Maandamano na Hisia za Gen Z

Maandamano na hisia za Gen Z,ni dhihirisho la kufeli kwa itikadi mbili:
1) Ilmaniya
Itikadi ilojengwa juu ya fikra ya kutenga hukmu Za ALlah Swt na siasa.
Itikadi ambayo,juu yake ni mfumo wa kibepari na nidhamu yake ya utawala demokrasia imesimama.
Itikadi hii,humpa mwanadamu,mwenye mapungufu mengi ikiwemo:

  • Ubinafsi
  • Fikra finyo isoweza kuona mustakabali
  • Kutegemea nguvu na uwezo wa binadamu kuliko muongozo kutoka kwa ALlah Swt

Haya na mengi, mwanadamu ndiye aliyjitwika jukumu la kutunga kanuni za maisha na kumpora ALlah Swt
haki Yake hiyo
2) Itikadi ya kanisa Ambayo tangu mwanzo ndilo lilochangia pakubwa kuibuka mfumo huu, leo pia yadhihiri mapungufu yake. Wanasiasa wa Kenya walihusisha kanisa pakubwa kuomba kura.
Na kanisa licha ya kujitenga kisiasa,likawa mbele kuwapigia debe.
Yaleyale yaliyokuwepo kabla ya mapinduzi ya Ufaransa 1789,ambapo kanisa kwa mapungufu ya mafundisho
yake, yalishindwa kuwanasihi na kuwaongoza viongozi ndio leo yajirudia. Mkoloni alipovamia Afrika,alikuja na biblia mkono mmoja na bunduki mkono wa pili. Wengi wa wamisheni walikuwa majasusi wa kibepari walovaa magwandwa ya upasta na upadri, Kiasi ya kusemwa msemo maarufu ”Where the Cross(missionaries) went,the flag(colonialists) followed.” Kumaanisha[Palipo elekea msalaba(wamishenari) nyuma ake wanakuja wakoloni]
Juzi kushindwa kwa kanisa kulipelekea kuzaliwa kwa mfumo wa kibepari demokrasia.
Hivi sasa kushindwa kwa kanisa na mfumo wa kibepari,kwapelekea wazi Uislam kama suluhu la
kudumu la muozo ulozaliwa na itikadi hizo mbili.
Iwe ni karibu au mbeleni, Lakin ukafiri umebainika wazi kushindwa kumtatulia mwanadamu
matatizo yake.

Jee Waislam mwachangia vipi kuwaongoza waja wa ALlah Swt kuona nuru hio?!!

 

Imeandikwa na Hussein Muhammad

Mwanaharati wa Hizb ut-Tahrir,

Kenya.