Mageuzi ya Baraza la Mawaziri: Mkakati wa zamani Nyuso mpya

Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari

Rais William Ruto amewateua wanachama wanne wa chama kikuu cha upinzani kama sehemu ya baraza jipya
la mawaziri huku maandamano yakiendelea kulitikisa taifa hili la kanda ya Afrika Mashariki. Rais alikuwa
ameahidi kuteua baraza jipya la mawaziri "pana" ili kukabiliana na maandamano ya G-z yaliyoshuhudiwa mwezi mmoja uliopita. Hatua hiyo β€˜inalenga’ kuwezesha upatikanaji wa ajira, usimamizi thabiti wa madeni, kuimarishwa kwa uwazi na uwajibikaji katika matumizi ya pesa za umma.

Tungependa kueleza yafuatayo:-

Masuala yaliyoibuliwa na kizazi cha G-z yamekua ni yaleyale ambayo yamekuwa yakiibuliwa na jamii kwa
ujumla katika historia ya Kenya.Tukiangazia kwa makini matatizo haya, tunaona kwamba bado hayajapata
suluhu ya kikweli bali wanasiasa wamekua wakiyapatiliza na kuyazungusha kwa mzunguko wao muovu wa
kisiasa hatimaye kuyatokomeza kwenye giza totoro. Uhalisia wa hali hii ya kutamausha kamwe wanasiasa
hawatoibadili kwa ajili ya maslahi ya umma, bali tabaka la kisiasa na hata wale wanaoitwa G-z wamefunga
mwito wa mabadiliko kwa dhana kwamba mabadiliko yako kwenye marekebisho ya kikatiba na kubadilisha
wanasiasa.
Tunasema mfumo wa kibepari, zana ya kikoloni inayotumikia kunyanyasa β€˜nchi za ulimwengu wa tatu’ ndio
suala linalohitaji kujadiliwa hapa. Ingawa tunathamini maandamano ya sauti ya G-z dhidi ya IMF na Benki ya
Dunia kama zana za kifedha za kikoloni, hata hivyo, kuna haja ya kuendeleza hisia hizi za kisiasa ili kuelewa
uhalisia ulioko wa mfumo huu wa Kibepari unaotawalishwa kote duniani na Kenya ni miongoni mwa muhanga
mfumo huu
Mfumo wa Kibepari umetengeza urongo juu ya mabadiliko kwa kuyafunga na chaguzi za mara kwa mara,
marekebisho ya katiba na haki ya kuandamana licha kwa yote hayo hakujashuhudiwa mabadiliko yoyote yale
ya kimsingi. Kwa fika hii ya kina na ufahamu huu uliowazi tunasema bayana kwamba watu wapya na wale wa
zamani kwenye baraza la mawaziri ni mkakati uleule wa zamani matokeo yake ikiwa ni yaleyale wala hakuna
mapya.
Tunasema mabadiliko makubwa ni wito kwa Uislamu kama mfumo pekee unaompendeza Mola wa wanadamu… Mfumo ambao unalazimika kurudisha utu wa mwanadamu kama kipaumbele cha kisiasa. Juu ya utekelezaji wake chini ya mfumo wa utawala Khilafah unahakikishia watu maisha mazuri. Uislamu ndio chaguo pekee la kumkomboa mwanadamu kutokana na kufeli huku kwa mara kwa mara kwa mfumo wa kirasilimali,kwani unahakikisha ustawi wa kiuchumi na Kisiasa. Kihistoria, kwa utekelezaji wake, Uislamu uliwanyanyua wanadamu kutoka kwenye minyororo ya utumwa wa kiuchumi na unafiki wa kisiasa.

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari Hizb ut Tahrir Kenya