Amir wa Hizb ut-Tahrir mwanachuoni mkubwa Ataa Bin Khalil Abu Al-Rashta, Allah amuhifadhi, Ofisi kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir ilizindua kampeni kubwa ya kiulimwengu kukumbuka tukio la kukombolewa kwa Constantiniyya #Constantiniyya (Mji wa Hiraqla uliozingirwa kuanzia tarehe 26th Rabiul Awwal hadi tarehe 20th ya Jumada al-Awwal mwaka 857 AH sawa na tarehe 5 April hadi 29 Mei mwaka wa 1453 ikawa kwa hilo bishara ya hadithi tukufu ya bwana Mtume SAAW ikatimia.
«لَتُفْتَحَنَّ الْقُسْطَنْطِينِيَّةُ فَلَنِعْمَ الْأَمِيرُ أَمِيرُهَا وَلَنِعْمَ الْجَيْشُ ذَلِكَ الْجَيْشُ»
”Itafunguliwa Konstantiniyya basi amir bora ni amiri wake na jeshi bora ni jeshi hilo.”
Kwa upande wake kwenye kampeni hii ya Kiulimwengu,Hizb ut-Tahrir Kenya ilifanya kumbukumbu yake kwa kushiriki kwenye kipindi mubashara katika Radio Rahma mnamo tarehe 13 January 2020. Kwenye kipindi hicho mwakilishi kwa vyombo vya habari Hizb ut-Tahrir Kenya Shabani Mwalimu akiwa pamoja na mwanachama wa ofisi ya habari Ali Omar walizungumzia kuhusu ukombozi wa Constantiniyyah bishara njema iliotimia na nyengine kufuatia.
Na katika siku ya Jumatano 15th, 2020, sawa na 20th Jumadal Awwal 1441 wanaharakati wa Hizb ut-Tahrir wakaandaa mfululizo wa maandamano baridi na darasa mbalimbali kote nchini Kenya. Mjini Mombasa maandamano hayo yalifanywa nje ya msikiti wa Al-aqswa Kisauni, Msikiti wa Khairat Kilifi na msikiti wa LungaLunga. Kwenye maandamano hayo, wanaharakati waliweza kubeba mabango yenye ujumbe usemao: *“Ukombozi wa Konstantinople Bishara njema iliotimia na zikifuatia na nyengine njema! Kurudi kwa Khilafah chini ya manhaj ya Mtume (Saaw), kuwapiga na kuwashinda kabisa mayahudi na kukombolewa kwa mji wa Roma.”
Maghrib mwa siku hiyohiyo baada ya swala ya Maghrib wanaharakati wakiongozwa na Shabani Mwalimu wakafanya darasa kubwa katika miji ya Mombasa, Nairobi na Kilifi. Maudhui hasa yakawa ni kuhimiza umma wa Kiislamu kuwa na yakini juu ya kutimia kwa bishara njema tatu za Mtume wa MwenyeziMungu ( saw), kwani Mtume (Saw) hazungumzi ila kwa Wahyi. Aidha, wazungumzaji wakahimiza kusema kwamba bishara njema hazitotimia kwa kuteremshwa Malaika kutoka binguni wakiwa nazo, kwani ni katika sunna ya MwenyeziMungu kwamba sisi tukijifunga kikamilifu katika kufuata maamrisho yake kumnusuru Yeye Allah kwa kufanya kazi ya kuisimamisha tena Khilafah ya pili kwa mfumo wa Mtume Muhammad (Saw) na hapo ndiyo MwenyeziMungu (swt) atatupa nusra yake.
[وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ بِنَصْرِ اللَّهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ]
“Na siku hiyo Waislamu watafurahi,Kwa nusra ya MwenyeziMungu. Humnusuru Amtakaye ; Naye ni Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. [Ar-Rum: 4-5]
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari Hizb ut Tahrir in Kenya.
KUMB: 1441 / 04
Ijumaa 22 Jumadal awwal 1441 H /
17/01/2020 M
Simu: +254707458907
Pepe: mediarep@hizb.or.ke