Uislamu ni mfumo au muongozo wa maisha jumla. Kuwa na imani ya Uislamu kunatakiwa kuwe ni kwa njia ya kukatikiwa yaani kuwa na yakini juu ya kuwepo kwa Mwenyezi Mungu (swt). Yakini hii inapatikana kwa kutumia ishara ambazo hukinaisha akili tena ukinaifu uso kuwa na shaka hata chembe. Kwa yeyote atakayetumia akili yake kwa kuuangalia ulimwengu, mwanadamu na uhai basi atakatikiwa kiakili kuwa nyuma ya vitu hivi vitatu yupo Muumba naye si mwengine isipokuwa Mwenyezi Mungu (swt). Kukatikiwa huko kunampelekea huyo aliyekatikiwa kutaka kujua lengo la kuumbwa kwa vitu vitatu hivyo. Hivyo basi, inakuwa hana budi kumfuata mmoja miongoni mwa wanadamu ambaye amechaguliwa na Muumba na kupewa wahyi/muongozo kutoka kwa Mwenyezi Mungu ili aweze kuwafikishia wanadamu wenzake namna ya kuendesha maisha yao jumla kwa mujibu wa maamrisho na makatazo ya Muumba. Naye si mwengine isipokuwa Mtume wa mwisho Muhammad (saw).
Kwa mujibu wa maelezo hayo yanatudhihirishia kuwa kila Muislamu lazima ajifunge na imani/itikadi kuwa Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na Muhammad ni Mtume wake. Na itikadi hiyo iwe ndio marejeo yake kwa kila tatizo analokumbana nalo. Nayo ndio kipimo cha kupimia fikra na matendo yake. Kwa kifupi kupitia imani/itikadi hii Muislamu anaendeshea maisha yake yote. Kwa maana nyingine ni kuwa anapima vitendo vyake vyote kwa mujibu wa Halali (imeruhusiwa) na Haramu (imekatazwa) kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Kwa sababu hiyo ndoa ni sehemu katika vitendo ambavyo Muislamu ameruhusiwa.
Hivyo basi hukumu ya Kiislamu kwa waliooana na kuingiliana kisha mmoja wao akaritadi. Yafuatayo yatatokea:
Kwanza: Aliyeritadi (Murtad) atapewa nasaha mara tatu (3) atubiye na arudi katika Uislamu. Lau atakayekuwa ameritadi ni mwanamume; basi mke/wanawake wanatakiwa kukaa eda kuanzia punde tu itakapojulikana ameritadi. Ikiwa atatubu na kukubali nasaha basi atapiga tena shahada na atakuwa ni Muislamu. Kama itakuwa eda ya mke/wanawake bado haijaisha basi atamrudia mkewe/wakeze na Lau itakuwa eda ishakwisha itabidi waoane tena kwa mujibu wa masharti ya ndoa. [Imamu Shafi na Imamu Hanbali]
Pili, Ikiwa amekataa kurudi katika Uislamu baada ya kunasihiwa mara tatu (3). Basi amepoteza haki ya udugu (uzao), kuheshimiwa, kulindwa, kuhurumiwa, kurithi au kurithiwa. Itastahili auliwe: Mtume (saw) asema: “Yeyote anayetoka katika Uislamu na kwenda dini nyingine, basi muueni”. [Sahih Bukhari na Sahih Muslim]. Lau atatekelezewa hukm ya kifo, basi itakuwa amekufa kafiri na hastahili: kuoshwa, kukafiniwa, kuswaliwa na kuzikwa katika maziara ya Waislamu.
Tatu, Atakayekuwa amebakia katika Uislamu ndiye atakayekabidhiwa haki ya usimamizi na ulezi wa watoto. Lau itakuwa aliyebakia katika Uislamu ni mwanamume basi atakabidhiwa watoto na hivyo kuwasimamia na kuwalea ikiwa hana uwezo atastahili kusaidiwa na watu wanaomrithi au nduguze na ikiwa nao hawana uwezo basi serikali ya Kiislamu ya Khilafah yatakiwa kumuwezesha kupitia Bait ul-Mal. Na lau itakuwa ni mwanamke ndiye aliyebakia katika Uislamu basi msimamizi (walii) wa mwanamke atakuwa na jukumu la kumsimamia huyo mwanamke pamoja na watoto wake kila kitu. Ikiwa itakuwa huyo msimamizi hawezi kuwasimamia basi serikali ya Kiislamu ya Khilafah yatakiwa kumsimamia kupitia Bait ul-Mal.
Hakika kufaulisha nukta hizo tatu kwa ukamilifu wake hatuna budi kufanya kazi ya kurudisha utawala wa Kiislamu wa Khilafah kwa njia ya Utume. Hapo ndipo hukm zote za Kiislamu zitakapoweza kufanyiwa kazi kwa ukamilifu na kila suala litapata utatuzi kwa mujibu wa Shari’ah (Qur’an na Sunnah). Kinyume chake ni kuishi chini ya imani/itikadi batili ya kisekula inayotokana na akili iliyo na kikomo na mfumo wake muovu wa kirasilimali unaopima vitendo kwa maslahi! Hatima yake ni kukithiri kwa maasi!
Ali Nassoro Ali
Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kenya
Makala Na.49: Ijumaa, 11 Shawwal 1440 | 2019/06/14