Kuna watu wanapinga au kuhoji pale tunapozungumzia mateso ya Waislamu huko Gaza na kuhimiza majeshi ya Kiislamu yatangaze jihadi dhidi ya umbile haramu la Kiyahudi la Israel. Wanauliza, “Kwa nguvu gani?” au “Mbona huendi mwenyewe Gaza?” Hoja hizi hazina msingi wa kiakili wala kisheria.
Kwanza, ni muhimu kufahamu kwamba ninaposema tuhimize jihadi, siwaambii raia wa kawaida waende vitani. Ninazungumzia wanajeshi wa Kiislamu walio na silaha, mafunzo, na uwezo wa kijeshi, walioko katika nchi kama Misri, Uturuki, Pakistan, na nyinginezo. Hawa ndio wanaowajibika mbele ya Allah kuwasaidia ndugu zao wa Gaza na Palestina kwa jumla. Sasa iweje tukikumbusha majukumu yao, tunaambiwa tunafanya kosa?
Je, lazima mtu awe msemaji wa jeshi ili awe na haki ya kusema ukweli? Je, ni haramu kwa mwanachuoni, mwalimu, au hata raia wa kawaida kuhimiza majeshi ya Kiislamu wayatimize majukumu yao ya kisheria? Ikiwa ninyi mnaona hivyo, basi hamuelewi majukumu ya umma wa Kiislamu. Uislamu unatutaka tuamrishane mema na tukataze maovu – hata kwa viongozi na majeshi. Hiyo ndiyo njia ya umma kuchunga uadilifu na kusimama na haki.
Lakini cha kusikitisha, baadhi ya watu wakisikia tunataja majeshi ya Kiislamu waende kuikomboa Gaza, wanapandwa na jazba. Wanasema, “Mbona hufanyi wewe mwenyewe?” Huu ni ujanja wa kupoteza hoja. Kama ninakemea ufisadi serikalini, je, lazima niwe rais? Kama ninakosoa uongozi wa mashekhe, je, lazima niwe shekhe? Vivyo hivyo, nikihimiza majeshi yatimize jukumu la kijihadi, si lazima niwe mwanajeshi.
Wengine huhoji: “Mbona hayo majeshi hayaoni hayo mateso?” Hili ni swali la kinafiki. Kama majeshi hayo yamezuiwa na watawala vibaraka wasiojali damu ya Waislamu, basi sisi raia tunalo jukumu la kuendelea kuwahimiza, kuwaamsha, na kuwapa shinikizo wajue kwamba Ummah umeamka na haunyamazi tena.
Tunaposema Gaza inahitaji majeshi ya Kiislamu, hatumaanishi misada ya chakula au kauli za kisiasa. Tunamaanisha jeshi la Kiislamu linalokuja na nguvu, silaha, na nia ya kuukomboa Msikiti wa Al-Aqsa na ardhi ya Palestina.
Lakini kwa kuwa ujumbe huu huwachoma wanafiki, wanakimbilia kuufuta, kuupinga, na hata kuudhalilisha. Wengine huanza kejeli: “Kama una uchungu nenda mwenyewe Gaza,” kana kwamba kuwa na uchungu na Ummah ni kosa, kana kwamba kutekeleza faradhi ya kuhimiza jihadi ni ujinga. Ujinga mkubwa zaidi ni wa wale wanaopinga bila dalili, bila hoja, ila kwa misingi ya utetezi wa madhalimu.
Basi tunasema wazi: sisi hatunyamazi mbele ya uonevu. Sisi tutaendelea kuhimiza, kukemea, na kuamsha Ummah. Kwa sababu Gaza haililii dua tu – inalilia majeshi. Palestina haiitaji hotuba tu – inahitaji jeshi la Kiislamu lenye imani na silaha.
Na mwisho, kwa wale wanaojifanya Masalafi wa mamboleo lakini hawataki kusikia habari za Gaza, wasikie haya: kujifanya unafuata manhaj ya Salaf huku ukipinga jihadi ya kuukomboa Msikiti wa Al-Aqsa ni unafiki wa hali ya juu. Manhaj ya Salaf ni kusimama na haki, kutetea Waislamu, na kutekeleza jihadi pale inapolazimu.
Msiwe safu za madhalimu, msikimbie majukumu ya Ummah. Gaza inaita – mko wapi majeshi ya Muhammad?
Ustadh Mahdi Ali,
Mwenyekiti Wa Kamati Kuu Ya Mawasiliano,
Hizb ut Tahrir, Kenya.