Mfumo wa Kiuchumi wa Kiislamu ndio kinga pekee ya misukosuko ya kiuchumi ya mfumo wa Kiuchumi wa Kirasilimali.
Habari: Waziri wa fedha wa Kenya Ukur Yatani aliwasilisha bajeti ya Ksh.trilioni 2.7 ya mwaka huu wa fedha ulioanza Julai Mosi, akifafanua mipango ya matumizi ya serikali ikiwemo mikakati ya ukusanyaji ushuru ili kugharamia mapendekezo ya bajeti hiyo. Makadirio yake yamezunguka kwenye mipango ya kupiga jeki uchumi ili kuimarisha hali ya kiuchumi iliyosuasua kwa sababu ya janga la Covid-19. Bajeti hii ilikuwa chini ya kauli mbiu: ‘kuinua uchumi ili kutunza hali ya maisha, kazi, biashara, na kuukoa viwanda.’
Maoni:
Mdororo wa kiuchumi ulioshuhudiwa mwaka 1930 ulikuwa ndio mporomoko mkubwa uliopelekea kushuka vibaya kwa viwango vya riba, kiwango cha juu ya ukosefu wa ajira,na kuibua maandamano na harakati za mapinduzi ambayo yalisababisha utawala wa Kinazi huko Ujerumani hatimaye kuja kwa vita vya pili vya dunia. Msomi wa Kijerumani Joseph Schumpeter akizungumzia mikakati ya kukabiliana na mporomoko huo mkubwa wa kiuchumi alisema: “Hali hii inatupelekea tuamini kwamba kuimarika kwa uchumi kutawezekana tu kama kutakuja kwenyewe. Kwa mabadiliko yoyote yale ambayo kwa hakika yametokamana na mikakati ya kijuujuu, hivyo kazi ya kujikwamua na mtingisho huo mkubwa bado haijakamilika bali inazidisha masuala magumu ambayo hayatatuliwi kwa hatua zilizochukuliwa za kujikwamua ambazo zenyewe zilihitaji kunusuriwa hivyo kutishia biashara kwa janga jengile likiwa liko usoni“
Ulimwengu bado haujaimirika kiuchumi kutokana na msukosuko wa kiuchumi mwaka 2008 na kwa sasa janga la Covid 19 limesukuma uchumi wa dunia nyuma zaidi. Kinaya ni kwamba sera na mikakati ileile iliyotekelezwa, kama vile kuzidisha mzunguko wa pesa (Inflationary) kwa watu ili uwezo wao wa kununua uimarike au kuupunguza mzunguko (deflationary)kwa kupitia kuwaongezea watu mzigo wa ushuru katika kila bidhaa na huduma.Sambamba na hatua nyengine ya kuongeza mikakati ya kuinua uchumi au kuzidisha uchumi wenyewe, mikakati yote imeshindwa kuimarisha upya hali ya kiuchumi. Ni bayana kwamba uchumi wa kibepari ni wenye kukosa sera madhubuti na fikra sahihi za kuimarisha uchumi.
Urasilimali kutokana na misingi yake ndiyo kiini msingi cha majanga ya kiuchumi yanayoikumba dunia siku za nyuma na hadi sasa.Kutojimudu kwake kuokoa uchumi wa dunia kutokamana na majanga yake yenye kujirudiarudia kila mara na kusambaratika kwake kuko wazi kwa watu wote. Kwa kuangalia mtazamo wa kirasilimali kuhusiana na tatizo msingi la kiuchumi unaona kwamba tatizo hilo ni mahijati ya mwanadamu yasokuwa na kikomo na uhaba wa rasilimali, hivyo kwa msingi huu ni kutatua tatizo hili ni kupitia uzalishaji wa bidhaa na huduma. Hili kwa hakika ndio kosa kubwa la mfumo huu lililosababishia umasikini jamii na kuufanya utajiri uzunguke tu miongoni mwa tabaka dogo sana la watu.
Kuhusiana na suala la mfumo wa kifedha, kwa kule kuweka kwake mfumo wa kifedha wa riba unaojaalia masuala ya mikopo na Ubepari ndio umeshindwa zaidi na kuzidisha mizigo ya madeni, ubepari ndio umeshindwa kabisa kiuchumi. Mfumo huu umesababisha watu wengi kuishi kwenye uchochole kwa ule utaratibu wake wa kimakosa kuangalia tu maslahi ya kundi maalum la watu.
Kusoma kwa kwa bajeti za kila mwaka, kupunguza viwango vya riba na kuweka mipango ya kuinua uchumi pamoja na uchapishwaji wa pesa za makaratasi yote haya si chochote ispokuwa sehemu ya matatizo na wala sio suluhisho.
Mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu uko kipekee katika kujua lipi tatizo la kiuchumi na kuratibu vyema sekta ya fedha. Uislamu kinyume na urasilimali unaangalia tatizo la kiuchumi kuwa ni usambazwaji wa rasilimali na hulazimu kutofautisha kabisa masualab ya sayansi ya uchumi na mfumo wa kiuchumi
MwenyeziMungu (Swt):
كَيْ لَا يَكُونَ دُولَةً بَيْنَ الْأَغْنِيَاءِ مِنْكُمْ
Ili wasiwe kinyan’ganyiro baina ya matajiri wenu tu.
[TMQ Al-Hashr:07]
Hii ina maana kwamba awali ya yote kimsingi katika masuala ya kiuchumi, Uislamu huangalia usambazaji wa rasilimali hatua ambayo wanadamu waweze kukimu mahitaji yao kimsingi pamoja na kuchangamsha jamii nzima iweze kuwa na kasi ya uvumbuzi wa mbinu za uzalishaji kuweza pia kukimu mahitaji yao ya ziada.
Kuhusiana na sekta ya fedha, Uislamu unaharamisha mfumo wa kifedha ulio na msingi wa riba iwe ni katika shughuli za watu binafsi au katika ngazi za kitaasisis. Kwa hatua hiyo ya Kiislamu jamii inakuwa ni yenye uhai na uchangamfu katika kuendesha shughuli zake za kiuchumu na kuizuia kukaa tu pasina kutegemea benki ambazo hua miamala yake haina uhakika wowote wa kuimarisha uchumi.
Ili mfumo huu wa Kiislamu uweze kutekelezwa kikamilifu katika nyanja zote za kimaisha ni lazima iwe ni kwa kupitia kusimamishwa tena Al-Khilafah ambayo kihakika ndio serikali pekee ilio na jukumu la kuutekeleza Uislamu kikamilifu.
Imeandikwa kwa ajili ya afisi kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir.
Ali Omar Albaity,
Mwanachama wa Ofisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kenya