Huduma zote ambazo Mamlaka ya Palestina imewahi kuitolea Amerika na Mayahudi hazikuwapa hata neema kidogo mbele ya Trump hata makombo ameyakata!

Habari:

Jioni ya Jumatano, tarehe 19 Februari 2025, utawala wa Marekani ulitangaza kusitisha kwa asilimia mia moja ufadhili wote uliokuwa umetengwa kwa ajili ya vyombo vya usalama vya Mamlaka ya Palestina. Maafisa wa PA waliiambia The Washington Post kuwa hatua hiyo inaathiri uwezo wa vikosi hivyo kazini na kuathiri pia programu za mafunzo na vituo vya usalama vya Palestina. Chanzo kutoka kwa entiti ya Kiyahudi kiliiambia The Washington Post kuwa uratibu wa kiusalama kati ya entiti hiyo na PA hautaathirika, na kwamba “wafadhili wengine” tayari wamepatikana na wamekubali kuziba pengo lililoachwa na Marekani.

(Chanzo: Ma’an News Agency, kimehaririwa kidogo, 19/02/2025)

 

Maoni:

Ni kweli kwamba Trump alikuja na fikra ya mfanyabiashara, si ya mwanasiasa. Alitangaza tangu mwanzo kuwa anataka kukusanya pesa na kupunguza matumizi, akilitazama dola kama kampuni ya kibiashara yenye lengo la faida mafanikio yakipimwa kwa faida halisi (mapato pungufu ya matumizi). Hii imeathiri taasisi nyingi, mashirika, na hata nchi zilizokuwa zinategemea makombo kutoka Marekani.

Lakini uamuzi huu una ishara na athari nyingine kadhaa, zikiwemo:

1.Fedha ambazo Amerika ilikuwa ikitumia kwa PA zilikuwa kwa ajili ya vyombo vya usalama tu zana za kuifunga PA na ajenda ya Kimarekani na kuiwezesha kuendelea kutoa huduma ya uaminifu kwa entiti ya Kiyahudi.Hii ndiyo inayoitwa uratibu wa kiusalama, ambao umekuwa kama pumzi ya uhai ya PA na vyombo vyake vya usalama. Hizi ni fedha chafu kwa kazi chafu Allah asizibariki, wala asiwabariki waliotuma wala waliotumia.

2.Yule atakayeathirika zaidi kwa kukatwa kwa ufadhili huu ni entiti ya Kiyahudi yenyewe,kwa kuwa ni vyombo vya usalama vya PA vinavyolinda entiti hiyo. Kilichotokea wakati wa Operesheni Dhoruba ya Al-Aqsa na ndani ya miezi 16 iliyopita hasa miezi miwili ya mwisho kinathibitisha hili.PA imeongeza uratibu wa kiusalama, imewafuatilia wapiganaji wa muqawama, kuwakamata, na hata kuwaua baadhi yao kama ilivyotokea katika kambi za Jenin na Tulkarm, hadi haijabaki hata jani la mtini kuficha ushirikiano wao na entiti ya Kiyahudi.

3 Inawezekana Trump hatakitupa kabisa kifaa hiki cha PA na vyombo vyake vya usalama, kwa sababu vinahudumia maslahi ya Amerika na Mayahudi. Badala yake, atahakikisha angalau kiwango cha chini cha fedha kinapatikana kupitia watawala vibaraka kama wa Saudia,UAE, na Qatar. Kwa hivyo, atakuwa ametumia pesa za Waislamu wenyewe kuifadhili mamlaka inayopinga Uislamu na Waislamu.

4.Iwapo Trump ataamua kutotoa mbadala wa ufadhili, basi ujumbe wake kwa PA ni kuwa ijitegemee juu ya migongo ya watu wa Palestina kwa kuongeza kodi,ushuru, na ulazima wa michango  kuwakandamiza zaidi na zaidi hadi walazimike kuhama. Kwa namna hii, atakuwa amepiga ndege wawili kwa jiwe moja, kama methali inavyosema.

Uamuzi wa Trump ni funzo kwa kila msaliti na wakala: kwamba mwisho wa usaliti ni fedheha na hasara.Na adhabu ya dunia ni nyepesi sana ukilinganisha na ile ya Akhera, ambako maneno ya Mwenyezi Mungu yanawahusu:

Na wale waliowafuata watawatazama (viongozi wao) na kusema: ‘Laiti tungeweza kurejea tena, tungeliwataa kama walivyotutaa sisi.’ Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu atakavyowaonyesha matendo yao kuwa majuto juu yao, wala hawatatoka Motoni.”

(Surah Al-Baqarah: 167)

 

Iliandikwa kwa ajili ya Redio ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Mhandisi Baher Saleh

Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir