Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Siku ya Jumane tarehe 26, 2019 Raisi Uhuru Kenyatta na aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga walipokea rasmi ripoti ya kamati patanifu (Building Bridges Initiative- BBI). BBI ilichapishwa kwenye gazeti rasmi la serikali tarehe 24 Mei, 2018 kufuatia muafaka wa pamoja baina ya Rais Kenyatta na Odinga baada ya uhasama wa kisiasa ulioibuka kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi August 2017. Kikosi kazi kilichukua maoni ya baadhi ya wakenya kuhusu ajenda tisa ambazo zote kwa ujumla zinazungumzia kuboresha mfumo wa uongozi, mabadiliko ya kiuchumi upendeleo, ufisadi na utangamano.Na mnamo siku ya Jumatano 27,2019 ripoti hiyo ikazinduliwa rasmi ili umma kwa ujumla iwezi kuijadili.
Hizb ut-Tahrir Kenya ingependa kusema yafuatayo:-
Ni wazi kama ilivyoshuhudiwa migawanyiko baina ya wanasiasa hata kabla ya kuwasilishwa kwa ripoti hii, kuna ishara za mapema kuwa mizozo hiyo itaendelea kushuhudiwa zaidi hata baada ya kusomwa kwa mapendekezo ya ripoti hiyo. Hivyo, huenda nchi ikajipata tena kwenye mitafaruku zaidi inayopaliliwa na wanasiasa. Na vipi wanasiasa wanazungumzia suala la kuunganisha taifa ilhali wengi wao kama sio wote hugawanya umma kwa misingi ya kikabila na kimaeneo jambo linalotumbukiza nchi katika fujo kila baada ya uchaguzi!Twapenda hata hivyo kutahadharisha jamii ya Kenya kutotekwa na malumbano hayo huku tukikariri kwamba hakuna urafiki na uadui wa kudumu baina yao bali wote hutetea na kulinda maslahi yao ya kibinafsi na wala sio maslahi ya umma.
BBI pamoja na ajenda zake imetoa taswira mbovu ya hila za viongozi na wanasiasa wa Kidemokrasia ya kuendelea kuteka nyara hisia za raia kwa kuwazushia ajenda za kuwatia tamaa za kirongo.Yasikitisha kuona wasomi na mufakirina ambao hadi sasa hawajaona kwamba tatizo msingi linalokabili Kenya na ulimwengu kwa ujumla ni mfumo wa kibepari na siasa yake ya Kidemokrasia unaongazia zaidi maslahi ya watu wachache (tabaka la matajiri na wanasiasa) huku ikiacha wengi kuendelea kuumia. Na huu ndio uhalisia na ndipo twasema kuwa kubadilishwa kwa muundo wa serikali,katiba na mabadiliko ya kiuchumi huku mfumo wa kirasilimali ukawa bado ni wenye kutawala maisha ya watu ni kuongeza muda wa kuishi na matatizo au kuyazalisha mengine mapya. Na haya ni ukweli uso na shaka kwani miaka tisa tu baada ya kubadilishwa katiba na kuletwa muundo mpya serikali wa ugatuzi bado jamii ya Kenya inaendelea kukumbwa na matatizo chungu nzima.
Twakariri Kenya bali dunia nzima inahitaji mfumo bora nao ni Uislamu ulio na itikadi madhubuti ambayo ndani kuna sheria za MwenyeziMungu SWT Muumba wa wanadamu, ulimwengu na uhai. Kwa itikadi hii ndio serikali imara, mfumo wa kiuchumi na wa kijamii husimamishwa. Aidha kwa kupitia itikadi hii watu huunganishwa juu yake na kuwa umma mmoja wote wakiwa ni waja wanaonyenyekea MwenyeziMungu (swt). Na hivi ndivyo Uislamu ulivyozalisha wanasiasa bora wachajiMungu walioleta ufanisi wa kisiasa, kiuchumi na kijamii kama ilivyoshuhudiwa kwa karne kumi na tatu ndani ya utawala wa Khilafah. Nasi tunaamini, na In shaallah Khilafah itarudi tena hivi karibuni kuongoza tena dunia kwa siasa ya kweli itakayojaza ulimwengu mzima haki na uadilifu.
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari Hizb ut-Tahrir Kenya
KUMB: 1441 / 02
Alhamisi 1 Rabii’ II 1441 H /
28/11/2019 M
Simu: +254707458907
Pepe: mediarep@hizb.or.ke