Hizb ut Tahrir Kenya yafanya msururu wa Matukio kwa kumbukizi la miaka 104 la Kuvunjwa Utawala wa Khilafah

Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari

Kama sehemu ya kumbukumbu ya miaka 104 ya kuangushwa kwa Khilafah (Ukhalifa). Hizb ut Tahrir / Kenya ilifanya kampeni nchi nzima katika mwezi mtukufu wa Rajab 1446 AH.

Kampeni hii ilioanza mapema mwezi mtukufu wa Rajab ilijumuisha amali mbalimbali; Darasa kwa umma, Semina na maandamano baridi. Hii ilikuwa ni kuukumbusha Ummah juu ya hali yake ya kutamausha ambayo umekuwa ukikabiliana nayo tangu kuvunjwa a kwa Khilafah mnamo tarehe 28 Rajab 1342 Hijria sawia na tarehe 3 Machi 1924 CE.

Licha ya idadi ya Waislamu kukurubia bilioni 3, wamekua ni sawa na povu baharini kwa sababu ya kutokuwepo kwa Khilafah kama mlinzi  na ngao yake! Ummah umewahi umepoteza utu, heshima na mlinzi wake. Umbo la Kiyahudi la kimauaji likisaadiwa na mataifa ya kimagharibi yenye kiu cha damu limefanya mauaji ya halaiki kwa watu wa Gaza. Na huko Syria, mapinduzi ya yaliyobarikiwa yamefanikiwa kumwangusha kiongozi mbaya lakini wamagharibi wanafanya kazi kurejesha uongozi mwingine wa kisecular.

Kuangushwa  kwa Khilafah ni tukio la ovu na la kuhuzunisha lililoacha Ummah baada ya umoja wao, ukagawanywa kwenye ule mradi wa kikoloni wa Sykes-Picot na wao ardhi kukoloniwa na wakoloni. Damu za Waislamu zimemwagika katika ngome ya  Uislamu Sham na hadi hali hii haijawahi kuchemsha mishipa ya Majeshi ya Kiislamu kuwaunga mkono Mujahidina. Wale wanaoitwa viongozi wa upande wao wameamua kusalia kimya cha wafu!

Tunamuomba MwenyeziMungu SWT aharakishe kusimamisha Khilafah Raashida kwa mfumo wa  Mtume

{وَاللَّهُ غَالِبٌ عَلَى أَمْرِهِ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ}

Na MwenyeziMungu Ndiye Mwenye kushinda juu ya Jambo lake lakini Watu wengu hawajui

 

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari Hizb ut Tahrir

Kenya