Taarifa kwa Vyombo Vya Habari
Kwenye Mswada wa Fedha wa 2025/26 uliowasilishwa bungeni, uliosifiwa na serikali ilioko madarakani kama kichocheo kikubwa cha kiuchumi kwa kuwa hautatoza ushuru mpya au kuongeza zilizopo katika mapendekezo ya bajeti ya mwaka huu, Serikali inaweka mikakati zaidi katika usimamizi wa kodi na kujaribu kuziba mianya hiyo na kufanya ukusanyaji wa kodi kwa ufanisi. Mswada huu unalenga kupunguza hatua za kuongeza kodi na umependekeza msamaha kutoka kwa VAT ya litania ya bidhaa ambazo kwa sasa hazijakadiriwa.
Hizb ut Tahrir / Kenya ingependa kubaini yafuatayo:
Sera za kuwa na bidhaa ambazo zitakazowekewa sifuri zilizokadiriwa, ruzuku na kusamehewa kodi ni dalili za wazi kwamba asili ya maisha duni inatokana na utozwaji wa ushuru. Zaidi ya hayo, hatua hizi mpya zinazopendekezwa ni sera za kibandia tu na dalili zaidi ya taswira inayokinzana ya uchumi wa kibepari. Kwa upande mmoja, kodi inatazamwa kama kujitegemea na upande mwingine, misamaha ya kodi inachukuliwa kuwezesha uchumi! Uhakika wa mambo ni kuwa ushuru ni zana ya kudumisha thamani ya sarafu ya karatasi kupitia ukali wa seriakali na kiini hasa hali ngumu ya kiuchumi.
Mswada huu umeonyesha hadaa ya sera nzima ya kodi katika mfumo wa uchumi wa Kibepari ambao chanzo kikuu cha mapato ya Serikali ni ushuru. Katika mfumo wa Kirasilimali ushuru ni hitaji la kiuchumi ili kuweka hai mfumo wa Fedha za makaratasi na usawa wa biashara na sio kuinua uchumi na maisha ya raia wa kawaida.
Bajeti za serikali ya kibepari huzunguka ndani ya ushuru na kukopa kwa hivyo hakuna ukombozi wala kujitegemea kiuchumi.Ili kuendeleza mzigo kwa mwananchi wa kawaida, serikali za kibepari hulazimika kukopa kwa riba ili kuunganisha nakisi ya bajeti.
Suluhisho msingi la masaibu ya kiuchumi nchini Kenya na ulimwengu kwa ujumla halitapatikana kamwe kupitia ushuru na kukopa mikopo ya riba au kuunda sheria mpya za fedha. Uislamu ndio suluhisho pekee la matatizo yote ya kiuchumi.
Uislamu una utaratibu wa kipekee wa ukusanyaji wa mapato, ikiwa ni pamoja na mapato yatokanayo na mali za umma (kama vile gesi) na uzalishaji wa kilimo (kama vile kharaj), ambayo huingiza mapato bila kukaba shughuli za kiuchumi. Na mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu unagawa rasilimali kama vile nishati, ardhi ya malisho na maji kama mali ya umma. Kwa hakika tunaamini ni Dola ya Khilafah pekee inayotekeleza mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu ambao hautozi kodi zote za kikatili kama vile VAT na kodi ya mapato.
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari Hizb ut Tahrir
Kenya