Mnamo Jumatatu, 17 Juni 2019, habari zilizotawala katika ulimwengu wa Waislamu na duniani kote ni kifo cha Muhammad Mursi aliyewahi kuhudumu kama rais wa Misri (2012-2013) Serikali ya Misri imetaja kuwa chanzo cha kifo chake ni mshtuko wa moyo ingawa familia ya Mursi inashikilia kuwa serikali ya al-Sisi ilichangia kifo chake kwa kumnyima haki za matibabu. Habari hizi zilitamausha Waislamu kote duniani hasa ikizingatiwa kuwa Mursi alikuwa anakabiliwa na kesi mahakamani kuhusiana na shtaka la ukhaini.
Muhammad Mursi anajulikana kutokana na umaarufu wake katika chama cha Muslim Brotherhood kilichoanzishwa mwaka wa 1928 na muasisi wake akiwa ni Hassan al-Bana. Chama cha Muslim Brotherhood kimepigwa marufuku ndani ya Misri kutokana na ulinganizi wake wa kurudisha sheria ya Kiislamu kupitia demokrasia. Kwa kuwa chama hicho kilikuwa kimepigwa marufuku nchini Misri, hivyo basi mwaka 2000 Muhammad Mursi aligombania na kuchaguliwa kama mgombea huru na kuhudumu mpaka 2005. Baada ya wimbi la Mapinduzi ndani ya Misri na lililopelekea kung’olewa madarakani Hosni Mubarak, Chama cha Muslim Brotherhood kikahalalishwa na kisha kikazindua chama kipya kwa jina Chama cha Uhuru na Haki mnamo 30 Aprili 2011 naye Muhammad Mursi akiwa rais wa chama hicho kipya. Muhammad Mursi akashiriki uchaguzi wa Misri 2012 kama mgombea urais na kuibuka mshindi kwa kupigiwa kura asilimia 51.7 dhidi ya Ahmed Shafiq. Alihudumu kama Rais wa Misri kuanzia 30 Juni 2012 hadi 3 Julai 2013 ambapo alipinduliwa na kutolewa mamlakani na Mkuu wa Jeshi Abdel Fattah al-Sisi ambaye ndiye Rais wa Misri sasa.
Hakika Muhammad Morsi alifaulu kuingia mamlakani lakini si kwa kutumia njia ya kumuiga Mtume (saw) na lengo lake likawa si kutekeleza Uislamu kwa ukamilifu wake. Kwa maana nyingine njia ilimuelekeza kizani kinyume chake ni kuwa Ummah ulikuwa wataka kuelekezwa katika nuru kwa kutawaliwa na Shari’ah (Qur’an na Sunnah) na wamiliki wa nguvu (wanajeshi) walikuwa hawako mikononi mwake bali walikuwa chini ya Maagizo ya wakoloni Wamagharibi hususan Amerika. Hivyo basi kwa sababu ya kukosekana nukta tatu msingi nazo ni: 1. Njia ya makosa iliyotumika kuingia mamlakani, 2.Utekelezwaji wa Shari’ah kwa ukamilifu punde tu alipochukua mamlaka na 3. Jeshi kuwa mikononi mwa wasiokuwa Waislamu ikawa ndiyo sababu ya yeye kuyumba yumba na hatimaye kupinduliwa na kutiwa korokoroni!
Hakika katika kifo cha Muhammad Mursi tunajifunza kuwa sisi Waislamu tunatakiwa kuwa makini na tusibebwe na hamasa tunapokuwa na mchakato wa kutaka mageuzi. Hii ni kwa sababu mageuzi ya kimsingi hutegemea fikra/itikadi ya kukatikiwa inayozalisha mfumo na nidhamu madhubuti. Ni muhimu kufahamu kwamba licha ya kuwa sisi kama Ummah hatuna mlinzi na ngao, Serikali ya Kiislamu ya Khilafah inayotawala kwa Shari’ah. Hivyo basi, hatuna budi kuwa na lengo la kuyarudisha tena maisha ya Kiislamu kwa kupitia kusimamisha Khilafah. Ili kufikia lengo ni lazima kurudia njia aliyoitumia Mtume (saw) alipokuwa ndani ya Makkah kabla kuchukua madaraka ndani ya Madinah.
Kwa kutofahamu lengo na kwa kutumia njia ya makosa ya kuingia madarakani hatima yake ni kama yaliyomfika Muhammad Mursi na wengine waliomtangulia. Uislamu ni dini ya kisiasa na kufaulu kwa Waislamu ni mpaka siasa zao zisimamiwe na kiongozi muadilifu, Khalifah ambaye hakufungika na mipaka iliyochorwa na wakoloni. Khalifah ambaye siku itakapo tangazwa kusimama kwa Khilafah atakwenda mbio kuziunganisha ardhi zote za Waislamu na kuwakabili kwa mkono wa chuma madhalimu wote wanaowakandamiza Waislamu duniani kote na wakati huo huo kutangaza Jihadi ya kuikomboa Kashmir na Palestina kutoka kwa najisi Mayahudi.
Enyi Waislamu duniani kote kumbukeni kuomboleza kwenu kifo cha Muhammad Mursi ni ishara kuwa sisi ni Ummah Mmoja na Tunastahili kuwa chini ya Dola Moja na Kiongozi Mmoja, Khalifah. Kiongozi ambaye angelimnusuru Muhammad Mursi kutoka katika mikono ya watawala vibaraka madhalimu akiwemo al-Sisi ambao wanapanga njama kila kukicha ili kuendeleza umwagaji damu za Ummah huu mtukufu wa Kiislamu. La muhimu ni tushikamane pamoja na tufanyeni kazi adhimu ya kurudisha tena maisha ya Kiislamu kwa kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume. Hiyo ni bora kwetu hapa duniani na akhera.
Ali Nassoro Ali
Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kenya
Makala Na.50: Ijumaa, 18 Shawwal 1440 | 2019/06/21