Mashambulizi ya Kiubaguzi ndani ya Afrika Kusini ni Thibitisho Kwamba Fikra ya Umoja wa Afrika ni ya Uongo!

Ndani ya wiki ya kwanza ya Septemba 2019, kulizuka ghasia na uporaji uliolenga maduka yaliyokuwa yanamilikiwa na raia wa kigeni katika miji ya Jeppestown na Johannesburg. Takribani biashara 50 zinazomilikiwa na Waafrika kutoka katika sehemu nyingine za bara hili na hususan Wanigeria ziliripotiwa kuvunjwa na kuharibiwa katika tukio hilo. Msikiti uliopo katika Jumba la Jozi ulishambuliwa na kopi za Qur’an zikanajisiwa, kila duka lililokuwa katika jumba hilo liliporwa. Ghasia hizo zilisadifiana na mgomo wa waendeshaji magari wakipinga kuajiriwa kwa waendeshaji wasiokuwa Waafrika Kusini. Pia zilisadifiana na uchapishaji wa taarifa ya Shirika la Haki za Binadamu (Human Rights Watch) iliyosema kwamba watu 200 (wengi wao wakiwa ni waendeshaji magari wa kigeni) wameuliwa ndani ya Afrika Kusini tangu Machi 2018. Wakati wa ghasia baadhi ya magari ya mizigo yalichomwa na waendeshaji magari wageni walijeruhiwa katika mkoa wa KwaZulu-Natal.

Mashambulizi ya kiubaguzi yanajirudia kiuhalisia mfano mwaka 1998, raia mmoja kutoka Mozambique na wawili kutoka Senegal walitupwa nje ya gari la moshi lililokuwa linakwenda mbio na mnamo 30 Mei 2013, Abdi Nasir Mahmoud, Msomali alipigwa mawe mpaka kufa pamoja na vitendo vingine vya kinyama na kivurugu vinavyotendewa wageni ndani ya Afrika Kusini! Kwa kuwasha moto zaidi viongozi wa Afrika Kusini wenyewe ndio wanaopigia debe mfano Waziri wa Maendeleo ya Biashara Ndogo wa Afrika Kusini, Lindiwe Zulu ambaye alisema kwamba wamiliki wa biashara za kigeni hawawezi kushirikiana kwa amani na wenyeji wamiliki wa biashara mpaka waweze kuweka wazi siri za biashara zao! [Daily Nation, 08/09/2019]

Yaliyofuata baada ya mashambulizi na vurugu za kiubaguzi yanajumuisha, Nigeria kujitoa katika mkao wa Jukwaa la Uchumi wa Dunia (WEF) huko Cape Town, Muungano wa Mpira wa miguu wa Zambia (FAZ) walifutilia mbali mchuano wa kimataifa dhidi ya Afrika Kusini uliotakiwa kuchezwa Zambia, Botswana ilitoa ilani ya kusafiri na kuwaonya raia wake, Air Tanzania ilisitisha safari zake kuelekea Johannesburg. Kwa upande mwingine, Afrika Kusini ilisitisha kwa muda shughuli za ubalozi wake nchini Nigeria kutokana na mashambulizi ya kulipiza kisasi ambayo yalilenga biashara za Afika Kusini zilizokuwepo Nigeria mfano MTN, Multichoice and Shoprite ambazo zilisitisha uendeshaji wao kwa muda!

Maelezo hayo hapo juu yanafichua kufeli kiukamilifu kwa mfumo wa kisekula wa kirasilimali katika kuwaunganisha watu chini ya bendera ya ubinadamu na badala yake imewagawanya katika misamiati duni ya mipaka ya kikoloni kama utaifa, urangi na ukabila. Hivyo basi imesababisha kutengana na uadui baina ya kaka na dada, wazazi na watoto na jamaa! Mfano wa uovu wa hivi karibuni ni mnamo Jumatano, 26 Juni 2019, Charles Njagua Kanyi, Mbunge wa Kenya Eneo Bunge la Starehe wa chama tawala cha Jubilee alikamatwa kwa mashtaka ya kuchochea ghasia kutokana na matamshi yake ya ubaguzi wa kitaifa dhidi ya wageni (Watanzania, Waganda, Wapakistani na Wachina) wanao endesha biashara na kutawala masoko ya Nairobi. Zaidi ya hayo ni kikwazo cha Saudi Arabia kwa Qatar ambacho kilikata mahusiano baina ya watu wa nchi hizo mbili! Hivyo basi kila raia anajitizama kwa kioo cha utaifa! Kufanya mambo mabaya zaidi ndani ya mipaka ya kitaifa ukabila umepenya ndani ya mujtama! Kwa kuwa mfumo wa kisekula wa kirasilimali umesimama juu ya msingi wa kutenganisha dini na maisha/serikali na kipimo chake cha vitendo ni maslahi na manufaa; basi kushuhudia ubaguzi ndani ya Afrika Kusini, Marekani, Uingereza n.k hakushangazi!

Kwa upande mwingine, Uislamu umeharamisha ubaguzi wa rangi, ukabila na utaifa:

Mwenyezi Mungu (swt) asema:

(يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَاكُمْ مِنْ ذَكَرٍ وَأُنثَى وَجَعَلْنَاكُمْ شُعُوبًا وَقَبَائِلَ لِتَعَارَفُوا إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِنْدَ اللَّهِ أَتْقَاكُمْ)

“Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamungu zaidi katika nyinyi.” [Al-Hujurat: 13]

Mtume (saw) asema:

 (مَنْ قَاتَلَ تَحْتَ رَايَةٍ عِمِّيَّةٍ يَدْعُو إِلَى عَصَبِيَّةٍ أَوْ يَغْضَبُ لِعَصَبِيَّةٍ فَقِتْلَتُهُ جَاهِلِيَّةٌ) ‏

Yeyote anayepigana chini ya bendera ya upotofu, anayeunga mkono ukabila au anakuwa na hasira kutokana na ukabila basi atakufa katika hali ya ujahiliya.” [Al-Nasa’i and Ibn Majah]

Ni Uislamu na utawala wa Kiislamu pekee ambao unarekodi ya kushuhudiwa ya kuangamiza umadhehebu, ubaguzi wa rangi na ukabila na kuwaunganisha watu wa usuli, makabila na imani tofauti tofauti kuwa Ummah mmoja chini ya Dola moja. Aws na Khazraj wa Madina walipigana kwa miongo kadhaa lakini ni kupitia Uislamu ndipo walipounganishwa na kuwapa utukufu kwa kuwa Ansar (waliotoa nusra) na maisha yao yote ya hapa duniani ya muda na ya akhera ya milele kubadilika kuwa mazuri! Zaidi ya hapo uunganishwaji wa watu kutoka sehemu tofauti kuanzia Andalusia (Spain), Sindh (India), Baghdad (Iraq), Damascus (al-Sham/Syria), Al-Quds (Palestina), Constantinople/Instanbul (Uturuki) chini ya utawala wa Khilafah ni ushahidi tosha kwamba utekelezaji wa ukamilifu wa Shari’ah (Qur’an na Sunnah) ndio tiba ya ubaguzi wa rangi, ukabila na utaifa.

Hivyo basi, lau Afrika Kusini na Afrika kwa ujumla wanataka umoja wa kweli, basi lazima wajikomboe kutoka katika mfumo wa kisekula wa kirasilimali kwa kukata mahusiano yao na Wamagharibi wakoloni ambao ndio wanaopigia debe mfumo huo batili ambao unaangamiza watu duniani kwa kuweka kipaombele ubaguzi wa rangi, ukabila na utaifa kwa pazia ya uhuru wa kibinafsi! Njia pekee ya kimsingi ya kuweza kuondosha ubaguzi ndani ya Afrika na duniani kote ni kukumbatia ulinganizi wa kurudisha tena maisha ya Kiislamu kwa kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume; ambayo itakomboa Afrika na Mashariki ya Kati kutoka kwa Wamagharibi wakoloni, Kashmir kutoka kwa washirikina Wahindu na Al-Quds kutoka kwa Mayahudi najisi! Hatimaye kueneza amani na utulivu chini ya kivuli cha Uislamu.

 (وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ)

“Na siku hiyo Waumini watafurahi.” [Ar-Rum: 4]

Ali Nassoro Ali

Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kenya

Makala Na.62: Ijumaa, 21 Muharram 1441 | 2019/09/20